Kiongozi wa Korea Kaskazini: Kitufe cha silaha za nyuklia kiko mezani pangu

Chillah

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
8,294
8,856
Kiongozi wa Korea Kaskazini: Kitufe cha silaha za nyuklia kiko mezani pangu; zinaifikia ardhi yote ya Marekani
4bpl0bffdd4252zc2i_800C450.jpg

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amesema, nchi yake imefikia kiwango cha uwezo wa kupiga eneo zima la ardhi ya Marekani kwa silaha zake za nyuklia na kwamba "kitufe cha silaha za nyuklia" kiko juu ya meza yake.

Akihutubia mapema leo kupitia televisheni ya taifa kwa mnasaba wa Mwaka Mpya wa 2018, Kim amesema, "silaha hizi zitatumika pale tu usalama wetu utakapotishiwa".

"Marekani nzima inafikiwa na silaha zetu za nyuklia, na kitufe cha nyuklia muda wote kiko mezani pangu. Huu ni ukweli halisi, sio kitisho", ameongeza kueleza kiongozi huyo kijana wa Korea Kaskazini.

Kim Jong-un aidha amesema mwaka huu inapasa kujikita zaidi katika kuunda na kuzalisha kwa wingi vichwa vya nyuklia na makombora ya balistiki kwa ajili ya operesheni ya usambazaji.

Katika hotuba yake hiyo ya mwaka mpya kwa taifa, Kim aidha amesisitiza kwamba kuna umuhimu mkubwa mno wa kupunguzwa mivutano ya kijeshi katika rasi ya Korea na kuongeza kuwa mlango wa mazungumzo na Korea Kusini uko wazi.

4bn24fffef1ac8x1e5_800C450.jpg

Maonyesho ya makombora ya Korea Kaskazini
Kuhusiana na hilo amesema nchi yake inafikiria kutuma ujumbe kwenye Michezo ya Olimpiki ya Msimu wa Baridi iliyopangwa kufanyika mwezi ujao wa Februari katika mji wa Pyeongchang, Korea Kusini na kwamba kushriki Pyongyang kwenye michezo hiyo ni fursa nzuri ya kuonyesha umoja baina ya watu wa mataifa hayo mawili.

Tangu mwaka 2006, Korea Kaskazini imekuwa ikiandamwa na vikwazo vikali vya Umoja wa Mataifa kwa sababu ya kufanya majaribio ya silaha za nyuklia na ya aina mbalimbali ya makombora yakiwemo ya masafa marefu, ya balistiki. Lengo la vikwazo vyote hivyo ni kuilazimisha nchi hiyo isitishe majaribio yake hayo. Hata hivyo Pyongyang inatetea mipango yake ya kijeshi ikisisitiza kwamba inalenga kukabiliana na sera za kiadui za Marekani na waitifaki wake katika rasi ya Korea, ikiwemo Korea Kusini na Japan…/
 
Back
Top Bottom