Naomba kuwashauri wazazi wote najua vijana wengi hivi sasa wamefunga shule kwa ajili ya mapumziko, na ni wachache ambao wataendelea na masomo kama tution nk. Najua wengi wetu kama wazazi muda mwingi hatupo majumbani na tunakuwa katika shughuli zetu za utafutaji hivyo kuna uwezekano mkubwa vijana wetu kutokuwa na uangalizi wa karibu siku nzima tofauti na walipokuwa shule jukumu tuliwaachia walimu.
Naomba tuzingatie yafuatayo na mengine mnaweza kuongeza...
1. Hakikisha mtoto anapewa au anaandaliwa ratiba maalum kwa siku nzima ili awe bize asiwe mtu wa kurandaranda na kufanya mambo yaliyo kinyume
2. Wasitumie muda mwingi kwenye vitu kama Tv, Kompyuta, simu nk, nk maana huko kuna upotoshaji mwingi Wanapofungua shule walimu wanahangaika sana kuwarudisha katika hali ya kishule.
3. Ikiwezekana msafirishe kwa ndugu zake na vitabu vyake akabadilishe mazingira ya kusoma.
4. Katika kipindi hiki mitaani ndio kunakuwa na kitimtim cha watoto maana hukutana toka shule mbalimbali, malezi mbalimbali, maadili tofauti n.k.