Kiongozi yeyote anayewapa watu vyeo kwa kulipa fadhila anafaa?

Kwani mkuu wewe hili hauliangalii kwa mboni za kisiasa?...Hauoni kama uliyoaandika kwenye bandiko hili ni siasa tupu....Bandiko la kisiasa lazima lijadiliwe kwa mtazamo wa kisiasa Chifu...
 
Bavicha mnapigika kweli siku hizi, mmekosa hoja maskini mnalilia sisiemu eti wawachague chadema ktk nyadhfa, mpaka 2020 sijui mtakuwa mmepigika kiasi gani.
 
Unamsema mr liabilty alipohamia chadema akalazimisha watu wake wawepo kwenye nafasi za ubunge na viti maalum
Amepatikana mwenye chongo katika jamii ya vipofu hivyo nyie vipofu lazima mshangilie ili hali nae ana chongo!
 
Kuna kiongozi wa nchi fulani yeye amempa cheo cha ukuu wa wilaya mtu kama kulipa fadhila huyu hafai kuitwa kiongozi NA ALAANIWE
 
Ukiona kiongozi yeyote chini ya jua anachagua viongozi au watendaji kwa kulipa fadhila bila Kuangalia utendaji wa mtu jua kuna kasoro hapo na usitegemee jipya! Huwezi jaza watu wa propaganda kwenye uongozi utegemee UTENDAJI!

hiki kinachofanyika kwa sasa kitazamwe upya, kiukwel si haina nzuri ya kupata viongozi, wasiojua kujipendekeza kwa wakubwa itakua vigumu sana wao kupata nafasi mbalimbali, au wasiokua jiran kwenye kipndi mbalimbal vya tv kama walivyo hao akina polepole, nadhan na yule anayepiga makelele chanel ten angekua siyo mzee angeweza pata.
 
Kuna aliyekuwa mgombea aliahidi hadi vyeo katika idara nyeti za serikali kwa watakaomfanikisha kuingia magogoni.
 
Mbowe kampa mkewe mdogo ubunge viti maalum,Ndesamburo mtoto wake mbunge Viti maalum, Lowasa aliwaahidi kuwapa watu vyeo ndani ya idara mbalimbali.
 
Mbona hapa vyama vingine ni hivyo hivyo tu....hebu angalia mgawanyo wa viti maalumu......lazima wahusika kwa namna moja au nyingine wawe na kauhusiano fulani na wakubwa wa chama......
Sasa na wao kama wakipewa urais watashindwa kufanya waliyoyafanya wenzao.......ikiwa nafasi kama za viti maalumu wanagawana kama mkate wa familia....?!!

Nchi hii hakuna mpambanaji mwenye kuwatetea wanyonge kwa dhati kabisa bali kuna wachumia tumbo tu wanaojifanya kuukosoa mfumo kwa kuwa wao hawapo kwenye huo mfumo wa wizi......wakisha ingia humo wanakuwa kimya kabisa....na wengine bila ya aibu wanawasifia hao hao......
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…