Kipanya ana maana gani hapa?

Kipanya ana maana gani hapa?

Newword

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2019
Posts
326
Reaction score
304
Nimechunguza hii katuni sijan'gamua kitu.Hivi Masoud anatoa Ujumbe gani hapa??
IMG_20191223_173929.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
🙄🙄🙄🙄 na mimi pamoja na kutoa kote Macho sijaambulia kitu ,wacha tuwasubiri wenye Akili kubwa wasaidie kung'amua hili.
 
Yaani hapo ni ile kauli "Kauka nikuvae, pasuka nikushone"

Hii inahusu watu wenye nguo moja tu, yaani ikichafuka inafuliwa na kuvaliwa tena.

Sasa Chadema viongozi wao ni kama "kauka nikuvae"/Viongozi ni wale wale kauka nikuvae chanika nikushone.

Licha ya Chadema kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi, viongozi waliochaguliwa ni wale wale.

Kanzu mpya sheikh yule yule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeelewa kwa kulinganisha na misemo ya kiswahili.
1. Anika nguo mwezini
2. Twanga maji kwenye gunia
3. Piga deki barabara
4. Chota maji kwa tenga. N.k
Mikakati ya CDM haina mashiko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona ni fumbo nyanya kabisa. Kauka nikuvae.

Kwamba chadema hawana mtu zaidi ya Mbowe wa kuchaguliwa kuwa mwenyekit?

Unajua nguo 1 inafuliwa usiku ili kukicha uivae

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu ikiwa hawajavunja Katiba katika kuendesha Chama sioni tatizo la anae ongoza kuwa Madarakani kwa kipindi flani,ni ana aminika/aminiwa na walio mchagua.Ikiwa ndivyo hii Katuni haina maana kwa upande wangu labda kama pana tafsiri nyingine.
 
Wenzao wanaanika juani wao wanaanika gizani dah
 
Nimeanza kupata mwanga kidogo
Yaani hapo ni ile kauli "Kauka nikuvae, pasuka nikushone"

Hii inahusu watu wenye nguo moja tu, yaani ikichafuka inafuliwa na kuvaliwa tena.

Sasa Chadema viongozi wao ni kama "kauka nikuvae"/Viongozi ni wale wale kauka nikuvae chanika nikushone.

Licha ya Chadema kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi, viongozi waliochaguliwa ni wale wale.

Kanzu mpya sheikh yule yule.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni usiku ang'avu na mwana CDM amefua tayari nguo yake tayari kwa mapambazuko mapya ya harakati ya chama chake.

NB;
Sidhani kama kwa mvua hizi zinazoendelea Tz, mikoa yote mvua zinanyesha bila kupingwa...sidhani sidhani kama nguo iyo itakauka over night.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom