Kinyozi aliyekua akinyoa juu, sasa ananyoa ........

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,779
Katika hali isiyokua ya kawaida mshirika mwenzangu katika mishemishe za ujasiri wa mali na kuongeza kipato, alikua amefungua salon ya kunyolea nywele.
Salon hiyo ipo mjini kati , ghorofa ya 3 juu ambako palikua ni mtaa wenye magorofa mengi.
Hivi majuzi ghorofa hilo ambako salon ipo palikua pakifanywa ukarabati .
Na hivyo kulazimika baadhi ya wapangaji waliokua ghorofa ya 3 kuhamia vyumba vya chini kwa muda, kupisha renovation.
Ili wasipoteze customers wao pale salon , wakaweka sign point iliyosomeka " KINYOZI ALIYEKUA ANANYOA JUU SASA ANANYOA CHINI"
Bandiko hilo lilieleweka kwa maana tofauti na ilivyokusudiwa kwa baadhi ya wateja!
Ni kweli kuna waliosoma ubao huo na kula kona! Wenye Salon walipokujashtuka wateja wanapungua ndipo walipofanya utafiti wa kina, na kuhisi labda bandiko , walipobadili andiko muda mfupi idadi ya wateja ikarudi kama awali .
* Angalizo itokeapo shughuli zetu zinahitaji mabandiko ya utambulisho basi tuwe makini katika kuyaandika.
 
Jg...umetisha braza...
aya ngoja nipeleke hii afro yangu maana zimeanza kutokeza kwa chini...lol
 
Jg...umetisha braza...
aya ngoja nipeleke hii afro yangu maana zimeanza kutokeza kwa chini...lol

BAGAH ! Mambo? Mkuu siku hizi usiku sikuoni sana
kitaani ( jamvi)
leo nadhani match ya Madrid & Bayern ndo imekusogezasogeza au ?
 
Tunapoweka mabango inatakiwa yaeleweke yasiwe na utata mfano hilo bango ananyoa chini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom