Kisa cha Kaka Jambazi

Kisa cha Kaka Jambazi

naima79

Senior Member
Joined
Feb 27, 2009
Posts
188
Reaction score
115
Kisa kinahuzunisha jana usiku tulivamiwa na vibaka sijui majambazi, nyumba ninayokaa ni kuna nyumba tano but nyumba moja inakaa familia mbili yaan tunajitegemea ni vyumba viwili,jiko na sebule na kiveranda basi bwana wakavamia wakishawasachi wanawatoa nje so walianza kwa wenzetu me nikawasikia nikaficha kiasi kingi cha hela nikaacha laki na nikaficha simu kubwa nikaacha tecno ya zaman na kitochi na line nikatoa ninayotumia nikaacha zisizotumika sana(hapa jifunzeni) sasa wanawavamia wakikuta mke na mume wanawapokonya kila kitu mpaka pete, mimi niko nyumba ya mwisho nashare na mbinti wa miaka kama 22 hana kazi kapangishiwa na libaba linakujaga tunajua tu mume wa mtu ila hatujui ninani..

Sasa wakaja kwangu wakanisachi me nakaa na msichana mwanangu yuko boding wakatutoa nje,wakaingia kwa jirani sasa wakakusanya wakamvua yule mbaba pete, wakaanza kumuuliza bint we pete zako ziko wapi hana cha kujibu wakamtia ubapa wa panga, akawa analia wanamuuliza pete zako ziko wapi? Ikabidi ajiseme me mchepuko huyu anamkewe yaan tulitamani kucheka ila kwa pale tukashindwa wakasema haya we baba mkeo umemuagaje akasema nimewambia nimefuata mzigo kongo, mmoja wa majambazi akasema hawa wanaume ndo wamenifanya me nikawa jambazi shenzi zao baba alitutelekeza hatukosoma sasa nakukomesha mpigie mkeo

Mbaba anatetemeka anampigia mkewe halooo akasema jisemee kua umemdanganya ww malaya umempangishia nyumba, mbaba anavyojisemea yaan kila tukikumbuka tunacheka mke akatulia akauliza haya umempangishia wapi? Mwanaume anajieleza kua wamevamiwa na jambazi anamuamrisha, yule mke akasema weka loudspeaker wakaweka, mkewe akasema kaka jambazi asante naomba wapige picha hao shenzi, wenzake wanamwita jambazi yule Man eeh twende yule man anasema nina hasira niachen maana bila hivi namkata panga basi mzee mkojo unamtoka

Basi akawapiga picha akaomba atumiwe halafu akasema asante sasa baba mtoe hata jicho mwanaharamu huyo,basi akapigwa ubapa tu akaachwa wakaondoka sasa asubuhi wanaona aibu mwanaume kaondoka sijui kimeendeleaje ila nyumba nzima story ni kaka jambazi yaan tunamachungu ila tunacheka maana huyu dda alikua ananyodo jaman saa tano usiku wanaweza wakawa wanafanya mapenz kwennye kibaraza.. Wanaazima tu taa yao tunakereka ila tufanyeje
 
ha ha ha ha et "mie mchepuko dadeki" tu dah kwel inauma kuvamiwa ila kaka jambaz kakomesha mchepuko
 
kwa hizo nyodo, siku moja wangekuja kufanyia mapenzi hadi mlangoni kwenu saa tano usiku..
 
Hahahahaa huyo mke hafai eti asante kaka jambazi aiseee. Kama ni mwanamke wa uswahilini nahisi keshaandaa mdundiko kufurahia fumanizi la jambazi.
 
nokia naomba saa moja ya mkononi...najua unazo nyingi...
f69221e59d4e8a0f6b7e54daa30bc01d.jpg



Njoo uchukue hii
 
Hahahaah mitaa gani hiyo?? Hii ungewapa jamaa wa GPL ingeuza sana
 
Huyu sio kaka jambaz ni kaka kibaka..... mtaani kwetu kibaka ametuharibia.
 
Kaka Jambazi akifeli aka-share hiyo picha, ndiyo inaweza kuwa ticket yake kwenda ndani.
 
Back
Top Bottom