Kiongozi anapokuwa Muongo

Kiongozi anapokuwa Muongo

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
2,175
Reaction score
4,179
NI kujulishana juu ya Viongozi wa Serikali ,kuanzia Mkuu wa Nchi akifuatiwa na ngazi mbali mbali hadi balozi wa nyumba kumi kumi.

Ni kesi ngapi maarufu za kupotea watu maarufu ,tuwaweke pembeni kina sisi pangu pakavu.

Watu maarufu waliojulikana na kuvuma , kurahisisha ni zile zinazowahusisha wale wanaosema watafuatilia.

Pengine utamsikia Mkuu iwe wa nchi ,waziri au Polisi akiahidi kupitia vyombo vya habari kuwa wanafuatilia na WATATATOA habari kamili.

Niliifuatilia kupotea kwa Bin Sanane nikafuatilia ya Mohamed Kibao ambayo hapa hata Raisi aliagiza .

Je kuna report zimewasilishwa au kutolewa na vyombo vilivyochukua ahadi hadharani ?

Vyombo vya habari vilivyojaa na ndio vya kwanza kurusha habari wamewahi kuwakumbusha wakuu hawa ?
Maana siku hizi wakuu wengi wanajiingiza kwenye mambo ya muziki kushiriki tamasha ,matamasha ya aibu tupu ,wakiwafanya WaTanzana hawana akili au ni kama wao ,au wanapokea visa vyao, maana wanayoyafanya ni visa vya ajabu sana.

Au wanaona waTanzania wote wanashirikiana na watenda laana ? Nawaona wahovyo sana na hasa ukiwaona wanashiriki kwenye mambo ya ibada ,leo hii Marekani hao mnaowategemea nchi zao zinaanguka kiuchumi na kila siku zinazidi kuangamia mbali ya mabalaa ya moto,.

Kma kuna hayo makesi yalioahidiwa yalifanyiwa updeti tujulisheni au tuwekeeni link hapa.
 
😂😂😂 Nunua chuma punguza mmoja mmoja, Mungu mwenyewe kachoka kuachiwa kila kisasi alipe yeye
 
Back
Top Bottom