Kiongozi anapokuwa mbaguzi na muonevu

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,800
2,337
Kwa mara ya kwanza ktk awamu hii iliyojinasibu kuwa haitamuonea mtu na haki itatawala ndo tumeshuhudia mambo ya ajabu.

Ivi unawezaje kuwafukuza watu maelfu kwa maelfu kwa issue ya vyeti feki huku unawaacha kisa wana siasa na watawala wakati taratibu inasema angalau awe na degree.

Kiongozi wa nchi anapokuwa mbaguzi na mwonevu ni aibu ya taifa. Ni jambo la kusikitisha na kutia hasira sana. Zoezi hili ilikuwa nzuri kama panga hili lingepita kwa wote ila kitendo cha kuwaacha wengine amelitia doa taifa

Hakika kiongozi aliyeoungukiwa na akili huwaonea watu sana
 
Haya ni maajabu yanayoweza kutoka TZ peke yake.......

Eti maRC na maDC siyo watumishi wa Umma Bali ni wanasiasa na wao hawahusiki na mambo ya kufoji vyeti, eti kwa sababu nafasi zao hazihitaji kwenda shule na qualification pekee wanayotakiwa kuwa nayo ni ONLY kujua kusoma na kuandika!

Hiyo maana yake dereva anayemwendesha RC au DC anatakiwa kuwa msomi zaidi ya Bosi wake!

Kwa kuwa minimum qualification ya dereva wa RC au DC ni kidato cha nne.

Hiyo 'exemption' ya maRC na maDC kuitwa ni wanasiasa wakati katika hali halisi siyo wanasiasa Bali watumishi wa Umma imewekwa kwa 'special mission'

Hiyo 'exemption' imewekwa kwa makusudi maalum nayo si nyingine bali kwa ajili ya kumlinda mtu mmoja tu, naye si mwingine bali ni Daudi Bashite wa Koromije!
 
Kwenye sheria kuna principle moja muhimu sana nayo si nyingine bali inayosema kuwa sheria huwa haina MACHO.....

Hiyo tafsiri yake ni kuwa kama limefanyika kosa la jinai, sheria inapaswa kuchukua mkondo wake bila kujali nani aliyefanya kosa hilo la jinai.

Cha ajabu katika serikali hii ya awamu ya 5 imeamua kumlinda kwa nguvu zake zote, mtu mmoja aitwaye Daudi Bashite!

Nitaorodhesha baadhi ya makosa yake ambayo kama sheria katika serikali hii ya awamu ya 5 ingeamua kutokuwa na MACHO, huyu jamaa kipindi hiki asingepaswa kuwa uraiani, bali alipaswa kuwa jela.......

1. Alivamia kituo cha Clouds Media akiambatana na askari wenye silaha na kuwalazimisha watangazaji wa kituo hiko waitangaze clip 'yake' inayotaka 'kumpakazia' Askofu Gwajima kuwa eti kazaa na Binti fulani huko Kimara....

Baada ya watumishi wa kituo hicho cha luninga kumwambia kuwa taaluma yao haiwaruhusu kurusha taarifa ambayo hawana uhakika na ukweli wake, mtu huyo Daudi Bashite akawatishia watumishi hao wa TV kuwa atawabambikia kesi ya madawa ya kulevya na hivyo watafungwa jela!

Pamoja na kosa hilo la jinai la wazi, lakini hakuna chombo chochote cha dola kilichokuwa na 'ubavu' wa kumchukulia hatua mtu huyo UNTOUCHABLE!

2.Mtu huyo huyo ametuhumiwa kuwa amesoma Chuo kwa cheti ambacho siyo chake, kwa tafsiri nyingine amefoji cheti, lakini pamoja na kuwa tuhuma hizo zinaelekea kuwa ni za kweli, mamlaka zote nchini zimeshikwa na 'kigugumizi' na kushindwa kumchukulia hatua yoyote!
 
Hii ndiyo moja wapo wa nyufa aliyozizungumzia hayati baba wa taifa Mwl. J. K. Nyerere. Ubaguzi huu utaongezeka na utachukuwa sura mbalimbali dawa ni kuliombea taifa watu waungane katika kupalilia mema ya taifa Lao.
Kwa mara ya kwanza ktk awamu hii iliyojinasibu kuwa haitamuonea mtu na haki itatawala ndo tumeshuhudia mambo ya ajabu.

Ivi unawezaje kuwafukuza watu maelfu kwa maelfu kwa issue ya vyeti feki huku unawaacha kisa wana siasa na watawala wakati taratibu inasema angalau awe na degree.

Kiongozi wa nchi anapokuwa mbaguzi na mwonevu ni aibu ya taifa. Ni jambo la kusikitisha na kutia hasira sana. Zoezi hili ilikuwa nzuri kama panga hili lingepita kwa wote ila kitendo cha kuwaacha wengine amelitia doa taifa

Hakika kiongozi aliyeoungukiwa na akili huwaonea watu sana
 
Ukabila, ukanda,udini na double stardard ni sehemu ya matatizo kwa upendo,mshikamano na amani ya nchi.
 
Kwa mara ya kwanza ktk awamu hii iliyojinasibu kuwa haitamuonea mtu na haki itatawala ndo tumeshuhudia mambo ya ajabu.

Ivi unawezaje kuwafukuza watu maelfu kwa maelfu kwa issue ya vyeti feki huku unawaacha kisa wana siasa na watawala wakati taratibu inasema angalau awe na degree.

Kiongozi wa nchi anapokuwa mbaguzi na mwonevu ni aibu ya taifa. Ni jambo la kusikitisha na kutia hasira sana. Zoezi hili ilikuwa nzuri kama panga hili lingepita kwa wote ila kitendo cha kuwaacha wengine amelitia doa taifa

Hakika kiongozi aliyeoungukiwa na akili huwaonea watu sana
Pole sana kwa kukutwa na cheti feki
 
Hii ndiyo moja wapo wa nyufa aliyozizungumzia hayati baba wa taifa Mwl. J. K. Nyerere. Ubaguzi huu utaongezeka na utachukuwa sura mbalimbali dawa ni kuliombea taifa watu waungane katika kupalilia mema ya taifa Lao.
Nyerere aliwahi kuandika shairi moja akiiombea tanzania lakini mule kwenye maneno aliwataka watanzania wasimwachie mungu kila kila kitu tupigane
 
Back
Top Bottom