Kinondoni, Dar: DC Ally Hapi aagiza mtumishi wa umma kuwekwa ndani saa 48 kwa kumzimia simu!

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,007
2,675
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ameagiza Jeshi la Polisi kumuweka ndani siku mbili, Afisa Uthamini wa wilaya hiyo, Einhard Chidaga kwa kosa la kutotekeleza majukumu yake pamoja na kudharau wananchi kitendo kinachodaiwa kusababisha uwepo wa migogoro ya ardhi katika wilaya yake .

Hapi ametoa maagizo hayo leo katika mkutano wake na wananchi wa Kata ya Wazo uliofanyika kwenye viwanja vya Mkanada.

Baada ya wananchi wengi kulalamika kutolipwa fidia zao na Manispaa licha ya uthamini wa viwanja vyao kufanyika, na kwamba ilitakiwa Afisa Uthamini huyo awepo katika mkutano huo kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa malalamiko ya wananchi lakini hakutokea katika mkutano huku simu yake ya mkononi ikiwa haipatikani.

Hata hivyo, Hapi alisema kuwa Afisa huyo hatekelezi majukumu yake inavyotakiwa kwa kuwa tangu ameanza ziara ya kutembelea wananchi ili kujua kero na changamoto zao, Chidaga hajawahi kuhudhuria katika ziara yake.

“Polisi mtafuteni huyo mtu, alale ndani masaa 48. Anajua kabisa kuna mkutano wa wananchi na kwamba anahitajika kusikiliza na kutoa majibu ya malalamiko ya wananchi lakini amezima simu,” amesema.
 
Kuna tatizo la kukabidhiana nguvu zaidi ya uwezo wa mhusika, na nguvu zaidi humlevya aliye nazo ndiyo hapo unakuta mwenye nguvu anatenda kama amelewa.

Simu haipatikani, umejuaje kama kakuzimia makusudi? Umehakikisha? Kwahiyo baada ya saa 48 unampeleka mahakamani kisa kakuzimia simu?
 
Huyo mkuu wa wilaya ana akili kweli?
Mambo ya utumishi wa umma ni mambo ya kiofisi na sio kutafutana binafsi. Simu ya mkononi ni mawasiliano binafsi, mhusika anapaswa kupigiwa kwenye simu ya ofisi tena muda wa kazi tu.

Mkuu wa wilaya unafanya ziara zako binafsi, nyingi zikiwa nje ya muda wa kazi, tena za kushtukiza shtukiza halafu unategemea watumishi wa serikali wanaojitambua wawe wanafuatana na wewe kama kupe?
 
Hapi kumbe na ww unatembea mule mule mwa mako dah au boss mktukufu ndio anapenda style hyo
 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ameagiza Jeshi la Polisi kumuweka ndani siku mbili, Afisa Uthamini wa wilaya hiyo, Einhard Chidaga kwa kosa la kutotekeleza majukumu yake pamoja na kudharau wananchi kitendo kinachodaiwa kusababisha uwepo wa migogoro ya ardhi katika wilaya yake .

Hapi ametoa maagizo hayo leo katika mkutano wake na wananchi wa Kata ya Wazo uliofanyika kwenye viwanja vya Mkanada.

Baada ya wananchi wengi kulalamika kutolipwa fidia zao na Manispaa licha ya uthamini wa viwanja vyao kufanyika, na kwamba ilitakiwa Afisa Uthamini huyo awepo katika mkutano huo kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa malalamiko ya wananchi lakini hakutokea katika mkutano huku simu yake ya mkononi ikiwa haipatikani.

Hata hivyo, Hapi alisema kuwa Afisa huyo hatekelezi majukumu yake inavyotakiwa kwa kuwa tangu ameanza ziara ya kutembelea wananchi ili kujua kero na changamoto zao, Chidaga hajawahi kuhudhuria katika ziara yake.

“Polisi mtafuteni huyo mtu, alale ndani masaa 48. Anajua kabisa kuna mkutano wa wananchi na kwamba anahitajika kusikiliza na kutoa majibu ya malalamiko ya wananchi lakini amezima simu,” amesema.
Hiyo simu ni ya ofisi au yake binafsi? Alishawahi kumpa hela ya muda wa maongezi?
 
Back
Top Bottom