Kipindi bora cha redio cha jioni.

nyamalagala

JF-Expert Member
Jun 5, 2016
744
673
Amani iwe kwenu wana JF.Baada ya upepo uliokuwa unapeperusha ujasiri wa Daud Bashite kutulia,sasa naona harakati zinaendelea kama dawa.
Nikirejea kwenye mada tajwa,nimekuwa msikilizaji wa redio kwa muda mrefu kuliko kutazama Runinga.Hii ni kutokana na shughuli zangu kunipa wasaa wa kuwa karibu na redio kuliko runinga.Wakati niko kwetu mkoani nilikuwa msikilizaji wa redio Kwizera iliyoko Ngara na kipindi nilichokuwa nakipenda sana kilikuwa ni double mix lakini sasa kinaitwa Alasiri.Kwa upande wa Redio free nilikuwa napenda kusikiliza kipindi cha Mambomambo chini ya Juma Ahed Baraghaza.
Sasa niko kwa jiji la Bashite ambapo redio zimejaa sana.Nilivutiwa na kipindi cha Jahazi cha Clouds Fm kinachoongozwa na Kibonde,G.Habashi pamoja na G.Bantu.Kipindi hiki nilikipenda mwanzoni lakini sasa sikipendi kwani kilipata mpinzani ambaye habahatishi.Jahazi walizidisha mizaha na comedy nyingi huku utetezi wa hoja zisizoendana na hoja mezani.Sasa kipindi kinachousuuza mtima wangu ni kipindi cha Ubaoni cha E Fm kinachoongozwa na Mpoki,Seth na Emma Kapanga.
Kilichonivutia kwenye kipindi hiki ni mpangilio wake na sichoki kukisikiliza.Kuna ukurasa wa michezo,kubwakubwa za leo,Ripoti na Mrejesho.Achilia mbali vichekesho vilivyopo E fm jumlisha na vile vya Mpoki ambaye hukikoleza kipindi.Kipindi bora cha redio cha Jioni kwangu ni UBAONI.
Asubuhi navutiwa na kipindi cha uchambuzi wa magazeti cha MAGIC FM.Hiki kipindi ni zaidi ya kile cha tuongee magazeti cha RFA kwani uchambuzi wa magazeti hufanywa kwa utulivu na ubora.
Huu ni mtazamo wangu kutokana na ninavyoridhika na huduma zitolewazo na vipindi husika.Wewe unapenda kipindi gani zaidi.
 
Back
Top Bottom