Hii picha inaakisi kabisa fikra zangu. Kimsingi wazenji wako salama kwa sababu tupo nao, tukijitenga kama wachache wao wanavyotaka, wataanza kutengana wao kwa wao kati ya wale wenye udini na wale waliberali. Msingi wa hoja za UAMSHO ni kwamba sisi bara tunawazuia kupata misaada toka nchi za kiislamu wakati wao ni waislamu kwa nini wasisaidiwe na waislamu wenzao???(OIC).Vile vile huku bara kuna mambo ya kikafir kama MASHINDANO YA UREMBO (UMISS) kama tupo nao kwenye muungano wataonekana wameridhia mambo hayo ya kikafiri. Na hoja nyingizezo nyingi zisizokuwa na mashiko. Kazi kwao sisi yetu macho.