Kipanya aibuka na traffic

Kipanya aibuka na traffic

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
122,521
Reaction score
96,267
Msanii matata wa katuni almaarufu kama Kipanya ameibuka na wana usalama barabarani.

Binafsi nimeshindwa kuelewa nini amemaanisha kwenye ujumbe wa picha kwa jamii, mwenye uelewa tafadhali atujulishe maana elimu haina mwisho.

Screenshot_20210128-094728.jpg
 
Anamaanisha kuwa kuna hatari ya polisi kuanza kukusanya mapato kinyume na sheria za barabarani kwa lengo tu la kufikisha makadirio ya makusanyo waliopangiwa ambayo mara nyingi hayaakisi kiwango halisi, yaani makadirio ni makubwa kuliko hali halisi.
 
Anamaanisha kuwa kuna hatari ya polisi kuanza kukusanya mapato kinyume na sheria za barabarani kwa lengo tu la kufikisha makadirio ya makusanyo waliopangiwa ambayo mara nyingi hayaakisi kiwango halisi,yaani makadirio ni makubwa kuliko hali halisi.
Twaaafwaaaa
 
Kina hatari kubwa ya Askari wa usalama barabarani kuanza kubambikia watu makosa ili wafikie lengo waliloweka
Hili jambo sidhani kama wenye mamlaka watakuwa wamelitazama kwa jicho la pili.

Kwa kupewa malengo ya ukusanyaji itawapelekea ma traffic kubambikia madreva makosa ili mradi muamala usome.
 
Hayo ni malaengo ya serikali kuhakikisha kila Taasisi na Idara kubuni njia mpya za mapato na kujiendesha wenyewe
 
Anayeumia ni mwananchi maana kila sehemu anakamuliwa.
 
Kuna wale polisi wanakaa pale salenda na wengine wanakaa pale akiba.
Wakiona gari la mzigo wanadai risiti za mzigo na kuanza kukuuliza Bei Za vitu.
Mwisho wanakwambia hela ya kwenye risiti ni tofauti na thamani ya mzigo.
Hapo wanataka HELA.Tra wangaalieni Hawa polisi wamekuwa wanonea sana watu.bora mkae wenyewe.
watu wa tra ni waelewa lakini hao polisi wakisimamisha gari lazime watake hela.
HYO NI RUSHWA
 
Hao dawa yao ni kuwaendea na zile za moto tu hakuna haja ya kumuonea huruma dhurumati kama hao
 
Wana kera sana.sasa hivi polisi ndo wamekuwa tra wa kukagua risiti.
Na lazma wakuchomoe hela.
Unaweza ukamkazia ila Sasa umekodi gari la watu unachelewesha dereva inabidi umpe kwa shingo upande
Hao dawa yao ni kuwaendea na zile za moto tu hakuna haja ya kumuonea huruma dhurumati kama hao
 
Hili jambo sidhani kama wenye mamlaka watakuwa wamelitazama kwa jicho la pili.

Kwa kupewa malengo ya ukusanyaji itawapelekea ma traffic kubambikia madreva makosa ili mradi muamala usome.
Kama hujabambikiwa shukuru Mungu
 
Anamaanisha kuwa kuna hatari ya polisi kuanza kukusanya mapato kinyume na sheria za barabarani kwa lengo tu la kufikisha makadirio ya makusanyo waliopangiwa ambayo mara nyingi hayaakisi kiwango halisi, yaani makadirio ni makubwa kuliko hali halisi.
Duh kumbe maanaake nikuwa fine za Barabarani ni chanzo tegemewa cha mapeto mpaka kiwekewe target kama sales man.
 
Back
Top Bottom