Kisa cha mwanasiasa na Parachute | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kisa cha mwanasiasa na Parachute

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Luteni, Mar 25, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kulikuwa na watu wanne wakisafiri kwenye ndege ndogo ya abiria ndani ya ndege hiyo kulikuwa na daktari mmoja, mwanasiasa, Askofu na rubani. Wakiwa angani ndege ilipata hitilafu kukawa hakuna uwezekano wa kutua salama na bahati mbaya kulikuwa na life-jacket 3 tu yaani parachute.

  Kwa vile life-jackets hazikutosheleza wote wanne kukawa na majadiliano ya haraka haraka nani atangulie kuchukua hizo life-jacket na nani abaki,
  Daktari akasema; mimi ni mtu muhimu sana itabidi nichukue jacket moja nitangulie pindi mtakapoanguka niweze kuwahudumia na kuwatibu akachukua na kuruka nje dirishani yakabaki majacket mawili.

  Ikaja zamu ya mwanasiasa kujieleza akasema, kwa vile mimi Taifa bado linanitegemea na ikizingatiwa niliahidi project nyingi ambazo natakiwa kuzisimamia itabidi nichukue jacket moja ili taifa lisije kupoteza mtu muhimu........kwa haraka haraka bila hata kuangalia akakurupuka akachukua na kuruka nje kupitia dirishani.

  Kwenye hiyo ndege akabaki Askofu na rubani, kwa kuona umuhimu wa Askofu rubani akasema kwa vile wewe ni kiongozi wa kiroho chukua jacket lililobaki pindi utakapofika salama huko uniombee kwa Mungu hata kama nikifa kwenye ajali hii roho yangu iende peponi.

  Askofu akamjibu; ubarikiwe usiwe na wasiwasi bado tuna majacket mawili yule mwanasiasa kwa haraka zake badala ya kuchukua life-jacket alichukua joho langu la kiu-Askofu na kuruka nalo nje, Amen.
   
Loading...