Kipigo cha Yanga chageuka neema Coastal Union

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,310
Klabu ya Soka ya Coastal Union ya Tanga imeanza kuonja 'tamu' ya ushindi baada yakuzawadiwa fedha taslimu kiasi cha Shilingi Milioni Mbili na mfadhili wa timu hiyo, Alhaji Salim Bajaber ambaye pia ni mmiliki wa Kiwanda cha Unga cha Pembe ambao ndio wadhamini wa timu hiyo.

upload_2016-2-3_12-7-47.png

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union,Salim Amiri akimkabidhi fedha Nahodha wa timu hiyo, Hamis Mbwana “Kibacha”

Coastal Union walijikuta wakipewa motisha huo baada ya kuwafunga Yanga ya Dar es Salaam goli 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Makabidhiano hayo yalifanyika jana Februari 2, chini ya usimamizi wa wa Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo kwenye Mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Poppatal ya Jijini Tanga.

Chanzo: Idara ya Habari, Coastal Union
 
Back
Top Bottom