Kipilimba, Umekubali kuvuliwa nguo?


Uko sahihi kabisa, kwa Mara ya kwanza naona kumbe wakati mwingine unajivisha joho lisilo lako.

Ni kweli kabisa mbinu ya kupambana na anayetaka kugombea au watu wake ni makosa ya kiufundi kabisa, lakini pia yanasababisha watu wahisi kuwa ni aliyeko ndiye anamtumia, na huo ni woga mkubwa.
 
TISS huwa hawafanyi kazi kwa shinikizo,kuna watu wabobezi na wa ana akili za kutisha
Kama Musiba ana kuudhi mpeleke mahakamani kama membe alivyofanya
Wewe ndiye musiba? basi tumekwisha kichaa ekapewa rungu
 
Kwa sasa wanafanya kazi zote za watu wasiojulikana. Wanateka wanapoteza na ni makada wa chama chao kuangamiza mawazo mbadala.
 
Mkuu, ngoja nikupe like nimeona chief Maxence Melo ametoa ya kwake hapo
 
Tanzania Sikh si nyingi itaogelea kwenye bahari ya damu, baadaye itameguka vipande vipande, dhambi ya kutokuheshimu demokrasia itaitafuna nchi
 
Unaweza kumsema kumbe ndiye aliye nyuma yake, haya mambo yana mkono wa idara yote. Sifia zote ukandamizaji wa upinzani, mabadiliko na utungwaji wa sheria za takwimu, makosa ya mtandaoni, sheria ya habari, na sasa sheria ya mashirika ya kujitolea.
Ili kumnyosha mtu anatakiwa asikie sauti yako tu, unalosema kuwa anavuliwa nguo siyo kweli. Baada ya 2020 kutakuwa na vibweka zaidi. Taarifa na sifia zitatoka huko vijijini na watunga sheria ambao watakuwa wa upande mmoja na wachache sana kutoka kwa mamluki wa vyama vya siasa wanaenda kutunga nyongeza ya miaka ya utawala.
Na huyuhuyu huenda akawa mbunge na kuwa waziri wa mambo ya ndani na atakunyosha. Kuna jeshi linaandaliwa kuwamaliza kabisa wapinzani linaitwa green nini sijui, litaua na kuharibu wapinzani waziwazi hasa wenye ushawishi mbele yake mkuu wa idara.
Kwa nini watoa maoni, wenye kutafakari na wenye mawazo mbadala wanapingwa kwa nguvu zote hata kuuliwa ni sawa kuna jambo kubwa acha tusibiri.
 
Musiba anamtukana hadi VASCO na TISS kweli joka wamelifuga linaanza kuwala.
 
Kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake Musiba acha atoe maoni yake siasa ina mambo mengi ukiifatilia utaumiza kichwa usishangae Lissu ukamkuta CCM ndio maisha
Toa yako uone kilicho mtoa kanga manyoya shingoni.
 
Ni wewe kweli umesema haya
 
My Son drink water (mwanangu kunywa maji) naomba niseme neno hapa... Idara ya USALAMA wa taifa ndio kama idara moyo wa nchi... Hivyo utendaji wao kidogo ni tofauti kwakuwa wao ishu zao haziendi polisi au mahakamani bali wao huwa ni backup tu... Kwahiyo huchukua muda mrefu kidogo kuchukua maamuzi fulani japo hili kidogo ni tatizo kwakuwa kuna athari zinakuwa tayari zishatokea
Kama unakumbuka hapo nyuma bash boi alitaka kuivuruga hii idara lakini kilichokuja kutokea wote tulikiona.. Na kuna mengi nyuma yake hatukuyafahamu
Swala la Musiba ambaye kwasasa ni kama msiba wa taifa ni swala la muda tuu kabla hajanyooshwa akanyooka
Hofu yangu ni moja yeyote anayempa jeuri na kiburi Musiba amakinike naye ili asije kumletea msiba mkubwa
 
Kama ana masikio ya kusikia amekusikia loud and clear.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…