Kipindi cha maisha ni nyumba ni ufisadi nhc

Godwin Mneng'ene

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
215
84
Nafuatiliaga sana kipindi cha maisha ni nyumba, kwa mtazamo wangu waendeshaji wa kipindi cha maisha ni nyumba cha NHC akina Eprem kibonde wanakula fedha za bure tu , kwa sababu shirika la nyumba la taifa NHC lingetakiwa kutumia kitengo chake cha PUBLIC RELATIONS AFFAIRS & CSR chini ya dada Suzan Omar kuendesha kipindi hicho , ama sivyo haina haja ya kuwa na mtu kama yeye kwenye shirika hilo, hivi hawa NHC hawaoni wenzao wa Tanesco wanavyofanya kwenye kipindi chao cha tunaangaza jinsi badra masoud na wasaidizi wake wanavyoendesha kipindi vizuri na kutokana wanaijua vyema taasisi yao kipindi kinaendeshwa vizuri kabisa, tofauti kabisa na hawa akina kibonde nawaona ni wazugaji kabisa wapo kama pazia wanaita tu wataalamu wa NHC ndio wanaongea mwanzo mwisho hata maswali mengine wanayowauliza yanakuwa irrelevant kutokana kwamba hawaijui NHC vizuri.Na mwisho wa kipindi wanachukua chao. hapa mchechu sikuelewi.
Bw Nehemia Mchechu nakushauri mara moja sitisha hili dili ulilowapa akina kibonde mara moja na umtumie Suzan Omar aendeshe kipindi hiki, fedha za kuwalipa akina kibonde utumie kujitangaza kivingine kama vile kwa kubandika posters, lakini kwa tv presentation kama kipindi chako kilivyo cha maisha ni nymba ingekuwa poa zaidi ukamtimia huyo mdada kama hawezi kazi tafuta wenye ujuzi na rellevant education qualifications.
Kuiga sio ujinga waige Tanesco , naamini kutumia idara yako ya Public Relations & CSR haitagharimu fedha nyingi kama unavyowalipa akina kibonde.
Achana na mambo ya CBA hii ni taasisi ya serikali kuwa makini na dili unazowapa vijana wenzako macho mengi huku ,unajitahidi sana kuendesha shirika vizuri ,ila achana na hao akina kibonde wamekuingiza choo cha kike kwenye hicho kipindi na lazima nitaongea na NAO wahoji ili suala.
Any way hii issue kutokana siimaindi lazima nimtonye Mhe Lembeli aiongelee kwenye Bajeti ya mama Tibaijuka asipoiongelea nitawaambia vijana wa kazi waiongelee bungeni.
Siwezi kuvumilia kuona fedha zetu zinaliwa kienyejienyeji kiihivyo
 
Endelea kufanya uchunguzi vizuri. Utakuta Mchechu personally anafaidika vizuri tu na hicho kipindi.
Kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake. ktk dunia ya leo, idara yenye bajeti kubwa na yenye ulaji wa kutisha ktk makampuni/mashirika yote ni marketing! Ndo maana kumezuka PR agencies nyingi zikiwemo za uchwara hapa TZ na kwingineko.
 
Back
Top Bottom