Pistol
Senior Member
- Oct 13, 2015
- 194
- 86
Imeripotiwa tarehe 4 hadi 10 mwaka huu jumla ya wagonjwa 651 sehemu mbalimbali nchini na wagonjwa 3 kufariki dunia kutokana na kukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu ulioendelea kushamili kwa kasi kubwa.
Aidha jumla ya watu 13491 wamekumbwa na ugonjwa wa kipindupindu na watu 205 wanapoteza maisha kutokana na ugonjwa huo kwa kipindi cha miezi sita.
Naibu wa Waziri wa Afya Dk.Hamisi Kigwangalla ameitaja mikoa yenye milipuko ya ugonjwa wa kipindupindu ikiwemo Simiyu, Singida, Pwani, Morogoro,Tanga, Manyara, Mara , Arusha, Mwanza ikifuatiwa na mkoani Geita.
Idadi kubwa ya maambukizi ya kipindupindi ni Manispaa ya Morogoro ikiwa na wagonjwa 87, ikifuatiwa na halmashauri ya Morogoro wagonjwa 66, Arusha wagonjwa 50, Singida wilaya ya Iramba idadi ya wagonjwa 40 na mwisho ni manispaa ya Dodoma ikiwa na wagonjwa 33 ,hii ni miongoni mwa maeneo yenye maambukizi ya kipindupindu.
DK. Hamisi ameitaja mikoa ambayo haina maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu mpaka sasa ni mikoa saba ambayo ni Mbeya, Rukwa, Kagera, Kigoma, Lindi, Katavi pamoja na mkoa wa Mtwara.
Na kuendelea kusisitiza kuchukua taadhari kwa kunywa maji safi na salama, kula vyakula visafi pamoja na matunda kunawa mikono baada ya kutoka chooni na kabla ya kula chakula.