Kipi kianze, kujenga nyumba au kununua gari la kutembelea?

Unaweza kuanza na vyote pia... Ni wewe tu

20221018_134942.jpg
 
Hasara kuu ya nyumba inayo nigharimu mimi HAIHAMISHIKI ila naona ni much better kuliko hasara za gari ya kutembelea

Sent using Jamii Forums mobile app
Kipato, wapi alipo,na nature za biashara zake ndizo zitatathmini mtu ajenge nyumba au anunue gari,mfano mtu anaishi dar na kipato chake mfano ni mil. Moja kwa mwezi ni bora anunue gari ili aliingize kweny mzunguko kwa kibiashara halafu baadae akimeki mane ujenzi ufuate
Ujenzi wa nyumba unahitaji pesa,ila ujenzi wa banda unahitaji hela.
 
Inategemea na kipato chako. Zamani kumiliki gari ilikuwa Kama anasa tu, lakini kwa Sasa kumiliki gari ni hitaji la msingi Kama ilivyo tu kumiliki nyumba.. Hivyo, Kama uko vizuri fanya vyote.

Acha kufananisha mmiliki wa nyumba na mmiliki wa ki baby walk
 
Ushauri wangu kama unataka vyote first nunua kiwanja kusecure sehemu ya kujenga then nunua gari ..maana kujenga sio kazi rahisi ni pesa ndefu zaidi ya gari maana nyumba angalau 80-90 mil ndo standard ila ukiwa na 25 mil unapata gari nzuri ...Nina maana angalia pia na umri huu ujana ndo unaweza kutumia gari kwa vile bado unahangaika mara kazini mara pale haswa kama hapa dar kushika Bomba daily na ule mminyano unafika job shati kama halijapigwa pasi perfume imepoa kwa mminyano..

Kwa ununue gari ni kwamba kwa sasa una mihangaiko kama Kijana ya kutafuta maisha ila ukifika uzeeni ambao ni umri wa kustaafu hautakuwa na mambo hapo ndo utakuwa na uhitaji mkubwa sana wa kukaa nyumbani basi hapo nyumba ni muhimu sana kwako..

Kama umepanga sehemu nzuri tafuta kiwanja hata porinu huko mpaka ukitaka kuja kujenga pashakuwa mjini na una pesa za kutosha ,raha ya kujenga uwe na pesa ndefu so unaacha bima na bati juu mpaka uje kupiga finishing kwa pesa za mawazo mpaka unakuja kuhamia ramsi bati zishaanza kupauka.
 
Ninachokiona mm umasikini ndio unasumbua wengi wanaoshabikia gari nikwasababu hawakuyakuta kwenye familia zao na walikuwa Kwa shida hivyo starehe walizotakiwa wazifanye wakiwa wanasoma huko za kubebea mademu,pombe wao wanawaza wakiwa wameanza maisha rasmi
Kama hawakupata utotoni kwa hiyo wafanyeje, waendelee kula msoto hata kama uwezo wanao....pia watoto wao na wenyewe wale msoto?

We ndio una akili za kimaskini.
 
Back
Top Bottom