Kiongozi wa sukuma gang

Kiongozi wa sukuma gang

Chupayamaji

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2017
Posts
5,780
Reaction score
13,684
NGUVU YA SUKUMA GANG NA WAASISI WAKE.

Na; George Kabadi

Sikushitushwa na taarifa ya uwepo wa press ya Askofu wa Taifa, Dr Josephat Gwajima, kilichonishitusha ni Gwajima kuitisha press ya kujisafisha kabla hujachafuka, ametutangazia kwamba yeye si kiongozi wa kundi linaloitwa Sukuma Gang na anamuunga mkono Rais Samia.

Swali la kujiuliza!
Ivi ni lini Gwajima ametajwa kuwa ni kiongozi wa kundi hilo?
Binafsi jibu sina! Na namna pekee ya kutuaminisha kwamba Gwajima ni kweli hahusiki na SUKUMA GANG ni kurudisha kumbukumbu nyuma.

Tuanzie hapa, Sukuma Gang ilianzaje.

Sukuma Gang ililiasisiwa kati ya mwaka 2016, 2017 na kuwa rasimi katikati mwa mwaka 2019 na kupata mwitikio mkubwa kati ya January hadi Mach 2020, likijulikana kama ISANGE LYA BHADUGU. Ikiwa ni hatua ya mwisho ya kuwashawishi vigogo mwenye mioyo migumu kutoka kanda ya ziwa, kwani tayari kulikuwa na msingi uliyoitwa CcmMpya, iliyokuwa ukiendelea kuwashawishi wanasiasa dhaifu kwa kuwapa ahadi za madaraka ili waunge Juhudi. Isange lya Bhadugu liliasisiwa kama kundi la WhatsApp lenye makusudio kadhaa, ambayo ki msingi yalitumika kuficha uhalisia wa kusudio halisi. Yalianzishwa makundi mengi ya WhatsApp na yalienda kwa namba kutokana na mwitikio na wingi wa watu. Dhumuni la kuanzishwa kwake ki geresha likiwa ni;
Kufahamiana na
Kusaidiana
Kujifunza ki sukuma kwa watu waliyozaliwa mijini.

Utaratibu huo uliendelea kwa muda. hata hivyo kwa kuwa lengo kuu lilikiwa ni kujiimarisha ki siasa kwa baadhi ya waanzilishi wake akiwemo Gwajima mwenye, na akiwa mlango wa mwisho ili umfikie mtu ambaye aliitwa Ntemi "Dr John" Vikao vilikuwa vikifanyika katika hotel flan, hata hivyo Ntemi alikuwa hahudhuri na taarifa za vikao vyote ziliwasirishwa kwenye makundi yote ya WhatsApp na mtu mmoja aliye julikana kwa jina la Peter Rashid Abubakar. Pia Isangi Lya Bhadugu lilikuwa na ''Watwale" hawa ni kama wazee wa baraza ambao waliongozwa na John Cheyo na viongozi wengine wa serikali, Chama Cha Mapinduzi na watu wengine wa vyama vya upinzani waliykuwa katika mkakati huo. Kufikia Mach 03/2020 nguvu ya kundi hili ilikuwa kubwa na tarehe hiyo MARIA SARUNGI alihoji dhumuni la kundi hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter na taarifa hiyo ilizua mtafaruko wa kwanini Gwajima aanzishe makundi ya kikabila.

Kadri ya siku zilivyokwenda kundi lilijibadili kutoka kwenye tawira ya u kanda na kuwa ngome ya pande zote za nchi na kuungwa mkono na watu wa maeneo mengine kwa kuwa tayari CcmMpya ilikuwa ishaaminika kuwa ni salama na makundi ya ISANGE LYA BHADUHU yakavunjwa na kujichomeka rasimi katika falsafa ya CcmMpya, ki uhalisia CcmMpya ndiyo Sukuma Gang na ISANGE LYA BHADUGU ni mkakati uliyotumika kuwavuna watu wa kanda ya Ziwa.

Kushamili kwa Sukuma Gang/CcmMpya.

Kutokana na misingi ambayo ilianza kujengwa tangu 2016, hadi kufika mwaka 2020, Sukuma Gang ilikuwa na ushawishi mkubwa kuanzia serikali na ndani ya Chama Cha Mapinduzi, ikiwa na watu wa kanda zote, Kasikazini, Pwani, Nyasa na Magharibi lengo likiwa ni kutengeneza serikali inayoendana na Dr John na Sukuma Gang wakiwa ndiyo washauri wakuu. Lengo likiwa ni kuyavunja makundi vyote ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi, miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ili kuyavunja nguvu makundi mengine ni kuwachukua wapinzani na kuwapa nafasi nyeti ndani ya serikali na chama.

Kuungwa mkono na kukua kwa Nguvu ya Sukuma Gang.

Kutokana na mikakati na mipango ya muda mrefu, kuelekea uchaguzi wa mwaka 2020, umafia ulianzia ndani ya Chama Cha Mapinduzi wakati wa kura za maoni. Wangombea ambao hawakutakiwa walikatwa na kutupiwa vilago hata kama waliongoza katika kura za maoni. Waliyo wekwa ni wale wanamikakati wa Sukuma Gang ambao wengi wao walishindwa katika kura za mani

Nguvu ya Sukuma Gang ni kubwa; Sukuma Gang huenda ikaendelea kuisumbua Serikali kwa miaka mitano zaidi kwa sababu ya mizizi yake.
Ki uhalisia 95% ya wabunge waliyo ingia bungeni baada ya uchaguzi 2020, wanatokana na mikakati na ubabe wa Sukuma Gang, 75% ya watumishi wa Umma na taasisi nyingine ni Sukuma Gang.

Gwajima akisema hahusiki na Sukuma Gang ananishangaza kwa kuwa alishika nafasi ya pili kwenye kura za maoni lakini yupo bungeni na washirika wake akina;
Silinde yupo bungeni
Kimei yupo bungeni
Waitara yupo bungeni
Eric Shigogo yupo bungeni
Mwambe yupo bungeni na;
Wabunge wengine wengi wapo bungeni kutokana na nguvu ya Sukuma Gang.

Pia Gwajima anaposema si kiongozi wa Sukuma Gang, ni kweli na simpingi kwa maana huenda muda wake wa kuwa kiongozi wa Sukuma Gang umemalizika na kumwachia kijiti mtu mwingine, maana yeye ni miongoni mwa waasisi na wanufaika wa Sukuma Gang.

NAJIULIZA
Je, kuna mtu alimuuliza kuwa bado ni kiongozi wa Sukuma Gang ama yeye mwenyewe amejishitukia kwanini hatumuulizi?

Ushauri wangu, akiwa mwasisi naomba moja asizikane fikra zake!

Mwl Nyerere alimwambia Mzee Makamba.
"Mwanangu heshima na njaa havikai sehemu moja"

George Kabadi
Mkulima Wa Siasa na;
MgombeaUrais2035
 
Sukuma gang ni msemo tu unaolenga kuwadhalilisha wanasiasa wanaoipenda nchi yao na wazalendo ili wale wanaojiita watoto wa mjini waendelee kuharibu nchi

Tena dhana ya kusadikika. Huwezi kuwakuta popote pale kikundi cha watu kinachoitwa kwa jina hilo.
 
Nilipo kua nasoma chuo Cha afya Cha kibena njombe nakumbuka propaganda ya namna hii ilikuepo.
 
Hichi kitu ni halisi kwa 100%.
Hili kundi la Sukuma Gang lilikita mizizi mirefu mnoo ndani ya serikali na CCM. Ni kundi hatari kwa utawala wa Samia na huenda likaendelea kusumbua kwa muda mrefu zaidi.
 
Tusimlaumu fundi-mwashi.Mara ya mwisho nilipomuuliza kwa nini kuta alizojenga zimepindapinda?Akaniambia pimamaji yake haikuwa na maji.Fundi huyo!
 
Mbona yote aya sikuyaona pindi awamu ya 5 iko madarakani. Binadamu wanapenda kuonekana wako mbele ya muda, wakati kila kitu kinatokea kilipaswa kua hivyo.

Sukuma gang kwa Maelezo na kwa nilivyosoma lilikua group la kabila tena kwa wabunge wasukuma.

Ata sisi pia tuna magroup ya ukabira kulingana na kazi, mfano biashara, dereva
 
Hii nchi ipo siku kitaeleweka tu,
Lakin kinachosumbua hapa ni uwingi wa wasukuma,
Makundi ya makabila yapo mengi lakini kwanini wasukuma!?
Jibu ni jepesi,......uwingi wao

Na kitu ukiwa na hofu nacho sana ndiyo unakipa nguvu

Na zaidi msukuma huwezi kumkwepa.

Popote utakapoenda yupo,

Kila ofisi yupo

Hata ukipanda basi lolote linalotoka dar msukuma yumo

Na mbaya zaidi wasukuma hawana mambo mengi

Lingekuwa kabila lingine kwa namna mnavyowasonga kingeeleweka

Lakin wao wapo kama hawaoni

Ila chonde chonde usimsonge mtu ambaye hakusongi

Akibadilika ni mbaya sana

Tutaanza kutafutana hapa mjini tusionane

Hebu tulindeni aman yetu

Tuache ukabila wasukuma ni wengi hatuwawezi.
 
Alikuwa anajibu swali la mwandishi wa habari.

Siku nyingine fuatilia kabla ya kukurupuka kupotosha.

#kataawahuni
 
NGUVU YA SUKUMA GANG NA WAASISI WAKE.

Na; George Kabadi

Sikushitushwa na taarifa ya uwepo wa press ya Askofu wa Taifa, Dr Josephat Gwajima, kilichonishitusha ni Gwajima kuitisha press ya kujisafisha kabla hujachafuka, ametutangazia kwamba yeye si kiongozi wa kundi linaloitwa Sukuma Gang na anamuunga mkono Rais Samia.

Swali la kujiuliza!
Ivi ni lini Gwajima ametajwa kuwa ni kiongozi wa kundi hilo?
Binafsi jibu sina! Na namna pekee ya kutuaminisha kwamba Gwajima ni kweli hahusiki na SUKUMA GANG ni kurudisha kumbukumbu nyuma.

Tuanzie hapa, Sukuma Gang ilianzaje.

Sukuma Gang ililiasisiwa kati ya mwaka 2016, 2017 na kuwa rasimi katikati mwa mwaka 2019 na kupata mwitikio mkubwa kati ya January hadi Mach 2020, likijulikana kama ISANGE LYA BHADUGU. Ikiwa ni hatua ya mwisho ya kuwashawishi vigogo mwenye mioyo migumu kutoka kanda ya ziwa, kwani tayari kulikuwa na msingi uliyoitwa CcmMpya, iliyokuwa ukiendelea kuwashawishi wanasiasa dhaifu kwa kuwapa ahadi za madaraka ili waunge Juhudi. Isange lya Bhadugu liliasisiwa kama kundi la WhatsApp lenye makusudio kadhaa, ambayo ki msingi yalitumika kuficha uhalisia wa kusudio halisi. Yalianzishwa makundi mengi ya WhatsApp na yalienda kwa namba kutokana na mwitikio na wingi wa watu. Dhumuni la kuanzishwa kwake ki geresha likiwa ni;
Kufahamiana na
Kusaidiana
Kujifunza ki sukuma kwa watu waliyozaliwa mijini.

Utaratibu huo uliendelea kwa muda. hata hivyo kwa kuwa lengo kuu lilikiwa ni kujiimarisha ki siasa kwa baadhi ya waanzilishi wake akiwemo Gwajima mwenye, na akiwa mlango wa mwisho ili umfikie mtu ambaye aliitwa Ntemi "Dr John" Vikao vilikuwa vikifanyika katika hotel flan, hata hivyo Ntemi alikuwa hahudhuri na taarifa za vikao vyote ziliwasirishwa kwenye makundi yote ya WhatsApp na mtu mmoja aliye julikana kwa jina la Peter Rashid Abubakar. Pia Isangi Lya Bhadugu lilikuwa na ''Watwale" hawa ni kama wazee wa baraza ambao waliongozwa na John Cheyo na viongozi wengine wa serikali, Chama Cha Mapinduzi na watu wengine wa vyama vya upinzani waliykuwa katika mkakati huo. Kufikia Mach 03/2020 nguvu ya kundi hili ilikuwa kubwa na tarehe hiyo MARIA SARUNGI alihoji dhumuni la kundi hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter na taarifa hiyo ilizua mtafaruko wa kwanini Gwajima aanzishe makundi ya kikabila.

Kadri ya siku zilivyokwenda kundi lilijibadili kutoka kwenye tawira ya u kanda na kuwa ngome ya pande zote za nchi na kuungwa mkono na watu wa maeneo mengine kwa kuwa tayari CcmMpya ilikuwa ishaaminika kuwa ni salama na makundi ya ISANGE LYA BHADUHU yakavunjwa na kujichomeka rasimi katika falsafa ya CcmMpya, ki uhalisia CcmMpya ndiyo Sukuma Gang na ISANGE LYA BHADUGU ni mkakati uliyotumika kuwavuna watu wa kanda ya Ziwa.

Kushamili kwa Sukuma Gang/CcmMpya.

Kutokana na misingi ambayo ilianza kujengwa tangu 2016, hadi kufika mwaka 2020, Sukuma Gang ilikuwa na ushawishi mkubwa kuanzia serikali na ndani ya Chama Cha Mapinduzi, ikiwa na watu wa kanda zote, Kasikazini, Pwani, Nyasa na Magharibi lengo likiwa ni kutengeneza serikali inayoendana na Dr John na Sukuma Gang wakiwa ndiyo washauri wakuu. Lengo likiwa ni kuyavunja makundi vyote ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi, miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ili kuyavunja nguvu makundi mengine ni kuwachukua wapinzani na kuwapa nafasi nyeti ndani ya serikali na chama.

Kuungwa mkono na kukua kwa Nguvu ya Sukuma Gang.

Kutokana na mikakati na mipango ya muda mrefu, kuelekea uchaguzi wa mwaka 2020, umafia ulianzia ndani ya Chama Cha Mapinduzi wakati wa kura za maoni. Wangombea ambao hawakutakiwa walikatwa na kutupiwa vilago hata kama waliongoza katika kura za maoni. Waliyo wekwa ni wale wanamikakati wa Sukuma Gang ambao wengi wao walishindwa katika kura za mani

Nguvu ya Sukuma Gang ni kubwa; Sukuma Gang huenda ikaendelea kuisumbua Serikali kwa miaka mitano zaidi kwa sababu ya mizizi yake.
Ki uhalisia 95% ya wabunge waliyo ingia bungeni baada ya uchaguzi 2020, wanatokana na mikakati na ubabe wa Sukuma Gang, 75% ya watumishi wa Umma na taasisi nyingine ni Sukuma Gang.

Gwajima akisema hahusiki na Sukuma Gang ananishangaza kwa kuwa alishika nafasi ya pili kwenye kura za maoni lakini yupo bungeni na washirika wake akina;
Silinde yupo bungeni
Kimei yupo bungeni
Waitara yupo bungeni
Eric Shigogo yupo bungeni
Mwambe yupo bungeni na;
Wabunge wengine wengi wapo bungeni kutokana na nguvu ya Sukuma Gang.

Pia Gwajima anaposema si kiongozi wa Sukuma Gang, ni kweli na simpingi kwa maana huenda muda wake wa kuwa kiongozi wa Sukuma Gang umemalizika na kumwachia kijiti mtu mwingine, maana yeye ni miongoni mwa waasisi na wanufaika wa Sukuma Gang.

NAJIULIZA
Je, kuna mtu alimuuliza kuwa bado ni kiongozi wa Sukuma Gang ama yeye mwenyewe amejishitukia kwanini hatumuulizi?

Ushauri wangu, akiwa mwasisi naomba moja asizikane fikra zake!

Mwl Nyerere alimwambia Mzee Makamba.
"Mwanangu heshima na njaa havikai sehemu moja"

George Kabadi
Mkulima Wa Siasa na;
MgombeaUrais2035
Sasa hivi kuna family gang.
 
Back
Top Bottom