Mbao za Mawe
JF-Expert Member
- May 11, 2015
- 23,372
- 54,909
Kila siku tunashuhudia kukua kwa mitandao ya kijamii katika mawasiliano na mara nyingine imefika wakati mitandao hii imekuwa ikiweka wazi maisha ya watu katika jamii.
Ila kwangu mimi najiuliza kipi kinafanya kuongezeka kwa picha za utupu katika hii mitandao tunayotumia? Maana nimezoea nikiona watu wanashirikishana picha za vyakula wanavyokula ila naona sasa hivi hii tabia ya kuanza kushirikishana picha za utupu ikizidi kukua kwa kasi sana sijui nini tatizo!!
Kwa miaka ijayo nahisi hiki kitu kitakuwa zaidi ya sasa kwani zamani nilizoea kuona picha hata kama ni za utupu zilikuwa za mataifa ya nje ila leo hii ni za hapa hapa nchini tena mwananyamala, wanawake kwa wanaume wamekuwa na kasumba ya kutumiana picha hizi na kusambazwa mitandaoni !
Sijajua ukweli juu ya kushamiri kwa vitendo hivi siku za hivi karibuni au tuseme hii nayo ni njia mpya ya kutafuta kiki maishani ?
Au watu wapo kwenye Biashara zao wanauza bidhaa mtandaoni maana nahisi mtu hutuma utupu wake uyole ili atangaze biashara kwa wateja wake.
Siku za mbeleni tusije shangaa kukuta picha za watu unaoheshimiana nao za utupu mitandaoni