Kingwangallah: Tunaomba Albaldir Uliyotuahidi

Kingwangallah: Tunaomba Albaldir Uliyotuahidi

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2009
Posts
3,444
Reaction score
265
Baada ya ndugu yetu Dr. Ulimboka kutekwa na hatimaye kuteswa na wanaosadikika kuwa Wana usalama wa Jeshi la polisi, licha ya Dr. Ulimboka kumuomba ACP Ahmed Msangi Kumrudishia Simu na Wallet yake, hadi wa leo, hakuna yeyote aliyekamatwa kutokana na tukio hilo Mbaya zaidi, mshukiwa namba moja kapewa ulaji wa kuunda tume ya kuchunguza utekaji nyara huo.

Wana CCM waadilifu tunajiona mayatima ndani ya chama. Serikali yetu imekuwa ya wenda wazimu. Ni kama vile hatuna serikali, kwa maana hiyo, tunaomba ndugu yetu Mh. Kingwangallah kutusaidia tuweze kufanya maombi ya "Albadilr" ili wahusika wapata adhabu ya mola, kwani serikali haionyeshi ushirikiano wa kutenda haki. Mtashangaa masikini watatu wanabambikiziwa hii kesi mbaya.

Waislamu na Wakiristo, wazalendo wote tushirikianeni tutafuta njia mbadala ya kukomesha vitendo kama hivi ili hawa manyanga'au ndani ya polisi wapukutike mmoja baada ya mwingine. Wanalindana na Bunduki, sisi imani yetu ndio ulinzi wetu. Tuone kati ya Mungu (allah) na Bunduki nani ni mlinzi mkubwa
 
Kwanza akamwambie Mheshimiwa Spika wa bunge la the comedy airishe hiyo bajeti ili wajadili ripoti ya Mheshimiwa Margareth Sitta ya(Kamati ya kudumu ya afya na ustawi wa jamii) halafu turudi kwenye michezo yetu ya kawaida ya usanii bungeni.Ukiwa stressed kazini ukirudi nyumbani pata kiburudisho cha vituko Mjengoni !
 
Akili mbovu na huyo Kigwangwala wako! Msituletee habari zenu za uchawi hizo! It's un-professional.
 
Akili mbovu na huyo Kigwangwala wako! Msituletee habari zenu za uchawi hizo! It's un-professional.
Uchawi wapi wewe, subiri ahlul lbadir ije utaona wanavyopukutika hapa; na ukiniudhi nakwambia nitanuwia na wewe unayetudhihaki uwemo!
 
Uchawi wapi wewe, subiri ahlul lbadir ije utaona wanavyopukutika hapa; na ukiniudhi nakwambia nitanuwia na wewe unayetudhihaki uwemo!

Embu peleka ujinga wako huko, uislamu gani huu siku hizi
 
Akili mbovu na huyo Kigwangwala wako! Msituletee habari zenu za uchawi hizo! It's un-professional.

Heshima mbele Mkuu!
Raia wanapobaki kwenye hali ya Ukiwa wanakuwa hawana jinsi. Kama hiyo unprofessional wal ndio njia ya kutafuta haki, basi hatuna jinsi. Nyie na majumba yenu yanalindwa na Askari wa bunduki, sisi tusio na walinzi mnaotuteka tuna kuwa hatuna jinsi ila kukimbilia popote pale kutafuta msaada. Tukija kwa pole kutafuta haki tunaombwa rushwa na kubambikiziwa kesi,

Tukienda mahakamani tunanyimwa haki zetu. Kwa hiyo kuwaombea vifo ndio dawa pekee ambayo itatusaidia ili uishi kwa amani
 
Mimi sio hao unaowazungumzia, mimi ni mlalahoi wa chini mno! But tunapopishana ni sehemu ndogo sana, kuwa suala la Kigwangwala kuomba watu wasome Albaldir ni wendawazimu, nilishamwuliza kuwa "wewe ni daktari wa darasani???" Nadhani umenielewa hapo.
 
CCM inachungulia kaburi kwa kweli, ukiona hadi bunge linaamuliwa na serikali kuhakikisha linazuia mijadala ya kulaani serikali na linaruhusu mijadala ya kumdhalilisha Dk Ulimboka haihitaja hata elimu ya std 7 kujua serikali inahusika. Mbaya zaidi Mh Kingwangallah alikuwa kimya akaacha chama kiwakilishwe na mzinzi wa kitaifa Mwigulu na Bar Maid mstaafu Stella Manyanya

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Uchawi wapi wewe, subiri ahlul lbadir ije utaona wanavyopukutika hapa; na ukiniudhi nakwambia nitanuwia na wewe unayetudhihaki uwemo!
It's too funny, tena bora uliweka picha yako kabisa, nilikuwa nasoma statement yako hapo then naangalia picha yako una-smile hakika haviendani hata kidogo. Siwezi kuwemo hata iweje! Jaribuni... itawarudi hiyo!
 
Uchawi wapi wewe, subiri ahlul lbadir ije utaona wanavyopukutika hapa; na ukiniudhi nakwambia nitanuwia na wewe unayetudhihaki uwemo!

kaka Kigwangalla, una imani na tume iliyoundwa kuchunguza unyama aliofanyiwa Dk.Ulimboka?
 
It's too funny, tena bora uliweka picha yako kabisa, nilikuwa nasoma statement yako hapo then naangalia picha yako una-smile hakika haviendani hata kidogo. Siwezi kuwemo hata iweje! Jaribuni... itawarudi hiyo!
huwa hatujaribu...wewe sema uko tayari nikuweke na wewe kwenye kundi la wenye kumdhihaki MUNGU?
 
Mimi sio hao unaowazungumzia, mimi ni mlalahoi wa chini mno! But tunapopishana ni sehemu ndogo sana, kuwa suala la Kigwangwala kuomba watu wasome Albaldir ni wendawazimu, nilishamwuliza kuwa "wewe ni daktari wa darasani???" Nadhani umenielewa hapo.
Kila mtu na imani yake, mtuache na ya kwetu! wasiwasi wa nini?
 
Nimegundua assaulters wa Uli wamo humu humu JF kujibu hoja, naona hii ya ahlul badr imewatisha sana...na hatuachi, acha tushike udhu tunuwie na mtakiona cha mtema kuni!

Ujinga wa dini unakusumbua go ahead
 
Embu peleka ujinga wako huko, uislamu gani huu siku hizi

-Ndugu yangu, kama hauusiki mbona uwe na wasi wasi? Ukimya msafi ungeshukuru kwa maana hao waalifu wataletwa mbele za haki pasipo rushwa. Wewe kupinga wakati unajua fika kwamba wamefanya unyama inaleta maana tofauti kwamba; wewe ni mmoja wa washukiwa. sisi tunakimbilia albaldir kwa maana hatuna jinsi nyingine na mbele za Mwenyezi Mungu (Allah ) hakuna rushwa wala uonevu kila mtu anapewa haki yake. Hadi na Ahmed Msangi naye anapewa haki yake. Kama alimteka ulimboka atabaki salama na kama kweli alishiriki, basi atapata thawabu yake...kama unaona haina tija, tupe njia mbadala itakayotupa haki... Tafakari
 
hii ndio dawa pekee ya kuwapukutisha. Ila sasa kama mkuu wa nchi alihusika haitampata?
 
Nimegundua assaulters wa Uli wamo humu humu JF kujibu hoja, naona hii ya ahlul badr imewatisha sana...na hatuachi, acha tushike udhu tunuwie na mtakiona cha mtema kuni!

Tunaomba usimwe faster basi machungu hayajaisha
 
Uchawi wapi wewe, subiri ahlul lbadir ije utaona wanavyopukutika hapa; na ukiniudhi nakwambia nitanuwia na wewe unayetudhihaki uwemo!

Wewe jamaa unachekesha sana. Hiyo ahlul Ibadir yako haifanyi kazi bana.

Huyo Msangi awekewe bounty tu. Mimi hapa nipo tayari kutoa dola 500. Popote pale alipo huyo jamaa ajue kuwa yuko wanted, dead or alive.

Binafsi nikikutana naye lazima nimtwange mingumi. His ass is grass.
 
Back
Top Bottom