Kipi bora kununua Hiace mpya kwa 30M ama kuchukua Tata Marcopolo kwa mkopo

Nenda Kahama kafungue Plant ya dhahabu ambayo itagharimu 30millions tu na baada ya miezi sita kama hujaanza kuzungumza kifaransa utaniambia

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii sijawahi iwaza.fursa ni nyingi na zote unatoka.kikubwa uifumanie moja na utulie nayo na uijulie. Ni kama kuipata mke safi mana wanawake ni wengi na wote wana uzuri wao.
Anyway thank you
 
Bavaria,
Mkuu habari. Nina mpango wa kufungua hardware kwa mtaji wa M10 mkoani naomba ushauri wako ni nn chakuanza nacho na wapi naweza pata vifaa vya jumla. Natanguliza shukrani
 
Nilipiga hii kazi mwaka 2018 karibia iniue kwa pressure,,sio kazi rahisi kihivo. Niliingia ludewa huko kisha nikapeleka nguzo mtwango kwa mateso mengi,,nilirudi home nimechakaa kama nimetoka kwenye vita Vietnam huko. xav bero,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tata ukinunua cash ni mil99, ukinunua kwa mkopo ni mil113, unalipa kwanza mil30 alafu ndio unamalizia taratibu, na zile gar zimetembea km 20,000, tata engine tu, body wanatengeneza marcopolo,nunua coaster mayai mkuu
 
Nashangaa sana watu ambao wana mtaji wa milion thelathin halaf wanataka wawekeze wapate 50k kwa siku..daaah hatari sana. Ngoja nikufumdishe biashara ndugu japo sikulazimishi.. Uza nguxo za umeme,,ile miti ambayo haijawa kua treated bado,kuna soko la uhakika hela mkononi.. Mtaji wake wa kwanza hauzid milion tatu,na faida yake sio chini ya milion na laki nane kwa kila trip,kwa hyo ni ushapu wako ukikata miti ya kujaa semi tatu kwa mpigo it means utapata milion na laki nane mara tatu...ambayo 5,400,000. Ukifanya mara mbili kwa mwez ukatoa gar tatu tatu unakula milion 10.8. Hakuna TRA,hakuna kununua spea wala hakuna kusikia gar imeandikia huku..

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ngozo moja ya umeme nitakua nimenunua bei gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daladala ni sawa na jini mufilisi usipokuwa makini Ina walaji wengi kuanzia nguo jeupe,yono,breakdown,mafundi,sumatra,kwa uchache ukiona Simu ya konda sawa na simu ya mtoa roho.
Mimi nadhani tatizo ni tabia ya watu kuigana kwenye utendaji wa kazi. Ukiwa na daladala na ukaendesha biashara yake akama ilivyo desturi ya wenye daladala wote ni lazima utalia. Wengi utakuta wanampa dereva na konda halafu wanamwambia nataka kiasi fulani kwa siku... njia hiyo ni lazima itakuumiza na gari litakongonyoroka mapema sana. Njia nzuri ni mtu kubuni njia ya utendaji kazi tofauti. Ni bora umiliki gari moja ambayo utakuwa unaendesha au kukusanya fedha mwenyewe kuliko kuwapa watu wafanye wanavyotaka.
 
taja njia nzuri kwa mtu ambaye ni mwajiriwa au ana kazi nyingine ukitoa hyo ya daladala
 
taja njia nzuri kwa mtu ambaye ni mwajiriwa au ana kazi nyingine ukitoa hyo ya daladala
Unaweza kuwa na ndugu/rafiki mwaminifu labda? Na usiniambie hakuna ndugu/rafiki mwaminifu kwani mimi ninao (japo vile vile ninao wengine walaghai sana)! In short ni kuwa sisi waafrika wengi ni wezi. Hivyo biashara kama gari ni ngumu sana (lakini inawezekana) kupata mtu mwaminifu.
 
Ndo hapo kuongea nao vizuri mkuu ama hunielewi bado. Ama sio ni mkenya nayeongea naye
Futa habari za rushwa kwenye biashara. Acha nature ifanye kazi yake, amini tu kuwa Hiace hazikutakiwa. So, usifikirie hiace kwa Mwanza
 
Back
Top Bottom