Kipigo - Stroke | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipigo - Stroke

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Nov 16, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Kipigo ni nini?
  Pia huitwa ugonjwa wa kuvamia bongo. Hutokea wakati ambapo mishipa ya damu ubongoni mwa mtu huziba na kupasuka na kufanya baadhi ya seli (Cells) za ubongo kufa. Hizi seli za ubongoni zinapokufa, shughuli ambazo sehemu hiyo ya ubongo hudhibiti hupotea. Hizi ni pamoja na uwezo wa kuongea, kusonga, na kukumbuka vitu. Iwapo unazitambua dalili enenda hospitalini haraka iwezekanavyo kwa matibabu. Kupata matibabu haraka kunamaanisha kuwa kuna nafasi bora ya kupona kabisa.

  Ni zipi dalili za kipigo?

  • Kupooza au kufa ganzi kwa uso, mkono ama mguu, hasa kwa upande mmoja tu wa mwili
  • Kuchanganyikiwa kupata shida kuongea au kuelewa mambo
  • Shida ya kuona ukitumia jicho moja au yote
  • Shida ya kutembea. Kizunguzungu au kushindwa kufikiri vizuri na kusawazisha mambo
  • Kuumwa na kichwa pasipo kutambua kiini
  • Kichefuchefu cha ghafla, kuwa na homa na kutapika kwa dakika au hata masaa
  • Kuzirai, kuchanganyikiwa, kifafa ama kuzimia kwa muda
  Unawezaje kuzuia ugonjwa huu?

  • Ni muhimu shinikizo lako la damu likaguliwe mara kwa mara iwapo liko juu kuna uwezekano mkubwa wako kupata ugonjwa wa kipigo.
  • Fanya mazoezi na ule chakula kisicho na mafuta mengi. Pia kiwe na chumvi kidogo
  • Chunguza iwapo mpigo wako wa moyo uko sawa. Utahitaji tiba ya kupunguza uwezekano wako kupata ugonjwa wa kipigo
  • Wacha kuvuta sigara mara moja. Huzidisha mara dufu uwezekano wa kupata ugonjwa huu
  • Iwapo wewe hulewa, punguza kipimo hadi chupa mbili tu kwa siku.
  • Punguza kiwango cha ‘cholesterolÂ’ mwilini na ni muhimu ikaguliwe kila mara
  • Iwapo una ugonjwa wa Sukari, dhibiti na uchunge sana aina ya chakula unachokula.
  • Iwapo una shida na kuzunguka kwa damu mwilini, tibiwa.
  Unatibuje ugonjwa wa kipigo?

  Iwapo una mojawapo wa hizi dalili, hata kama hazisababishi uchungu au zikitokea hupotea haraka, enenda hospitali ukatibiwa haraka na mapema unaweza kudhibiti kuharibika kwa ubongo wako. Iwapo kuna uzibaji au kuvuja kwa damu, daktari atajaribu kuvitibu kwa dawa au upasuaji.

  Watu wengi ambao wamewahi kupata ugonjwa wa kipigo, huwa wanalazimika kujifunza kutembea tena. Mwanzoni, wanapoendelea kupata nafuu huwa hawakumbuki vitu ama hata wao hushindwa kusongeza baadhi ya sehemu za miili yao. Kupona huchukua muda, ni kibarua, huhitaji msaada na utulivu. Watu wengi huhitaji utunzi maalumu. Jifunze mengi zaidi kuhusu kupata nafuu.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Dr Mzizi Mkavu uko deepu kwenye hayo yahusuyo afya mzee ...

  Lakini, vipi unaonaje wazo la kujizuilia mbali kipigo kwa watu kujijengea kawaida ya kufanya mazoezi ya mwili kwa gharama nafuu kama vili watu wazima kujijengea kawaida ya kukimbia, kuruka kamba, na hata kujidhibiti wenyewe kutokuwa pipa la taka la kila lilikalo ????
   
Loading...