Kisa cha Milli Vanilli Rob n Fab

Kisa cha Milli Vanilli Rob n Fab

el nino

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Posts
4,712
Reaction score
5,070
Kwa wale wafuatiliaji wa muziki wa zamani na muziki kwa ujumla basi hawawezi kuacha kulifahamu kundi hili lililozaliwa Ujerumani Magharibi lililokuwa tishio kabisa mwisho mwa miaka ya themanini na tisini mwanzoni...

Kundi hili liliteka spika za Radio na kumbi za starehe kwa kutoa vibao vikali kama kile maarufu zaidi cha "Girl you know ts true", waliendelea kuachia vibao vingine vikali kama "im gonna miss u na Blame it on the rain"

Kama wahenga walivyosema kuwa siku za mwizi ni 40, kumbe manager wa hili kundi "Frank Farian" aliwachukua waliokuwa wanaonekana waimbaji Rob na mwenzake Fab Pilatus na kuwaweka kama geresha tu kwenye video za nyimbo na jukwaani wakati hawakuwahi kuimba nyimbo hata moja..(sababu ya uwezo wao wa kucheza na muonekano mzuri)

Yaani ni sawasawa na leo uje kuambiwa eti Diamond hakuwahi kuimba nyimbo hata moja , nyimbo zake zote alizoimba kuna mtu alikuwa analipwa na Kina Babu tale aimbe then kwenye video , jukwaani, magazetini anatokea Diamond..

Issue nzima ilikuja kustukiwa Baada siku moja kwenye shoo, milli vanilli wakiwa wanaperfom wanazuga wanaimba wao kumbe wameweka playback, saa ngapi cd isigome!!... Ikaanza kurudiarudia kiasi cha kumfanya member mmoja wa kundi kutaka kukimbia jukwaani...

Baada ya kashfa hiyo, milli vanilli waliporwa tunzo yao ya grammy ambayo walishinda as the best new act, kwa aibu waliyoipata Rob na mwenzake Fab, iliwatesa kiasi cha kumfanya Rob aghubike kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya na hatimaye kujiua... ImageUploadedByJamiiForums1441622673.005093.jpg
 
Mkuu haya mambo ya lip syncing yalianza siku nyingi. Huyo huyo producer wao Frank Farian akiwa na kundi la Boney-M pia la huko huko Ujerumani alikuwa akifanya mchezo huo. Wale wanawake watatu katika kundi hilo la Boney-M ni kweli walikuwa wakiingia studio na kuimba. Lakini sauti ya kiume inayosikika kwenye nyimbo zao ilikuwa ikiimbwa na kuwekwa kwenye nyimbo huko studio na mtu mwingine tofauti (producer mwenyewe Frank Farian) na siyo yule member mwenzao (Bobby Farrell) ambaye uwa anaonekana kwenye video zao kama mwimbaji wakati kiukweli alichokuwa akifanya yeye ni lip syncing tu anapokuwa jukwaani. Huyu jamaa alifariki miaka minne au mitano tu iliyopita. Pia kwa masahihisho madogo kwenye hii thread ndugu yangu ni kwamba aliyefariki ni Rob Pilatus na siyo Fab Morvan. Rob alifariki almost two decades ago.
 
Biashara ya showBiz ina mambo mengi sana asee
 
shukrani mkuu... niitaka kuendelea kuelezea baada ya kundi a mii vanili kuvunjwa ikaundwa kundi l lingine ambalo iliundwa na wale waliokuwa wanaimba ukweli... wakaiita The real milli lakini halikutamba kabisa
 
Nakumbuka Father alinunua casette yao 1991 na mpaka leo anayo kwenye collection yake. Nilikuwa naipenda sana Ma Baker ingawa sikujua kilichoimbwa.
 
collection ya boney m
 
Duuuh kitambo sana nlikua napenda sana huo wimbo wa blame it on the rain........girl gonna miss u....oldz zina ladha yake....
 
Back
Top Bottom