Kipindi cha bunge katiba H.Polepole,Warioba, waliitwa si wazalendo,leo wanatuita sisi si wazalendo!

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,438
14,916
Neno uzalendo linanichanganya,

Walioko madarakani na wenye mamlaka wanapenda kuwaita walio pembeni si wazalendo,na kila wakati wanawasihi wawe wazalendo

Je lengo lao ni kututaka tuwe wazalendo au lengo lao ni kutuambia "msitusumbue na msiwe wakorofi"

Je kuwahoji watawala ni kupungukiwa uzalendo?kudai haki za msingi ni kutokuwa uzalendo?je kutetea nchi yako inapovunja sheria ni uzalendo wakati wewe manzese kila siku unachoma moto wavunja sheria?

Humphrey Polepole alipokuwa anapingana na bunge la katiba aliitwa kibaraka wa nchi za magharibi,hana uzalendo,mzee warioba mpaka akapigwa ngwala na Paulo,Leo hawa akina Polepole wamefuzu wapi kozi ya uzalendo mpaka wanatukosoa wakati wao juzi tu waliitwa si wazalendo?
 
Hii sawa sawa na mchezo wa mpira, akisajiliwa yanga anashambulia goli la simba, msimu ukiisha akahamia simba anavua jezi na hisia zote na kuanza kushambulia goli la yanga, tena kwa nguvu za ajabu. Huyo ndio H Plpl.
 
Saw a na wale nyoka wenye vichwa viwili a.k.a ndumilakuwili,pande zote kichwa cha huyu nyoka kinasema,sasa je kichwa cha huku na kule kina kauli moja?

Maana anayeongea na kichwa cha upande huu kinasema hivi,anayeongea na kichwa cha upande ule kinasema vingine,lakini nyoka ni yuleyule mmoja
 
Waache uhuni huo!
walikuwa wanaficha Suala la ndege yetu ili iweje?
 
Akili kama yako Mtoa maada utaitwa siyo mzalendo mda si mrefu. Unachochea vita na nchi za magharibi zinakupa support hahahaaaa
 
Neno uzalendo linanichanganya,

Walioko madarakani na wenye mamlaka wanapenda kuwaita walio pembeni si wazalendo,na kila wakati wanawasihi wawe wazalendo

Je lengo lao ni kututaka tuwe wazalendo au lengo lao ni kutuambia "msitusumbue na msiwe wakorofi"

Je kuwahoji watawala ni kupungukiwa uzalendo?kudai haki za msingi ni kutokuwa uzalendo?je kutetea nchi yako inapovunja sheria ni uzalendo wakati wewe manzese kila siku unachoma moto wavunja sheria?

Humphrey Polepole alipokuwa anapingana na bunge la katiba aliitwa kibaraka wa nchi za magharibi,hana uzalendo,mzee warioba mpaka akapigwa ngwala na Paulo,Leo hawa akina Polepole wamefuzu wapi kozi ya uzalendo mpaka wanatukosoa wakati wao juzi tu waliitwa si wazalendo?
Wakijibu uniite nije haraka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom