Wacha nimalizie thread
2. Mafanikio kiroho.
Kila roho inatakiwa iwe na mahusiano mazuri na Muumba wake( tunamwita Mungu)
Mungu wa Wakristo anaitwa "Mimi niko ambaye niko"
Mahusiano hayo yawe kwenye level ya kuwasiliana kama vile unavyowasiliana na mzazi wako wa kimwili kumsikia akikupa directions maonyo nk na wewe hapo kuwasilisha hoja zako naye akakusikiliza. Kutumia nguvu zake kukemea uovu wa Ibilisi juu yako na wengine na kuzishindaa kabisa nguvu pinzani.
Ukiona huwezi kumsikia Mungu anaposema na wewe, jua bado hujafanikiwa kiroho.
3. Mafanikio ya Nafsi yako.
Uhuru wa nafsi ndiyo mafanikio yako.
Nafsi yako ikiwa kifungoni (mateka wa shetani) basi utakuwa unapita kwenye changamoto za kila namna,
1. Utaonewa na karibu kila atakayekutana nawe,utadhulumiwa, utadharauliwa nk
2. Utaugua magonjwa yasiyoelezeka, ajali za mara kwa mara
3. Utafanya kazi kubwa na matunda yake hutayaona.
4. Ndoa na mahusiano yako na watu wengine yatashambuliwa Sana.
5. Kusongeka kwa nafsi ( siku hizi yanaitwa magonjwa ya akili, mfano kutamani kujitoa uhai, fikra hasi kila wakati, kujitenga na watu nk)
6. Kutokuridhika,tamaa iliyopindukia, kushindwa kujizuia matamanio ya kimwili, ulevi na anasa.
7. Kushindwa kufanya mema, kwa maneno mengine hakujua baya na jema,nimeshakutana na mtu aliyekuwa akichagua tu uovu, baada ya kufunguliwa nafsi yake alikiri kuwa alipokuwa akitenda ule uovu alikuwa anashangaa sana akiambiwa kuwa amekosea,amefanya vibaya, alihisi yuko sahihi sasa anaona alikuwa akikosolewa kwa haki.
Na mengine mengi,
Nafsi yako ikiwa huru utaona kuwa ✓unaishi wakati wazungu wanasema (live the moment) mfano ukiona ndege utamwangalia ndege na utamwona ndege na uzuri wake, na siyo uone vitu vingine ndani ya ndege kama kelele, usumbufu, uchafu wa kinyesi chake, ulozi na ushirikina nk
Ukiona mto au ziwa au bahari basi utaona maji mazuri, utaona uhai wa viumbe, utaona utulivu na burudiko, usafiri wa kukutoa mahala kwenda pengine. Hutaona hofu na ajali na vitu kama hivyo.
✓Utayapenda maisha,utayafurahia,utaridhika.
✓Utaijua thamani ya wewe kuwapo ulimwenguni.
✓Magumu utayachukulia kama njia za kufungua fursa mpya.
✓Utaweza kutofautisha zuri na baya.