Kisa cha kweli:Rafiki aliyefungwa miaka 30 kwa "kubaka",daftari la wageni NECTA likamuokoa kifungoni

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
Huyu ni Rafiki yangu toka udogo,tukiwa shule ya Msingi mpaka Sekondari.Tulikaa pamoja na kusoma pamoja.Namzungumzia rafiki wa kufa na kuzikana.

Duniani kuna visa wakuu,visa hivi visikie kwa jirani lakini visikukute wewe au mtu wako wa karibu.Miaka 10 iliyopita,mwezi kama huu,huyu ndugu yangu alianza taratibu za kukata rufaa ili shauri lake liweze kusikilizwa tena.

Alifungwa kifungo cha miaka 30 gerezani.Kesi yake ilikuwa ya kutungwa na kubambikiwa.Pesa ilitembea na wakubwa wakaisimamia kesi yake.Nakumbuka alivyolia kwa kilio cha nguvu,siku Jaji alipogonga meza baada ya kumuhukumu kutumikia miaka 30 behind the bars!!

Kosa la kusingiziwa kubaka lisikie tu,kweli sio wote walio garezani wana hatia,wengine ni kesi za kusingiziwa.

Kila nilipoenda kumcheki gerezani jamaa alikuwa analia sana.Aliamua kuwa muhubiri na mwimba kwaya wa gerezani,katekista na muongoza ibada mbalimbali mle gerezani.Aliamini ipo siku atatoka,maana alimlilia Mungu wake,toka mawio ya jua mpaka machweo yake.

Baada ya miongozo ya watu wa gerezani(Wafungwa wengi hujua sana taratibu za sheria na namna ya kukata rufaa) jamaa aliamua kukata rufaa.Hoja kubwa ikiwa,siku na tarehe aliyoshutumiwa kutenda kosa,ndio siku na tarehe aliyokuwa Dsm,eneo la baraza la Mitihani akifuatilia "result slip" yake.

Huu ndio ulikuwa ushahidi mkubwa,kitabu cha wageni cha baraza la mtihani,kilionyesha mnamo terehe hiyo,siku hiyo,majira fulani mshitakiwa aliandika jina lake na sahihi yake ktk kitabu cha wageni kwenye lango la Baraza la Mitihani-Dsm.

Kitabu kile kilithibitishwa na Baraza la Mitihani kuwa ni sahihi,na baraza likathibitisha kuwa,tarehe tajwa,na siku tajwa ya mwezi tajwa,majira ya mchana,kitabu kinachoonyesha kuidhinishwa na kutolewa kwa "result slip" kilikuwa na sahihi ya afisa wa NECTA na mchukuaji wa "result slip" ambaye ndio mtuhumiwa.

Ndugu mwema alishinda kesi,sahihi na jina ktk vitabu vya NECTA vilmuokoa kuendelea kutumia miaka 29 iliyobaki baada ya kuwa tayari ametumikia mwaka mmoja jela.Ilikuwa ni siku ya ajabu,ikawa kama ndoto,ilikuwa ni siku ambayo majina na utukufu wote wa Mungu ulitajwa.Siku hii,kwa sahibu wangu,haikuhitaji muujiza wa kuhamisha mlima toka uwanda mmoja kwenda mwingine.Rufaa ile iliyoambataba na ushindi,ulikuwa ni muujiza tosha.

Pesa hudunisha utu,pesa hununua haki na pesa hubadili haki kuwa batili na batili kuwa haki.Sio wote walio gerezani wana hatia,na sio wote hawana hatia.

Sasa ni baba wa watoto watatu,ni miaka kumi na ushee sasa imepita.Kama ilivyo kwa wengine kukumbuka siku yao ya kuzaliwa,kwa ndugu yangu hii ndio siku kubwa ya kukumbukwa maishani mwake.Kila ifikapo,huandaa ibada na sadaka...Kumwambia Mungu...WEWE NI MUNGU WA HAKI.

Imebaki kuwa simulizi,itakuwa historia na baadae hadithi.Kimoja na kikubwa,huwa hatamani kuisimulia hii kwa mke wake,na hadhani kama atakuja kuisema kwa watoto wake.Imebaki kuwa fundo la siri katikati ya mifupa ya kifua chake.

Hii ni habari ya rafiki kipenzi,mjelajela wa kubaka!Ambaye hata kwa uso na sura yake,hudhani kuwa anaweza kutamani kubaka, achilia mbali hata kubaka kwenyewe.Haki mbinguni,duniani ni ubatili.
 
Miaka 10 iliyopita ni kama 2007 au 2006.

Result slip hupewa within one year after NECTA.
Jamaa ni classmate wako. Kwa haraka haraka ni kuwa una age less than 33years.

Mkuu namna unavyoelezea mandege humu JF huwa ninahisi wewe ni above 40
 
Inanikumbusha Paulo na Sila waliomba milango ya gereza ilifunguka na wafungwa wengine wakamtukuza Mungu. Pia Daniel alitupwa kwenye tundu LA simba akatoka salama. Meshaki, Shadrak na Abednego walitupwa kwenye tanuru la moto haukuunguza hats Uzi was mavazi yao.

Haki huinua taifa.
 
Huyu ni Rafiki yangu toka udogo,tukiwa shule ya Msingi mpaka Sekondari.Tulikaa pamoja na kusoma pamoja.Namzungumzia rafiki wa kufa na kuzikana.

Duniani kuna visa wakuu,visa hivi visikie kwa jirani lakini visikukute wewe au mtu wako wa karibu.Miaka 10 iliyopita,mwezi kama huu,huyu ndugu yangu alianza taratibu za kukata rufaa ili shauri lake liweze kusikilizwa tena.

Alifungwa kifungo cha miaka 30 gerezani.Kesi yake ilikuwa ya kutungwa na kubambikiwa.Pesa ilitembea na wakubwa wakaisimamia kesi yake.Nakumbuka alivyolia kwa kilio cha nguvu,siku Jaji alipogonga meza baada ya kumuhukumu kutumikia miaka 30 behind the bars!!

Kosa la kusingiziwa kubaka lisikie tu,kweli sio wote walio garezani wana hatia,wengine ni kesi za kusingiziwa.

Kila nilipoenda kumcheki gerezani jamaa alikuwa analia sana.Aliamua kuwa muhubiri na mwimba kwaya wa gerezani,katekista na muongoza ibada mbalimbali mle gerezani.Aliamini ipo siku atatoka,maana alimlilia Mungu wake,toka mawio ya jua mpaka machweo yake.

Baada ya miongozo ya watu wa gerezani(Wafungwa wengi hujua sana taratibu za sheria na namna ya kukata rufaa) jamaa aliamua kukata rufaa.Hoja kubwa ikiwa,siku na tarehe aliyoshutumiwa kutenda kosa,ndio siku na tarehe aliyokuwa Dsm,eneo la baraza la Mitihani akifuatilia "result slip" yake.

Huu ndio ulikuwa ushahidi mkubwa,kitabu cha wageni cha baraza la mtihani,kilionyesha mnamo terehe hiyo,siku hiyo,majira fulani mshitakiwa aliandika jina lake na sahihi yake ktk kitabu cha wageni kwenye lango la Baraza la Mitihani-Dsm.

Kitabu kile kilithibitishwa na Baraza la Mitihani kuwa ni sahihi,na baraza likathibitisha kuwa,tarehe tajwa,na siku tajwa ya mwezi tajwa,majira ya mchana,kitabu kinachoonyesha kuidhinishwa na kutolewa kwa "result slip" kilikuwa na sahihi ya afisa wa NECTA na mchukuaji wa "result slip" ambaye ndio mtuhumiwa.

Ndugu mwema alishinda kesi,sahihi na jina ktk vitabu vya NECTA vilmuokoa kuendelea kutumia miaka 29 iliyobaki baada ya kuwa tayari ametumikia mwaka mmoja jela.Ilikuwa ni siku ya ajabu,ikawa kama ndoto,ilikuwa ni siku ambayo majina na utukufu wote wa Mungu ulitajwa.Siku hii,kwa sahibu wangu,haikuhitaji muujiza wa kuhamisha mlima toka uwanda mmoja kwenda mwingine.Rufaa ile iliyoambataba na ushindi,ulikuwa ni muujiza tosha.

Pesa hudumisha utu,pesa hununua haki na pesa hubadili haki kuwa batili na batili kuwa haki.Sio wote walio gerezani wana hatia,na sio wote hawana hatia.

Sasa ni baba wa watoto watatu,ni miaka kumi na ushee sasa imepita.Kama ilivyo kwa wengine kukumbuka siku yao ya kuzaliwa,kwa ndugu yangu hii ndio siku kubwa ya kukumbukwa maishani mwake.Kila ifikapo,huandaa ibada na sadaka...Kumwambia Mungu...WEWE NI MUNGU WA HAKI.

Imebaki kuwa simulizi,itakuwa historia na baadae hadithi.Kimoja na kikubwa,huwa hatamani kuisimulia hii kwa mke wake,na hadhani kama atakuja kuisema kwa watoto wake.Imebaki kuwa fundo la siri katikati ya mifupa ya kifua chake.

Hii ni habari ya rafiki kipenzi,mjelajela wa kubaka!Ambaye hata kwa uso na sura yake,hudhani kuwa anaweza kutamani kubaka, achilia mbali hata kubaka kwenyewe.Haki mbinguni,duniani ni ubatili.

Pamoja Na story nzuri bado umetupa somo la kujifunza
 
Miaka 10 iliyopita ni kama 2007 au 2006.

Result slip hupewa within one year after NECTA.
Jamaa ni classmate wako. Kwa haraka haraka ni kuwa una age less than 33years.

Mkuu namna unavyoelezea mandege humu JF huwa ninahisi wewe ni above 40
Siyo lazima awe ni yeye Barafu ndiyo classmate wa mfungwa, soma heading inasema "Kisa cha kweli:"
Weka umakini kwenye heading ndugu utagundua kuwa Barafu anaweza kuwa kaiwasilisha tu kwa niaba ya huyo "classmate"!
Karibu...
 
Wakati mwingine Mungu husimama na waumini wake pale ambapo wanapotaka kudhulumiwa haki zao. Kama mtuhumiwa wa kubambikiwa unaweza kukata tamaa kabisa ukijua sasa nafungwa kwa tuhuma ambazo si za kweli. Halafu kukawepo na ushahidi wa kukuondoa kwenye janga kubwa ambalo labda lingekuharibia maisha yako yote hapa duniani. Tumshukuru Mungu. Mungu Mkubwa.
 
Dah ni vizuri kuwa tunaandika majina yetu kwenye vitabu ya wageni vilivyo katka ofisi mbalimbali maana hauwezi jua litakalotokea mbele.

Tiketi za basi, za Ndege,risiti Madukani, risiti hotelini risiti petrol station, kitabu cha hoteli ama guest, Ni muhimu sana. Yupo Mchungaji mmoja alituhumiwa kutishia kuua huko kijijini mwao mikoa ya Kati. Siku ya tukio alikuwa Katika taasisi moja karibu kilomita 180 Katika Wilaya nyingine. Yeye alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo.

Kikao kilifanyika siku ya jumamosi na Jumapili. Alisafiri siku ya tatu yake yaani Jumatatu saa 5 kwenda makao ya Wilaya kisha saa 8 Mchana basi limchukue aende Mkoani na hatimaye Kurudi kwao kijijini. Hakufika kijijini siku hiyo kwani basi lilifika saa 11 Mkoani. Mchungaji alilala guest makao ya Mkoa.

Alifika kwao jumanne saa 5 asubuhi siku ya tano baada ya kudaiwa kumtishia mwananchi mmoja hapo kijijini kifo Jumamosi iliyopita saa nne asubuhi pale Kanisani kwao. Mchungaji alikuwa amesafiri kuelekea Mkoani siku ya Ijumaa na kulala hapo na hatimaye kuondoka jumamosi asubuhi kwenda kwenye taasisi. Hakuwepo kijijini.

Katika Kesi alitoa barua ya kuitwa kikaoni, tiketi ya kutoka kwao Ijumaa kuja Mkoani, risiti ya kulala gesti Mkoani na kumbukumbu ya kitabu cha wageni. Tiketi ya basi Mkoani hadi kijijini IIlipo taasisi, muhtasari wa kikao cha Bodi Wenye sahihi yake na ile ya Katibu yaani Mkuu wa Taasisi aliyekuwa shahidi wa kwanza. Tiketi ya Kurudi Mkoani na risiti ya guest. Alishinda Kesi Mara moja.
 
Back
Top Bottom