Kiongozi ni Dira ya watu anawaongoza

Kiongozi ni Dira ya watu anawaongoza

Janken jr

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2016
Posts
1,125
Reaction score
1,184
kiongozi ni dira ya wananchi wa eneo husika,kiongozi anapokuwa na maona mazuri ndivyo anawaongoza watu wake kuwa na maono mazuri,yeye ndie hutoa automatically mwelekeo wa kimaono wa watu wake wapi waelekee.maendeleo yoyote au kinyume chake popote pale duniani ni matokeo ya maono ya viongozi,nchi zenye furaha na upendo au ghasia ni matunda ya maono ya uongozi uliopita au uliopo,sisi watanzania tulikuwa tunajivunia amani na upendo miongoni mwetu ni kwa sababu ya maono ya waasisi wa taifa hili yaliyopelekea kujenga misingi imara ya upendo nakukomesha ukabila,udini ,ubaguzi na makandokando yake.lakini naiona ile misingi inamomonyolewa kwa kasi ya ajabu,sina uhakika kama tupo salama kama vile tunavyoaminishwa. sioni wenye hekima na busara wanaostuka katika hili,naona jahazi letu linakwenda mlama.

upendo unapotea kwa kasi ya kimondo na kwa kasi kama kimbunga,wote tupo fofo tumewaachia wachache watukaririshe maneno kuwa bado amani yetu ipo imara,wazi sasa mwangwi wa ukanda unavuma,unavumishwa sijui kwa makusudi wanasiasa kwa maneno na vitendo.wapo wengi hawaridhiki na kinachoendelea wengine waona wanatengwa hawana pa kusemea,wanaumia kimya kimya,wengine wameamua kuitisha ata sensa ili mkijitathimini,sijui watakuja na majibu gani.wanatukaba,wanatubagua kwa vitendo na maneno,kisha wanaomba tuwaombee ,kivip ili muendelee kutumiza!!Nchi imekuwa ya visasi,magogoni ina control mpaka vyumba vya wahariri,yuko nwapi Issakwisa mwaifunge?

Hapana,hii nchi ni yetu sote tuijenge klwa upendo na kwa vitendo vya usawa na upendo.kiongozi ukiwa na maono ya chuki dhidi ya makundi flan unaambukiza chuki hizo kwa wengi zaidi,kiongozi ukiwa busara na hekima utwaongoza watu wako mkatika njia hiyo hiyo na wasaidizi nao watafuata njia hiyo hiyo.nafikiri kila mmoja anaelewa
 
Back
Top Bottom