Kipindi cha Urais Kiwe Kimoja

Kipindi cha Urais Kiwe Kimoja

SolarPower

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2011
Posts
223
Reaction score
27
Wakuu

Napendekeza kipindi cha mtu kuwa rais wa nchi yetu kiwe kimoja tu cha miaka mitano tu. Pendekezo hili linatokana na uzoefu tulioupata katika nchi yetu. Uzoefu unaonyesha kuwa nchi yetu haifaidiki na rais mmoja kutuongoza kwa awamu mbili. Hali halisi ya utendaji wa Marais wetu katika vipindi vyao vya pili ni kinyume na matarajio ya wengi.

Wazo la kuwa na kipindi kimoja cha Urais linapendekezwa liende pamoja na haya:-


1. Kila robo mwaka Rais kupitia Bunge awe anatoa taarifa ya kina ya utekelezaji wa mipango ya Serikali na kueleza yale ambayo yatatekelezwa katika robo za mwaka husika.

2. Kila mwaka Bunge liweke vigezo na kupima utendaji wa Rais na Serikali na kupiga kura kama Rais husika anafaa kuendelea kutuongoza au la.

2. Kwa upande wa Wabunge nao kipindi cha Uongozi kiwe kimoja tu cha miaka mitano na wao pia wawe wanapimwa kila mwaka kama ambayo imependekezwa kwa upande wa nafasi ya urais hapo juu.
 
Hata Katiba ya sasa pamoja na ubovu wake haijalazimisha kuwa na Rais mmoja kwa miaka 10......!!!
 
Hata Katiba ya sasa pamoja na ubovu wake haijalazimisha kuwa na Rais mmoja kwa miaka 10......!!!

Nakuelewa Bubona. Ni muhimu hilo la Rais kuongoza kwa kipindi kimoja tu cha miaka 5 likawa wazi ndani ya katiba ya mwaka 2015.
 
Back
Top Bottom