quimby_joey
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 390
- 166
jana nilipata wasaa wa kumsikiliza huyu kibaraka wa CCM na serikali yake, Rajabu Kiravu wakati akijibu swali la mwandishi mmoja. Jamaa kwa kujiamini kabisa akasema jamii ya watanzania inafuga wezi na kuwakumbatia, mwizi ambaye anjulikana mtaani kama mtoto wa mzee fulani hata siku moja hawezi kukamatwa, kunyooshewa kidole wala kuitwa mwizi, mwizi ni yule anayetoka mbali ambaye hafahamiki pale. Kiravu alikuwa hajui kuwa kutokana na wao kumfaham Kikwete, na ndiye aliyewaweka pale basi hata kama ameiba kura yeye si mwizi, ila slaa anayelalamika kwasababu ni mgeni hafahamiki ananyooshewa kidole kuwa ni mchochezi anayechochea vijana wafanye vurugu kisa maslahi yake binafsi. jamani tunaburuzwa, haya ni matusi.