Kipindi cha Dira ya Dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipindi cha Dira ya Dunia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mcubic, Aug 28, 2012.

 1. mcubic

  mcubic JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 10,165
  Likes Received: 4,195
  Trophy Points: 280
  Kipindi cha Dira ya dunia BBC-Swahili kimeanza kurushwa jana kupitia Star Tv kuanzia saa tatu usiku kila siku Jumatatu hadi Ijumaa. Full coverage ya matukio mbali mbali yanayotokea duniani yanaoneshwa, na utangazaji hufanywa kutumia lugha ya kiswahili. Hii ni fursa kwa watanzania kupata habari mbalimbali za dunia kwa uelewa mkubwa kwani baadhi yetu kiingereza kinatupa tabu, na kuona jinsi lugha yetu ya kiswahili inavyosambaa katika dunia hii.

  Moja ya habari ilonisisimua jana ni ile ya mvutano wetu na Malawi wa kugombania mpaka. Habari hii ilipangiliwa vizuri, na kuonesha yale yalosemwa na Mh JK na JB huku mtoa taarifa akitembelea pande mbili za Tz na Malawi zilizo mipakani, huku waliopo upande wa Malawi wakionekana kuongea kiswahili fasaha pia. Habari nyingine ni ile ya kuuawa kwa sheikh mmoja Mombasa aliyesadikiwa kuwa ni Gaidi aliyepanga ulipuaji wa mabomu ulotokea Nairobi miaka kadhaa iliyopita.

  Ni fursa kwetu Watanzania kuiweka Dunia Kiganjani...ukizingatia Televisheni za ndani hutupa kuduchu yanayojiri duniani.
   
 2. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tumekupata mzee. Lakini muda huo huwa nakuwa.... Hivi hakina marudio? Huu mtihani jamani.
   
Loading...