Kipi zaidi kati ya udongo na maji?

Yuyo Ahumile Shamalendi

JF-Expert Member
Mar 10, 2018
993
782
Wakuu tupo pamoja.

Moja kwa moja kwenye mada.
Naomba tubadilishane mawazo hapa Kuhusu hivi vitu.

Katika matumizi ya mwanadamu au viumbe hai tunaona kua udongo umemiliki kila kitu duniani, nikimaanisha kua kila kitu kinachomilikiwa na mwanadamu au kiumbe hai kimetokana na udongo au kimetoka kwenye udongo ingawa vingine vimepitia hatua nyingi tangu kutoka kwenye udongo mpaka kutufikia sisi.

Na vile vile maji nayo yamechukua nafasi kubwa kwenye viumbe hai.

Sasa swali hapa ni kipi zaidi ya Udongo au Maji, kinachotakiwa hapa wakuu ni kukizungumzia kitu ambacho ni zaidi halafu na sababu zinazopelekea kiwe zaidi ya kingine.

Nawasilisha, wakuu karibuni.
 
Back
Top Bottom