Maisha ya jamii kuanzia mtu binafsi yanahitaji mtaji wa afya kiakili, kiroho/kifikra na kimwili. Huwezi kudeliver 100% kama mwili wako ni goigoi. Hata kwenye michezo kuna kitu kinaitwa 'physic' yaani stamina ambalo ni tatizo kwa timu yetu ya taifa tunapokutana na mataifa mengine. Ikija kwenye familia na jamii hata taifa kwa ujumla wanahitaji rasilmali watu yenye nguvu ya kuzalisha na kulinda jamii na mali.
Hivyo ukakamavu ni muhimu kwa mtu binafsi, familia na jamii. Fikiria kila mara unavamiwa kwako unadhalilishwa mbele ya mkeo na wanao kisha mali zinaporwa. Lazima utaanza kufikiria udhaifu wako na kuurekebisha ili usiendelee kusumbuka na kadhia hiyo.
Kwa kuliona hilo, jamii na taifa wanaojitambua huhimiza na kutafuta njia za kujenga ukakamavu kuanzia kwenye familia, mashuleni nk.
Kwa umuhimu huohuo CCM imekuwa ikiwajengea uwezo na ukakamavu vijana wao kwa miaka mingi sana. Wamekuwa wakifanya hivyo ili kuepuka kuwa na vijana au wanachama magoigoi.
Kama CCM hawataki kuwa na vijana magoigoi basi tusitegemee kuna chama chochote duniani kita-speciallize kwenye kuwa na wanachama magoigoi. Si lengo la mada hii kueleza matumizi/application ya ukakamavu bali tukubaliane kuwa chaguo la kila mtu binafsi, familia, taasisi, jamii au taifa ni ukakamavu. Ugoigoi is definately not an option to anyone.
Sasa tujiulize kama wote tunapenda ukakamavu kwanini CHADEMA walipotangaza kutoa mafunzo ya ukakamavu (sio kuanzisha jeshi) kumezua mtafaruku na kuambiwa wanavunja sheria? (na sheria ipi inayozuia wananchi kujiweka wakakamavu?).
Ni chaguo lipi lingefurahisha- wangesema tutatoa mafunzo ya ugoigoi? Kwa nini ukakamavu ni sawa kwa CCM na iwe dhambi kwa CHADEMA? Kwani vijana wakakamavu wa Cdm watageuka wanyarwanda? Si wataendelea kuwa vijana wakakamavu wakitanzania? Ni kitu gani kinawatisha CCM ambacho kinakuwa hatarini ikiwa vijana wenzao wa Chadema nao wataacha ugoigoi na kuwa wakakamavu kama wao? Kumbe amani inakuwepo pale tu CCM Wakiwa wakakawavu na vyama vingine hasa CHADEMA wakiwa magoigoi?
AMANI NI TUNDA LA HAKI NA WAJIBU otherwise tunachokiita amani huwa ni woga na hofu inayosababishwa na ubabe na vitisho!