Elections 2010 Kinondoni Need MP like Mpoki Mwambuluku


Ohooooo. REAL?
 
AS mentioned, Hata mimi nadhani Mpoki Deserve. Alisoma Ilboru Seconadry in 90's na wakati huo kulikiuwa na watoto wengi walirudi kusoma nchini toka nje ya nchi, hakuwa na classes kama wengine, was friendly na mtu wa watu

NI aina gani ya mvinyo mmleweshwa...............................this has got nothing to do with politics............ashindane na wenzie
 

Sure, Balali alisoma, kufanya kazi na kuishi USA for decades lakini aliporudi kuwa gavana ndio alikuwa mwizi mkubwa akishikiana na majambazi akina Kagoda, Jeet Patel etc. Kwa hiyo kuishi na kuwa na exposure ya nje si issue hata vijana wanaoiba sana Barclays na Standard Chatered Banks ni walisoma UK na USA
 

NI kweli mkuu, angalia waliosoma vyuo vinavyosifiwa duniani? wamekaa kwenye uongozi kwa muda mrefu. Look at them, rotten to the core. Kama ingekuwa kuishi west na kuwa na elimu nzuri Mkapa aliqualify sana. Lived in US for like 10 years, went to Makerere (the best at his time) and Columbia Universities (one of the best in USA), lakini angalia sasa. EPA, Kiwira, ndege Radar etc. Look at mzee wa vijisenti elimu nzuri, lakini arrogant na amejiwekea vijisenti vya ufisadi ng'ambo. So kusihi na kupata e,imu nzuri ya west si sababu ya kuwa kiongozi anayefaa.
 

Bongolander,

..nadhani kuishi nje peke yake siyo kigezo kikuu cha kumpa mgombea uongozi.

..nadhani tunapaswa kuwa makini zaidi ktk kuchagua viongozi kuliko ku-base kwenye upinzani wa walioishi nje vs walioshi nyumbani.

..mgombea anapaswa kuwa na sifa za ziada juu ya kufanya kazi na kusoma nje ya nchi.

..kuna tatizo kubwa sana hapa Tanzania na limeshindikana kutatuliwa hata kwa kurudisha nchini wataalamu wetu waliofanya kazi nje. tatizo hilo ni utamaduni wa rushwa, wizi, na ubadhirifu. watu kama Dr.Balali walifanya kazi kwa uadilifu mkubwa ktk mashirika ya kimataifa, mara waliporudi Tanzania wamejitumbukiza ktk rushwa na ubadhirifu wa kutisha.

..sasa pamoja na kulaumu kwamba wataalamu wetu wanaorudi toka nje wametuangusha, labda tuangalie ni mazingira gani ya ndani ya Tanzania yanasababisha tunaangushwa[tunaibiwa,tunahujumiwa] na kila mhusika anayepewa madaraka.

..vijana, wanawake, wazee,...kila anayepata uongozi Tanzania ya leo haichukui muda mrefu anatumbukia ktk mambo ya ufisadi. tuna tatizo kubwa sana Tanzania na kwa kweli linahitaji umakini na uzalendo wa hali ya juu kulitatua.
 
Mshauri kwanza chama alicho gombea hawezi kutudanganya eti ataleta maendeleo wapi na wapi?
Angegombea chama kingine tungalijua jamaa ana uchungu na nchi yake lakini huko aliko jipachika tunategemea ni wale wale wa kushibisha matumbo yao kwanza kisha wapambe mnao mpigia debe. Hakuna kitu hapo.
Bora niendelee kushoe shine tu.
 

Je TIDDO MHANDO wa BBC ndiye huyu anayedhalilishwa na akina Lowasa hapa TBC 1? Je si alifanya vizuri tu kule BBC, nini amepewa hapa mpaka amekuwa kama Zuzu? Sasa hivi TBC 1 hata kule DSTV inaonyesha ovyo tu, inakatakata mpaka aibu. Ukifungulia KBTV kwenye DSTV iko clear sana! Tatizo ni uroho na kuhemea misaada, vinginevyo Tido angekuwa na akili ni vyema astaafu, kuliko aibu hii anayo jitia kwa kulamba miguu ya kina Lowasa na wenzake.
Hivyo kutembea nje, kusoma nje, kufanya mashirika ya kimataifa is one, na kuwa na moyo wa uzalendo ni kingine....tusimpokee mtu kwa CV yake. Kama CV yake nzuri, aombe kazi pale BOT, akawasaidie kuplan uchumi upya, lakini sio kwenye siasa ambako unakaa kikao kimoja na wasanii kama akina Hadija Kopa, halafu utegemee kutumia PHD yako vizuri....
 
[
Re: Kinondoni Need MP like Mpoki Mwambuluku




HUO UPARA, NA KUONYESHA VYETI KUNA WALAKINI.
1) Amenyoa Upara aonekane kijana zaidi
2) Hatupo hapa kwa ajili ya vyeti. Uongozi ni kujitolea
3)Professor Beno Ndulu na uprofessor wake wote, akili yake finyu kuliko hata ya madiwani wa kuteuliwa ambao wanajua priorities
To hell with his education; let him prove himself!!!
 
AHAHAHAHAHAHAHAHA....kwani huyu anatofauti gani na shemeji yetu shyrose bhanji??....atleast shrose huwa namuona akikabidhi visima vya maji vilivyochimbwa na boss wake nbc/nmb ... atleast naweza kusema anayajua matatizo ya watanzania likiwamo la kukosa maji hata hayo machafu...KUKAA/KUSOMA ULAYA/MAREKANI/EAST/NORTH/WEST has nothing to do with our maendeleo..refer sifa za kiongozi tunayemuhitaji toka kwenye HOTUBA ZA BABA WA TAIFA JK NYERERE...kama huyu msomi wako anazo basi aje agombee tutampa kula..am sorry..kula kwa ccm kura kwa wapinzani makini
 

Nyumbu,

..kama nimekuelewa hoja zetu hazitofautiani sana.

..tuchukulie mfano wa Dr.Balali: kwanini mtaalamu huyu alifanya kazi umahiri na uadilifu mkubwa alipokuwa World Bank, lakini aliporudi Tanzania akaweka kila kitu pembeni na kutumbukia ktk ufisadi? Tido Mhando alikuwa makini wakati yuko BBC, lakini tumemrudisha Tanzania tayari amekuwa bomu. the list can go on and on....

..kwa mtizamo wangu uongozi wa Tanzania umejaa mafisadi wengi kupindukia kiasi kwamba wanaathiri hata wataalamu wetu waliokuwa wakifanya kazi vizuri wakiwa nje. bila kuwasafisha mafisadi walioko ndani, ambao ni wengi, tusitegemee kwamba wataalamu wetu wanaorudi nyumbani watatusaidia.

..kuhusu suala la uzalendo: tutatumia njia zipi kuthibitisha kwamba mhusika ana sifa ya uzalendo? nadhani itabidi tu tubahatishe, na katika kubahatisha huko ndiyo kila siku inakula kwetu. tumebahatisha na Balali,Ndulu,Mrema[tanroads], etc etc

NB:

..kuna nchi kama Rwanda inasemekana huko wamefanikiwa. lakini mkumbuke kwamba jirani zetu hawa waliondoa uongozi na serikali nzima na kuanza upya.
 
Hata ungetuonyesha vyeti vingine mia kasoro moja. Its just nonsense. "Being a good leader is not a matter of academic excellencies". Watch out gentleman..........!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.
 
alipokosea kama msomi, ni kujaribu kuvutia watu/wapiga kura kwa kutumia vyeti vyake, hicho ni kiwango cha chini cha kufanyia kampeni, labda hapo kinondoni, maana waliongozwa na mwenye cheti cha computer, na hata Asha Baraka nae anapataka?
a quality of a leader is more than kuwa na vyeti lukuki etc, bali ni kuwa na commitment ya kuwasaidia unao waongoza.
labda kabla ya kuingia kwenye kinyanganyiro hichi angekuwa hata anaandika makala kuhusu mambo yamaendeleo, ingesaidia kuonyesha ni jinsi gani elimu yake itamfaa/imemfaa .
na angekuwa ameaanza kuwaelimisha hao wajisiriamali/wakazi wa kinondoni jinsi gani wanaweza kuboresha maisha yao, kwa mtaji hiyo hiyo midogo walio nayo au kuendeleza makazi yao kama usafi nk nkn
 

MPOKI MWambulukutu akionyesha vyetivyake

Duh kwahiyo anatembea na photocopy za vyeti vyake kwenye kampeni?he is out of touch..

Angekutana na huyu jamaa angegaragazwa vibaya...

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Deo Sanga a.k.a Jah People anayeomba ridhaa ya wana CCM kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Njombe Kaskazini kupitia chama hicho, amejinadi kwa wapiga kura wake akisema yeye ni msomi mwenye elimu aliyoiita ya Juu Kabisa ya Darasa la Saba .

“Naitwa Deo Sanga au Jah People, mpenda maendeleo, mtu wa watu, mpenda watu na watu ndio nyie, elimu yangu ni darasa la saba lakini ni la darasa la saba la juu kabisa,” alisema na kushangiliwa na mamia ya wanaCCM waliojitokeza katika mkutano wa wanaCCM walioomba uteuzi wa kuwa wagombea wa ubunge katika jimbo hilo uliofanyika juzi jioni katika kata ya Ubena, Makambako Njombe..

Katika hali iliyoonekana kihoja kwa baadhi ya wanaCCM na wananchi wengine walioshiriki mkutano huo, alipoulizwa na mmoja wa wanaCCM hao nini maana ya elimu ya juu kabisa ya darasa la saba, Sanga alisema pamoja na kuwa na elimu hiyo, iko juu ya kichwa chake kwasababu ni nyingi na ndiyo imemuwezesha kuwa Mkurugenzi wa Kampuni kubwa kabisa ya usafirishaji wa Jah People.

FRANCIS GODWIN----NI MATUKIO DAIMA: MGOMBEA UBUNGE AJIGAMBA KUWA AMESOMA ELIMU YA JUU YA DARASA LA SABA
 
Msomi yeyote mzuri mwenye dhamira safi kutoka ndani ya Moyo wake hawezi kugombea Ubunge kupitia CCM, kwa sababu huko ni kujipaka matope. Jambo moja dhahiri ni kwamba wanadhani ukipitishwa kura za maoni CCM basi tayari wewe ni Mbunge, hii maana yake ni kwamba wanautaka ubunge kwa maslahi yao kwanza.
 
Sahara voice said:
Jambo moja dhahiri ni kwamba wanadhani ukipitishwa kura za maoni CCM basi tayari wewe ni Mbunge,

Saharavoice,

..kuna ukweli fulani katika madai hayo.

..bila wananchi kuikataa CCM hali itaendelea kuwa hivyohivyo.
 

Katika majimbo mengi nchini, kushinda kwenye kura za maoni ndani ya CCM ni vigumu zaidi kuliko kuwashinda wagombea wa vyama vingine kwenye uchaguzi mkuu, hiyo ndio hali halisi kwa sasa.
 

Umesema vyema kabisa ndugu. Mtu yeyote ana haki kabisa kugombea uongozi ni haki ya kikatiba.Kisichotakiwa ni majigambo au mtu kudhani kwa vile ana advantage kama hizo za kusoma nje ya nchi basi anasimama nafasi nzuri kuliko watoto wa wakulima waliosoma Kigonsera, Msalato, BWIRU N.K. Kinachotakiwa ni uwezo wa kuongoza, karama, umahiri na pia ile hali ya kuwa mkweli na siyo kutaka kudanganya wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…