Kinondoni na Siha, tusikubali ujinga huu! hata Mwl. Nyerere alikataa ujinga wa CCM, 1995 akachagua upinzani!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,504
113,618
Wanabodi,

Tafsiri ya Neno Ujinga.
Naomba nianze na tafsiri ya neno mjinga maana watu humu hawakawii kusingizia watu kuwa tumetukana watu humu!. Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu
neno ujinga ni kutokujua.

Declaration of Interest
Naomba ku declare interest kuwa licha ya mimi kuwa ni mwanachama wa chama cha siasa, lakini pia ni Mtanzania mzalendo wa taifa langu, nikiwa ni muumini wa falsafa ya Mwalimu Nyerere kwa mawazo, maneno na matendo, hakupenda kuona Watanzania tulifanywa mazuzu, hivyo alikataa ujinga wa aina yoyote, kuanzia ujinga wa IMF na WB, wa mabeberu na wakoloni mambo leo na vibaraka wao, alikataa hata ujinga wa chama chake CCM, pale kilipowapelekea ujinga kwenye mgombea ubunge, na kumpigia kampeni mgombea safi wa upinzani, hivyo mgombea wa CCM akapigwa chini na mgombea wa upinzani akapita, hivyo kitendo kilichofanywa na CCM majimbo ya Kinondoni na Siha, kutuletea sisi wapiga kura watu wale wale tuliowaaminia kutuongoza, halafu wakatuletea ujinga kwa kujiuzulu, halafu unatuletea watu wale wale, huku ni sawa na kutufanya sisi wote pia ni wajinga, hivyo hili ni bandiko elimishi, kuwaelimisha wale wasiojua, kuwa kitu CCM ilichowafanyia wananchi wa Kinondoni na Siha ni ujinga, nimejitolea kuelimisha ili tuukatae ujinga huu!.

Uzalendo wa Kweli ni Kutanguliza Mbele Maslahi ya Taifa, Kama Chama Kinaleta Ujinga, Weka Pembeni, Tanguliza Utaifa Mbele!.
Naendeleza zile Makala elimishi, za kuelimishana dhana ya uzalendo wa kweli wa taifa letu, ni kutanguliza mbele maslahi ya taifa na vingine vyote vinafuatia, hivyo Tanzania kwanza, vyama vije baadae. Ikitokea wewe ni mwanachama na chama chako kikatuletea ujinga Watanzania, tukuukatae ujinga huo, kwa kukitaa chama hicho kinacholeta ujinga, kwa kutokichagua, na kutomchagua mgombea wake, hata kama mgombea huyo ni wa chama chako, na badala yake unamchagua mgombea wa upinzani, ili kutuma ujumbe mzito kwa chama chako na viongozi wake kuwa Watanzania wote sio wajinga, hivyo hii itazuia viongozi wa chama chako kutowaletea tena ujinga kama huu next time.

Jee Chama Kama Chama, Kinaweza Kufanya Makosa?, Kikifanya Makosa, Wa Kulaumiwa ni Nani na Wakuadhibiwa ni Nani?.
Chama kama chama ni physical being, kama ilivyo kwa makampuni, ni personal being, kampuni inaweza kufanya makosa, na chama pia vile vile kinaweza kufanya makosa. Ila kama ilivyo kwa kampuni, ikifanya makosa, kampuni inaweza kushitakiwa, lakini linapokuja suala la adhabu, kama ni kosa dogo la kustahili adhabu ya faini, kampuni inaadhibiwa kwa kupigwa faini, na faini inalipwa, lakini kama ni kosa kubwa la jinai, linalostahili adhabu ya kifungo, kampuni haiwezi kufungwa jela, wanaofungwa jela ni wamiliki wa kampuni. Hivyo chama cha siasa kinapoleta ujinga, hili ni kosa kubwa la kustahili adhabu, kinashitakiwa kwa wananchi, namna pekee ya kukiadhibu chama kinacholeta ujinga wa namna hiyo, ni kukichapa bakora kwa kuwapiga chini wagombea wake, kwa kutowachangua, ili kutuma ujumbe Mzito kuwa Watanzania wote sio wajinga, kuletewa ujinga na kuuchagua ujinga huo!.

Jee Mwanachama Kuhama Chama Kimoja cha Siasa na Kuhamia Chama Kingine ni Kosa?.
Hapana, hakuna kosa lolote kwa mwanachama wa chama chochote kuhama chama kimoja na kujiunga chama kingine. Kama ilivyo kwa Watanzania kuwa huru kujiunga na chama chochote, au kutokuwa na chama chochote, vivyo hivyo, hakuna kosa lolote, kwa mwanachama wa chama chochote cha siasa, kukihama chama chake, kujiunga na chama kingine chochote na hata kurejea kwenye chama chake, na wengi wamefanya hivyo ni haki yao ya kidemokrasia. ila mwanachama mwenye dhamana ya Uongozi wa kuchaguliwa, kisha kuiacha dhamana hiyo na kuacha Uongozi, kisa anahama chama na ameahidiwa atasimamishwa yeye, halafu ni kweli, na chama kinakubali, kinamsimamisha na kuwarudia wananchi wale wale aliowasaliti, kuwaomba wamachague tena!. Huu ni ujinga ambao Watanzania tusikubali.

Kuna Tofauti Kwa Kiongozi wa Chama Cha Siasa, kujiudhuru na Kuhama Chama na Kiongozi wa Kuchaguliwa Kuhama Chama?.
Kiongozi yoyote wa chama cha siasa, yuko huru kuhama chama chake na kuhamia chama kingine. Hakuna kosa kwa kiongozi yoyote wa chama chochote cha siasa, kukihama chama chake na kujiunga chama kingine, mtu huyo atakuwa hajafanya kosa lolote kisheria, ila atakuwa amewakosea watu wa chama chake waliomwamini na kumpa Uongozi, lakini hajafanya kosa lolote kwa Watanzania. Mfano Prof. Lipumba, alipojiuzulu Uongozi CUF, aliandika barua ya kujiuzulu na kutoa sababu zake za kujiuzulu, kama sababu zake ni za msingi, watu wote wenye burasa, watakubaliana nae!. Lakini aliporejea, alipaswa kuandika barua ya kuomba kurejea na kukubaliwa, ndipo arejee. Kitendo cha Prof. Lipumba kujitoa CUF na kutoa sababu za kujitoa, kisha kujirejesha, ili hali sababu zilizomfanya kujitoa, bado zingalipo, huku ni kuwafanya wana CUF kuwa ni wajinga!. Wale wote waliomkubali na kujirejesha huko, ni kukubali ujinga, wanachama wa vyama vya siasa, wasikubali kufanywa wajinga na viongozi wao. Ujinga huu unaofanywa na viongozi wa siasa, unapopata baraka za viongozi wa taasisi za umma kama Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, na Ofisi ya Bunge, kutambua kuwa kuna CUF 2, kunaacha maswali bila majibu, kuhusu utimamu wa viongozi wa taasisi hizi!.

Jee Kiongozi wa Umma, Rais, Mbunge, Diwani, etc, Anapojiuzulu Uongozi, ni Kosa?.
Jibu ni ndio, ni kosa kubwa kwa kiongozi wa umma aliyeaminiwa na kuchaguliwa, kuamua kujiuzulu uongozi wa umma kwa sababu za kijinga za kumuunga mkono kiongozi fulani!. Kiongozi yoyote wa chama chochote, aliyechaguliwa, na watu, baada ya kuchaguliwa, anakuwa ni kiongozi wa umma, na sio kiongozi wa chama chake, kuchaguliwa kwake, kunabeba dhamana kubwa ya watu wote, waliomchagua, wasiomchagua na hata ambao hawakupiga kura. Uongozi wa umma ni dhamana ya watu unaowaongoza. Mfano rais Magufuli, japo ni Mwana CCM, na alipendekezwa na CCM kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Tangu baada ya kupitishwa na Tume ya Uchaguzi kuwa mgombea wa rasmi wa urais, status ya Magufuli inabadilika kuwa mgombea wa taifa wa urais, akiwakilisha CCM. Vivyo hivyo kwa wabunge na madiwani.

Mgombea Akiishapitishwa na NEC Anakuwa Mgombea wa Taifa, Akishinda ni Kiongozi wa Wote, Kiongozi wa Umma, Kujiuzulu ni Usaliti.
Baada ya kuchaguliwa na kutangazwa na NEC kuwa ni mshindi, hapa sasa mgombea huyu ana change status, kutoka uwakilishi wa chama na kuwa ni kiongozi wa umma. Uchaguzi unakuwa umekwisha kwa mshindi kuchukua kura zote yaani (the winner takes it all), akiishaapishwa, sasa anakuwa sio kiongozi wa CCM, wala sio kiongozi wa waliomchagua, anakuwa ni kiongozi wa wote, waliomchagua, wasio mchagua na hata ambao hawakupiga kura, anakuwa ni rais wa Watanzania wote. Kitendo cha rais, mbunge au diwani wa kuchaguliwa, kujiuzulu uongozi wa umma kwa sababu zilizo nje ya uwezo wa kibinaadamu, kama ugonjwa, kitaeleweka, lakini kujiuzulu kwa sababu nyingine yoyote, japo ni haki yake kikatiba, kujiuzulu huku ni kuwasaliti wale wote waliokupa dhamana ya uongozi kwa kukuchagua, na ni kuisaliti dhamana yao kwako ya Uongozi wa umma kwa wengine wote uliokuwa ukiwaongoza, hivyo huku ni kuwakosea sana wapiga kura, ila hawana jinsi zaidi ya kuheshimu uamuzi wako, japo watajisikia vibaya kwa kujisikia kuwa wamekuwa let down na wewe. Hivyo wabunge wote waliojiuzulu ubunge na madiwani wote waliojizulu udiwani, ni kuwasaliti wale waliowachagua. Mtu wa aina hii aliyefanya usaliti huu, kurejea kuomba kuchaguliwa tena nafasi ile ile aliojiuzulu!, huu ni ujinga wa kupitiliza!.

Viongozi wa Umma Wanaojiuzulu Uongozi wa Umma, ni Usaliti wa Umma Sio Wazalendo, ni Mamluki wa Vyama vya Siasa, Tusiwakubali Mamluki Hawa!.
Kuchaguliwa kwa kura, ni binding contract kati ya mgombea na wapiga kura kuwa utawaongoza kwa Kipindi Fulani. say miaka mitano. Kujiuzulu kwa sababu yoyote ile ni breach of contract. Ukiisha breach contract, huwezi kurudi kutaka tena contract ile ile ulio breach!. Kama ilivyo kwa mkataba wa ndoa, msingi wake ni mapenzi baina ya wanandoa, lakini hata ikitokea mbele ya safari, mwanandoa mmoja kujikuta mapenzi yamepungua, au yameisha, hawezi kujitokea tuu nje ya ndoa kupata penzi la ziada kujazia pale mapenzi yalipopungua, huku kutakuwa ni kusaliti ndoa!. Vivyo hivyo kwa viongozi hawa waliochaguliwa na kisha kujiuzulu Uongozi wa umma kwa sababu ya kuhama chama, ni usaliti kwa umma wa waliowachagua na wanaowaongoza, ni breach of trust, tusiwaamini tena na tusiwakubalie tena kurudi, wasije wakatuletea tena ujinga ule ule!.

Kama Kujiuzulu Uongozi wa Umma ni Usaliti, Chama Kinachompitisha Msaliti Kugombea Tena, ni Kuwafanya Wapiga Kura ni Wajinga.
Kama nilivyojenga hoja hapo mwanzo, viongozi wa umma wanaojiuzulu kwa sababu ya kuhama vyama, ni usaliti na kukosa uzalendo, lakini msaliti anapojiuzulu uongozi kwa ajili ya kuhama chama, halafu anaomba kugombea nafasi ile ile aliyojiuzulu, huku ni kuwadhihaki wapiga kura wa eneo husika, huku mimi nakuita ni ujinga na umamluki wa kisiasa. Ila chama kinachompitisha mamluki wa aina hii kugombea jimbo lile lile, huku mimi nakuita ni kuwatukana wapiga kura wa eneo husika, ni kama kuwafanya wajinga!. Jee Wapiga kura wa Kinondoni na Siha ni wajinga?. Jibu litapatikana kwa matokeo ya uchaguzi wa marudio, ila wito wangu ni, Watanzania tusikubali kufanywa wajinga na vyama vya siasa!, vyama vikituletea ujinga, tusiukubali ujinga huo, ila pia kwa vile miongoni mwetu, tunaweza kuwa na wajinga wengi kuliko tunavyojidhania, hivyo sitashangaa, kama CCM inatuletea ujinga huu kwa majimbo ya Kinodhoni na Siha na bado tukauchagua ujinga huo!.

Mwalimu Nyerere Alikataa Ujinga ile 1995 Kule Musoma, Kwa Kuukataa Ujinga wa CCM, na Bado Akawa Mwana CCM Mzuri!. Wana CCM wa Kinondoni na Siha, Msikubali Ujinga huu wa CCM!.
CCM japo ni chama kikubwa, na kikongwe, na kimefanya mambo mengi, makubwa na mazuri lakini pia CCM sio malaika, kuna mambo mengine madogo madogo ya kijinga ambayo CCM imefanya, na moja ni hili la kukiuka kanuni zake za uchaguzi na kutusimamishia wagombea wasaliti mamluki waliojiuzulu majimbo hayo hayo. Nikisema Chama kinafanya mambo ya kijinga, ninamaanisha wanaofanya ujinga sio chama kama chama, bali ni viongozi wa CCM ndio wanaofanya ujinga huu. Hii sio mara ya kwanza kwa viongozi wa CCM kufanya ujinga. Huko nyuma kuna ujinga fulani CCM iliufanya, Baba wa Taifa hili, Mwalimu Nyerere, alikasirika sana kwa ujinga huo, akasema kwa hasira kuwa "CCM sio mama yangu au baba yangu". Mwalimu akakiri kufanya makosa, kwa kusema "kufanya kosa sio kosa, kosa ni kurudia kosa", na hakuishia hapo, aliwalaumu viongozi waliokuwepo kwa kusema, kila awamu ina mazuri yake, na ina mengine ya kijinga. Akashangaa viongozi waliomfuatia badala ya kukumbatia mazuri, wao walifanya mambo ya kijinga!, hivyo akajiapiza hawezi kukubali ujinga!.

Mwalimu Nyerere Akataa Ujinga wa CCM!.
Hivyo katika uchaguzi wa ubunge wa jimbo la Musoma Vijijini mwaka 1995, CCM iliwatelia mgombea mwenye ujinga fulani, na Mwalimu Nyerere akasema wazi wazi, hawezi kuukubali ujinga huo, hivyo hakuubali ujinga ule, na alisema wazi na kumpigia kampeni mgombea wa NCCR-Mageuzi, na matokeo yake mgombea wa CCM akapigwa chini, hivyo kijiji cha Mwalimu Butiama, kikawa chini ya mbunge wa upinzani, na Mwalimu kukiri kumpigia kura mpinzani kwa ngazi ya ubunge kwa sababu CCM iliwaletea ujinga!.

Wapiga Kura wa Kinondoni na Siha, Tusikubali CCM Ituletee Ujinga!.
Vivyo hivyo kwa wana CCM ambao ni wapiga kura wa majimbo ya Kinondoni na Siha, hivi ni kweli CCM kilikosa kabisa wanachama waadilifu, wenye sifa kuwasimamisha katika majimbo hayo, hadi kuwachukua wagombea, mamluki wa kuokoteza, waliowasaliti wananchi wa majimbo hayo na kuwasimamisha tena!. Kitendo hiki ni kuiaibisha CCM, kuonekana haikuwa na watu hadi kuwategemea mamluki wa kisiasa?!. Yaani bila wanachama wa vyama vya upinzani kujiunga CCM, that means CCM is nothing!, empty!, haina watu safi wa kuwasimamisha!. Kitendo cha kiongozi kujiuzulu nafasi fulani ni kuutema uongozi, ni kama kutapika!, kitendo cha kiongozi huyu huyu aliyejiuzulu, halafu kuutaka tena uongozi ule ule, aliouacha, ni kama kurudia kula matapishi yake!, hivyo kumchagua tena kiongozi wa aina hii ni kama kinyaa fulani kwa sisi wapenda uadilifu usiotia shaka, hivyo kitendo cha CCM kuwasimamisha tena, ni kuwafanya wana Siha na Wana Kinondoni kuwa ni wajinga!. Hivyo natoa wito kwa Wana Kinondoni na wana Siha mnaomkubali Mwalimu Nyerere, na kuukubali msimamo wake katika kukataa ujinga ujinga, kamwe msikubali kufanywa wajinga.

Wasalaam.

Paskali
Update,
Mchangiaji huyu amenielewa vizuri na amefafanua vizuri kwa kutumia lugha rahisi na nyepesi.
Msemaji Ukweli umetoa nadharia potofu kwamba ' ni ujinga kumwambia mwingine ni mjinga." Nadharia potofu kwa sababu kila mtu anajua kuwa wapo watu wajinga. Na ujinga ni kutokujua jambo fulani. Ujinga siyo dhambi na kuwa mjinga siyo kosa. Kosa ni kujifanya mjinga. Ukijifanya ni mjinga unapanda cheo unakuwa Mpumbavu. Nadhani Ndg Mayalla alichokuwa anajenga katika hoja yake ni kuwa tusikubali kufanywa wajinga wakati sisi si wajinga. Wewe unayejiita Msemaji Ukweli ambaye unakumbatia na kuukubali ujinga huu, unajivika cheo kipya wewe mwenyewe. Kwa kuwa umekubali ujinga (mtu kula matapishi yake mwenyewe) wakati ukijua kuwa anachofanya ni ujinga. Ccm wanawafanya wananchi ni wajinga. Mtu anayetambua kuwa kinachofanyika ni ujinga, ama analazimishwa kufanya ujinga, naye akakubali kutenda ujinga (kumchagua mtu aliyekwisha kuwa mbunge, wa bunge hilo hilo, kipindi hicho hicho, kuwawakilisha watu hao hao) wewe ukakubali kutenda ujinga huo, wa kumchagua tena, hata baada ya waelimisha jamiii kama Ndg Mayalla kukufahamisha kuwa kufanya hivyo ni ujinga, lakini wewe ukaendelea kufanya ujinga huo, basi wewe ni mjinga squared, ama kwa sifa nyingine ni mpumb...vu. Why kwa sababu umefanya tendo la kijinga wakati unajua (baada ya kufahamishwa) kuwa tendo husika ni la kijinga, lakini ukaendelea kulifanya tendo hilo, basi mtu huyo ni mpumbavu. Ccm wasitufanye sisi ni wapumbavu.
Asante kwa ufafanuzi huu.
P
 
Wewe si kwenye bandiko lako la kwanza ulisema hupigi kampeni? Umegundua maji yako shingoni na sasa unaanza kuonyesha sura yako kamili ili kujaribu kuinasua boti ya kampeni inayozama!

Halafu hii dhana ya kuwaona wengine ni wajinga kwa sababu wanamtazamo na utashi tofauti na wako katika suala la kuchagua au kuchaguliwa (demokrasia) mnaitoa wapi? Hujui kuwa kura ni moja tu na haina madaraja ya wajinga na wasio wajinga.

Katika demokrasia ya kuchagua, wanachofundishwa wapiga kura ni namna ya kupiga kura na sio nani wa kumchagua.

Kuchagua ni utashi wa mchaguaji. Huwezi kumwambia ni mjinga kwa sababu hakumchagua yule ambaye utashi wako ulitaka achaguliwe. Ndiyo maana anayechaguliwa anakuwa ni kiongozi wa wote(waliomchagua na hawakumchagua)

Mimi nadhani ni ujinga kudhani wengine ni wajinga katika masuala ya demokrasia katika kuchagua na kuchaguliwa, ndio maana bungeni kuna MaProf, PhD, Form Four leavers mpaka darasa la saba. Hawa wote wanafanya kazi moja bungeni ambayo ni kuwawakilisha wananchi, kutunga sheria na kuisimamia serikali.

Unamleta Mwalimu Nyerere kwenye bandiko lako ili uuze propaganda ambayo haina mantiki au haishabihiani na hoja za Mwl. Nyerere.

Unaposema Mwl. Nyerere alimkataa mgombea wa hovyo huku akimuuza Mkapa ni sawa na kuwaambia wapinzani kuwa wao pia niwa hovyo kwa sababu walimkataa Mkapa na wabunge wengine ambao walikuwa wanauzwa na Mwl. Nyerere kama wagombea wasiokuwa wa hovyo.

Utawaokota tu wale ambao hawakuwepo kipindi hicho au hawajui historia ya Mwl. Nyerere.

Kwa kukusaidia, hata huko Uingereza kuna wabunge wanajiudhuru ubunge kwa kutokubaliana masuala fulani ndani ya serikali au chama chao na wanagombea tena katika uchaguzi mdogo na kushinda. Huwezi kusikia wanaowachagua wakiambiwa ni wajinga.

Soma hii LINK>>>> David Davis resigns from Commons

LINK>>>David Davis:Why I am resigning

Hakina kitu kibaya kama unafiki katika siasa na kudhani wewe unajua zaidi ya wengine katika masuala ya utashi kidemokrasia
 
Back
Top Bottom