WanaJF, kuna huyu mzee Kingunge Ngombale Mwiru ambaye amekuwa mtu muhimu sana katika siasa na sera mbali mbali za Tanzanai tangu enzi za Mwalimu Nyerere mpaka sasa. Huyu mtu alijulikana kama kichwa kilichokuwa nyuma ya Nyerere kuhusu uanzishaji na uendelezaji wa siasa na sera za Ujamaa hapa nchini.
Hakuwa mjamaa tu bali alikuwa Mkomunisti. Alikuwa na bado ni mtaalam wa Propaganda wa CCM. Hakuwa anamwamini Mungu. Katika ulaji wa viapo vya ofisi yeye alikuwa hatumii Biblia wala Quran.
Kwa hiyo mambo mengi yaliyoleta hadha kubwa enzi za Nyerere kama vijiji vya ujamaa inawezekana yalitokana na ushawishi wa Kingunge. Leo hii inashangaza yeye bado ni mshauri mkuu wa Kikwete kisiasa katika enzi hizi za Ubepari kubuhu na ufisadi.
Familia yake (mke na watoto) wanahusishwa na mikataba tata kama ule wa Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo. Tunapoangalia nyuma na kuangalia kwa macho mapaya huko tulikotoka naomba tumjadili huyu mzee, hasa wale wanaomfahamu kwa karibu.
Na kwa kuwa yeye bado yuko hai basi atapata nafasi ya kuelezea au kukosoa yale yanayosemwa. Tusingoje afe halafu ndiyo tuanze kumsifia au kumkosoa. Nawakilisha.