Asante sana kwa kisa hiki, kiukweli kwa Tanzania, kwenye makabila ya asili, Wasukuma ndilo kabila tunaoongoza kwa uungwana, na upendo, Wanaume wa Kisukuma ndio tunaoongoza kwa kupenda, Msukuma hawezi kuwa gaidi!.
Sifa za Wasukuma original chapa ng'ombe, kwenye mambo yetu, tulikuwa tuna nguvu kama alivyo Mtume SAW, hivyo mmoja hatoshi, atateseka bure!, hivyo wanawake wetu hawana wivu, mke mkubwa ndie anatafuta wenzake wasaidiane!. Walipokuja Wamisionari, wakaleta dini ya Ukristo na mauongo yao ya mke mmoja, mababu zetu wengi walishindwa, hivyo mpaka leo mpaka kesho, tupo Wasukuma wengi tumeupokea Ukiristo ila ni majasiri, hatuachi asili!.
Tena kuna utabiri, rais ajaye baada ya Samia ni Msukuma fulani, hivyo Tanzania inakwenda kuneemeka tena!.
P.