Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,361
- 4,816
Kiongozi wa Upinzani nchini Rwanda Victoire Ingabire amezuiwa kutoka nchini Rwanda kupokea tuzo ya haki za binadamu.
Bi Victoire Ingabire kiongozi wa upinzani nchini Rwanda alitunukiwa tuzo ya mtetezi wa haki za binadamu iliyotolewa na Shirika la haki za binadamu la Uhispania, lakini hakupewa haki ya kuondoka Rwanda kupokea tuzo hiyo, amesema.
Mnamo mwaka 2018, Bi Ingabire alipewa msamaha wakati alipokuwa gerezani akitumikia kifungo cha miaka 15 jela kwa kutishia usalama wa taifa na kupotosha ukweli juu ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994
.
Ni kwanini Bi Victoire Ingabire hakuweza kupokea tuzo?
Mtetezi wa haki za binadamu Nora Morales de Cortiñas, mwenye umri wa miaka 89, kutoka Argentina na mwandishi wa habari Muhispania Pascual Serrano pia walitunukiwa tuzo hiyo Alhamisi usiku katika tukio lililofanyika Madrid.
Bi Ingabire ameiambia BBC kuwa, kupewa msamaha ana haki ya kusafiri nje ya Rwanda wakati wowote anapotaka kufanya hivyo lakini kwa ruhusa ya waziri wa sheria .
"Nimeomba ruhusa lakini sikupata jibu'' - anasema Bi Ingabire.
Wizara ya sheria haijatoa maelezo yoyote juu ya madai yake.
Image caption Bi Victoire Ingabire alitoa hotuba ya kupokea tuzo hiyo moja kwa moja kwa njia ya video kutoka Kigali
Ripoti ya utawala ya Rwanda ya mwaka 2018 inaonyesha kuwa ina kiwango cha kuheshimu haki za binadamu kwa 87%.
Katika hotuba iliyotolewa moja kwa moja kwa njia ya video kutoka Kigali katika tukio mjini Madrid, Bi Ingabire alisema kuwa 'Rwanda bado iko mbali kufikia kuheshimiwa kwa haki za binadamu, kama vile haki ya kujileza na haki ya kisiasa '.
"Hili linaugarimu upinzani, tuna watu abao waliuawa, wakliotekwa na waliofungwa kwa ajili ya haki zao ", Alisema
"Kutokuwepo kwangu kule kupokea tuzo ni ushahidi mzuri wa kile ninachokisema" -Aliongeza. mtoto wake wa Kiume na wakike walipokea tuzo kwa niaba yake.
Kipengele cha 16 cha katiba ya Rwanda kinasema kila Myaranda ana haki ya kuondoka na kurejea nchini mwake.
Je Victoire Ingabire ni nani?
Victoire Ingabire Umuhoza alizaliwa oktoba tarehe tatu mwaka 1968.
Ni mke na mama wa watoto wa tatu.
Amesomea Sheria na masuala ya uhasibu na hatimaye kufuzu kwa shahada ya uchumi na biashara nchini Uholanzi.
Tangu mwaka 1997, Ingabire amejihusisha na harakati za upinzani nchini Rwanda akiwa mafichoni Uholanzi.
Aliteuliwa na muungano wa kundi la viongozi wa upinzani ambao una wanachama nchini Rwanda, barani Ulaya, Marekani na Canada.
Mnamo mwezi Januari mwaka 2010 Bi Ingabire alirejea Rwanda kutoka mafichoni nchini Uholanzi baada ya kutajwa kuhusika kwenye mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, ili kugombea uchaguzi wa urais.
Mwezi Aprili mwaka 2010, aliwekwa chini ya kifungo cha nyumbani.
Unaweza pia kusoma:
Alikamatwa baadaye na kufikishwa mahakamani ambapo yeye na washirika wake wanne, (Kanali Tharcisse Nditurende, Luteni kanali Noel Habiyaremye, Luteni Jean Marie Vianney Karuta na Meja Vital Uwumuremyi), walifunguliwa mashataka ya uhaini.
Alizuiliwa kugombea uraisi wa Rwanda kufuatia mashtaka yaliyokuwa yanamkabili.
Wakuu wa mashtaka wa Rwanda walimfungulia kesi kwa tuhuma za kuunda kundi lenye lengo la kusambaratisha nchi, kulazimisha vitendo vya ugaidi, na kuwachochea raia kuasi dhidi ya serikali.
Mashitaka ambayo alikanusha na kusema kuwa yalichochewa kisiasa
Oktoba 30, mwaka 2012, mahakama kuu mjini Kigali ilimhukumu kifungo cha miaka minane jela baada ya kumpata na hatia ya kupanga njama dhidi ya serikali kupitia vitendo vya ugaidi na vita.
Disemba mwaka 2013, mahakama ya juu zaidi nchini Rwanda ilidumisha hukumu ya mahakama kuu dhidi yake na kumuongezea kifungo gerezani kutoka miaka minane hadi miaka 15.
Bi Ingabire, ni mwanachama wa jamii ya Wahutu na alihoji kwa nini makumbusho rasmi ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda hayakujumuisha Mhutu yeyote.
Wengi wa watu 800,000 waliouawa walikuwa Watutsi lakini baadhi ya Wahutu waliowaunga mkono Watutsi waliuawa na Wahutu wenye misimamo mikali.