Kipanya hapa alikuwa anamaanisha nini?

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
kp04012016.jpg
kp04012016.jpg


Yaani anamaanisha jamaa ana vuruga vuruga na kukaba watu roba ila wananchi bado mambo magumu na hakuna dalili hata ya maisha bora kwa kua bomba halina hata dalili ya kuunganishwa ili litoe maji?

Au nyie mmeelewaje wadau...
 
pombe na mawaziri wake wanatafuta sifa kwa watendaji hili hali bado wananchi wanataabika na kero mbalimbali.
 
Sinema,mbwembwe..maigizo ya kutisha..kushtukiza..hayana tija kwa mtanganyika wa kawaida..
 
hats kipindi kile tulianza na kasi mpya Ari mpya je? Ilidumu kwa muda gani?
 
...tuwape muda! sisi wenyewe tulisema hazina hakuna kitu...
 
Raisi, mawaziri badala ya kushuhulika na kero za wananchi, wamebaki kushuhulika na viongozi wa taasisi bila kujali tija kwa wananchi.
 
hata Roma haikujengwa kwa siku moja. huwezi kushughulikia kero za wananchi ukazimaliza bila kushughulikia na kutokomeza ufisadi
 
Mkuu anasoma sana vimemo halafu anachukua hatua panga pangua mwisho wake sijui ni nini? Wananchi wanasubiri hayo mabadiliko lakini safari bado ni ndefu. Baraza la mawaziri makatibu wakuu bado ni mzigo kwa taifa. Gharama zinazoigharimu taifa ni ile ile kilichobadilika ni namna ya matumizi. Punguza gharama ni kupunguza idadi ya viongozi hawa watu wanalipiwa nyumba wanakuwa na magari mawili kama si matatu yanayohudumiwa na serikali. Mbona wenzetu walioendelea hawana utaratibu huu wa kulipiwa kila kitu? Sasa mshahara wa nini kama serikali inakugharamia kila kitu? Serikali ijitumbue majibu makubwa kwanza kabla YA kushinda na kukimbizana barabarani pasipo tija.
 
Back
Top Bottom