Kipi bora kununua Hiace mpya kwa 30M ama kuchukua Tata Marcopolo kwa mkopo

Kuna uzi ulikuwepo jukwaa hili pale juu kabisa ukizungumzia biashara ya usafirishaji na changamoto zake, ulikuwa mzuri sana. Ulieleza haya mambo kinagaubaga.
Ila nasikitika nimeutafuta sana siuoni na pale juu haupo.
 
Mkuu @kaisangora , uzi wenyewe unaozungumzia maswala ya biashara ya daladala nimeutafuta nimeupata. Moderetaor waliutoa pale juu, ila nimeuufufua umeanza kuandikwa na mkuu anonymuz.
Natumai kuna kitu cha kujifunza ingawa uzi ni wa zamani.
 
Abiria hawakosekanag mkuu hata siku moja,..uamue kupiga route ndefu, yaan mfano ukitoa ubungo , hakuna kupakia wala kushusha mpaka kahama, kuna wakati kutakua na upungufu, ila kama njian unabeba na kushusha, pesa ipo mzee

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu huwa napita sana hiyo njia nafanya route mara nyingi sana kutoka dar kwenda mwanza, dar kwenda chato na bukoba kwa gari ndogo abiria ni wa tochi halafu raha halafu coster uipige route ndefu upakie kama daladala hiyo safari itakuwa ndefu sana
 
TATA ukipiga shamba hukosi kulaza 300,000/= kwa siku tena huwa gari linapumzika kuliko mikimbizano ya daladala jijini DAR. Ukiweza nenda Morogoro upate route ya Moro - Kisaki ama Moro - Mahenge. Pia route ya DAR to Kisaki ina abiria wa kutosha
Moro-Mahenge asiende hiyo route itamcost.
Chukua Toyota Coaster au Nissan Civillian.

Kama unataka usiumize kichwa sana nenda Malawi kachukue body 2 za Toyota DCM kule utapata kwa bei ya kutupwa ukija huku utatafuta kadi ya gari iliyopata ajali na utazifungia engine za 3B au 2H.

Au mtafute mtu mwenye DCM mvue hapa hapa Tanzania unapata kwa bei ndogo na itapiga kazi muda mrefu.
 
Angalia tu gari gani nyingi dar, ni tata ama eicher, then decide eisely
Thank you mkuu ubarikiwe. Unaweza ukanipa muda wako kwa kuweka nyama kidogo ni kwa sababu gani na wengine ili tujifunze kwa kuelezea tofauti ya tata na eicher. Nina imani tumezaliwa hata hatuwajui wazazi ila tumekuwa wakubwa tukawajua. Am sure everything is learnable kikubwa uwe tayari kujifunza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu huwa napita sana hiyo njia nafanya route mara nyingi sana kutoka dar kwenda mwanza, dar kwenda chato na bukoba kwa gari ndogo abiria ni wa tochi halafu raha halafu coster uipige route ndefu upakie kama daladala hiyo safari itakuwa ndefu sana
Mkuu..sio lazima upakie kila kituo..au kushusha, unaangalia vituo muhim kama vinne au vitano

Unapiga fresh tu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashangaa sana watu ambao wana mtaji wa milion thelathin halaf wanataka wawekeze wapate 50k kwa siku..daaah hatari sana. Ngoja nikufumdishe biashara ndugu japo sikulazimishi.. Uza nguxo za umeme,,ile miti ambayo haijawa kua treated bado,kuna soko la uhakika hela mkononi.. Mtaji wake wa kwanza hauzid milion tatu,na faida yake sio chini ya milion na laki nane kwa kila trip,kwa hyo ni ushapu wako ukikata miti ya kujaa semi tatu kwa mpigo it means utapata milion na laki nane mara tatu...ambayo 5,400,000. Ukifanya mara mbili kwa mwez ukatoa gar tatu tatu unakula milion 10.8. Hakuna TRA,hakuna kununua spea wala hakuna kusikia gar imeandikia huku..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
atakufa kwa pressure.
labda angetafuta dsm za mzee wa casri wa gongo la mboto
Moro-Mahenge asiende hiyo route itamcost.
Chukua Toyota Coaster au Nissan Civillian.

Kama unataka usiumize kichwa sana nenda Malawi kachukue body 2 za Toyota DCM kule utapata kwa bei ya kutupwa ukija huku utatafuta kadi ya gari iliyopata ajali na utazifungia engine za 3B au 2H.

Au mtafute mtu mwenye DCM mvue hapa hapa Tanzania unapata kwa bei ndogo na itapiga kazi muda mrefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa itabidi akonde miaka 2 na ule mwaka wa 3 ndo arudishe afya
Mkuu naona watu wanaongea wasiyoyajua kila mtu ni Mjuaji tuu lakini ukweli wa mambo hawayajui

Mie naomba nikupe experience yangu, nilichukua mwezi wa tatu Tata 105M. Unalipa 30% ambayo ni kama 30.15M. Bima kubwa 10.6M. Wanakukopesa 73.5 interest in 23% Jumla inakuja 92M kwa mwezi unarejesha 3.8M. Sasa mie niliipeleka mkoani inapiga route mkoa to mkoa baada ya kutoa matumizi yotee mafuta na posho inalaza 150k mpaka 250k siku hazilingani. inatembea masaa 8 mpaka tisa kwa siku gari haichoki tofauti na Dar inatembea zaidi ya masaa 15. Kwa mwezi unauhakika wa kulaza 4.5M mpaka 6M

Gari ikiwa bado mpya service ni oil tuu kila baada ya wiki inategemeana na urefu wa safari yako Max service Km ni 7000, Tairi na break baada ya muda kwa sababu inatembea kila siku.

Kila biashara ina changamoto watu wasikutishee kwani wanaoifanya wanawezaje. Tafuta dereva Mzuri konda weka ndugu yako unaemwamini utatembea kifua mbele. Baada ya miezi 24 unamaliza mkopo wako unaendelea kula maisha au uanweza kuuza hata 40M unarudisha hela yako. Gari ukiitunza vizuri inaweza kufanya kazi hata miaka zaidi ya 10.

Angalizo hii biashara hela ya hesabu usiende kulia bata inatakiwe uiwekee kwenye account na hyo account usiizoee fanya kama hauijuii kabisa maana gari muda wowote inaweza taka hela afu we hela ushalia bata ndo hapo unaposikia mtu amepaki gari. Siku zote hela za biashara usiziingize kwenye matumizi yako binafsi au ya nyumbani acha biashara ijiiendeshe yenyewe huku matumizi yako unayatoa sehemu nyinyinge

Ukihitaji Contact za Tata karibu. All the Best

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana mkuu hiece kutoka japan kama sikosei kwa sasa super roof ni 30+ , pank 28+ sina uhakika na hizo bei lakini siko mbali na hapo. Mimi nilikuwa namshauri jamaa anunue zilizopo hapa nchini ambazo hata kwa chini ya 10ml unaweza kupata.
Mkuu nataka ninunue hiace,nataka niiweke iringa,Umeongelea 20M,naweza kupata hiace kwa hiyo bei kuagiza kutoka japan?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
alibadilisha biashara, ila muda c mrefu atarudi.
Yule bwana DCM anakuuzia hadi 30M na unaondoka moyo mweupe.
Anauza DCM kwa million 30 kwa kigezo kipi anakuwa ameisuka sana body au yeye anafunga engine ipi mpaka auze bei kubwa.

Malawi watu walizifata na bei ilikuwa inacheza kwenye million 6,7,8 miaka ya 2009.
 
Back
Top Bottom