Kingunge Ngombale Mwiru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kingunge Ngombale Mwiru

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ruge Opinion, Aug 3, 2011.

 1. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  WanaJF, kuna huyu mzee Kingunge Ngombale Mwiru ambaye amekuwa mtu muhimu sana katika siasa na sera mbali mbali za Tanzanai tangu enzi za Mwalimu Nyerere mpaka sasa. Huyu mtu alijulikana kama kichwa kilichokuwa nyuma ya Nyerere kuhusu uanzishaji na uendelezaji wa siasa na sera za Ujamaa hapa nchini.

  Hakuwa mjamaa tu bali alikuwa Mkomunisti. Alikuwa na bado ni mtaalam wa Propaganda wa CCM. Hakuwa anamwamini Mungu. Katika ulaji wa viapo vya ofisi yeye alikuwa hatumii Biblia wala Quran.

  Kwa hiyo mambo mengi yaliyoleta hadha kubwa enzi za Nyerere kama vijiji vya ujamaa inawezekana yalitokana na ushawishi wa Kingunge. Leo hii inashangaza yeye bado ni mshauri mkuu wa Kikwete kisiasa katika enzi hizi za Ubepari kubuhu na ufisadi.

  Familia yake (mke na watoto) wanahusishwa na mikataba tata kama ule wa Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo. Tunapoangalia nyuma na kuangalia kwa macho mapaya huko tulikotoka naomba tumjadili huyu mzee, hasa wale wanaomfahamu kwa karibu.

  Na kwa kuwa yeye bado yuko hai basi atapata nafasi ya kuelezea au kukosoa yale yanayosemwa. Tusingoje afe halafu ndiyo tuanze kumsifia au kumkosoa. Nawakilisha.
   
 2. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2011
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hivi bado ni mbunge wa kuteuliwa tu?
   
 3. Researcher

  Researcher Senior Member

  #3
  Aug 3, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mjadala wa kushindwa au kufanikiwa kwa ujamaa inaweza kuwa topic nyingine. Naona tusimame kwenye hoja ya uadilifi, uzalendo na nidhamu iliyokuwepo kwenye utawala wa mwalimu.

  Alichokosa mzee wetu Kingunge ni utashi wa kuwapisha chipukizi kuchukua hatamu..kama kweli aliamini katika siasa za Mwalimu, angefikia hatua ya kuamua mwenyewe kwamba siasa sasa basi ngoja niwapishe vijana, ila alikuwa mzito kufanya hivyo...

  Ila kwa upande wa hizi tabia za siku hizi za kujilimbikizia mali, kuhujumu nchi kwa kununuliwa dhidi ya mikataba mibovu na hata kushiriki makundi ya siasa, huyu mzee sijamsikia kabisaaaa..bado kuna damu ya Mwalimu ndani yake.Nakiri kwamba mwanae anamuangusha kwa kiasi fulani.

  Yangu ni hayo.
   
 4. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  hachafuliwi na mwanaye sababu mikataba yote michafu ya familia yake imepatikana kwa influence yake,infact ni miradi yake..kwa mstari mmoja nasema kingunge alijifanya mjamaa kwa kumuogopa nyerere..huyu ni fisadi period
   
 5. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145


  Mungu Atajibu Soooooooooooon and Very Soooooooooooon
   
 6. Rohombaya

  Rohombaya JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 8,261
  Likes Received: 3,095
  Trophy Points: 280
  Wakati wa mwalimu aliaminiwa lakini wakati wa mafisadi amekaa na mafisadi wakamuambukiza ufisadi naye akaona afanye ufisadi... ukikaa na rafiki mvuta bangi ama nawe utavuta ama watu watasema unavuta bangi.
   
 7. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  He's but an old brat!
   
 8. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Amekuwa overpowered na mkewe, Mimi nimewahi kufanya mawasiliano ya kibiashara na familia ya mzee Kingunge, believe me Mzee Hana kauli kwa yule mama chotara wa Kihaya. Mengi yanayotokea yanafanywa behind his back
   
 9. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  CCM wanapeana vya kula, toka AZIMIO LA ZANZIBAR kila mtu anaweka kapuni

  We angalia nyumba aliyokuwa anaishi wakati wa Uhai wa JK na Sasa hivi...
   
 10. nditolo

  nditolo JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 1,335
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Yeye binafsi anahusishwa kumiliki mapanton yote pale kigamboni kwa mgongo wa serikali.
   
 11. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  mzee si mbaya sana, kinachonikera ni influence zao kutumiwa na watoto wao ili kujinufaisha. Inakera pale unapokumbuka mtoto flani wa kigogo alikuwa kilaza lkn leo amepata platform ndo anafanya maamuzi yetu wote na ndo anafaidi keki yetu tena kwa mbwembwe. Upuuuuuzi
   
 12. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ngombale Mwiru alivuta hisia za wasomi wa mrengo wa kulia mwishoni mwa miaka ya sitini alipokuwa msomi pekee kulikosoa azimio la Arusha kwa kuzungumzia demokrasia bila ya kufafanua ni aina gani ya demokrasia iliyokuwa ikizungumzwa; ya kilibrali au kijamaa? Katika siku na miaka iliyofuatia azimio la Arusha Ngombale alijipambanua yakuwa alikuwa katika mrengo wa kushoto wa baba wa taifa. Nakumbuka mwaka 1971 wakati huo akiwa RC wa Dsm alijaribu kutumia mgogoro uliokuwepo kati ya wanafunzi wa mlimani na Msekwa kwa lengo la kuwang'oa wale wote waliokuwa wamepewa dhamana kubwa kubwa na huku wakiwa kwenye mrengo wa kulia kisiasa. Ngombale alipata pigo kubwa alipohenguliwa kutoka katika ukuu wa mkoa baada ya kukataa kuunga hoja ya serikali bungeni. Hadha zilizomkuta katika kipindi hicho inaelekea zilimfanya alegeza kamba katika msimamo wake kisiasa; maana aliporejeshwa katika ukuu wa mkoa wakati huo kukiwepo na uhaba wa bidhaa muimu alimwachia mke wake kushiriki katika ulanguzi wa bidhaa muimu kwa kutumia jina lake. Mtindo huu wa mke wake Ngombale wa kushiriki katika biashara zenye utata chini ya mgongo wa mumemwake unaendelea mpaka leo. Kwa kuzingatia ukweli huo ni dhahili mzee Ngombale katika kipindi chote alipokuwa akifanya kazi chini ya mwalimu alikuwa ni mjamaa wa jukwaani lakini kwa ndani alikwishaanza kuutamani ubepari. NNdiyo maana mpaka sasa mzee huyo ameendelea kuwa na ushawishi mkubwa katika tawala za sasa, Kwa mfano inasemekana amechangia sana katika uteuzi wa Mkama ambaye ni kama mwanafamilia wake, kstiks nafasi ya katibu mkuu wa CCM.
   
 13. M

  Mantaleka Senior Member

  #13
  Aug 3, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mhn, kwishney hakuna kitu kutoka kwa huyo mzee, hatakumjadili hakuna maana, mwacheni asubiri siku zake zifike akawajibike kwa muumba wake.
   
 14. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kingunge ni mnafiki, ameugeuka ukomunist kuliko hata mabepari. Yeye amekuwa mstari wa mbele kujilimbikizia mali kwa kuliibia Taifa na kampuni ya mwanaye Kinjiketile iliyokuwa inakusanya ushuru wa parking jijini Dar. Alikuwa anamsanifu Mwl. JKN.
   
 15. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Huyo mzee nyerere alisha mjua ni mnafiki sana, hakuwahi kuwa wairi wakati wa wake, mkapa akajipendekeza, nae akamsaliti ili ansaidie kikwete, baade kamstukia, kamtoa kuanzia cc, na si mbunge sasa, sema tu atakuwa anaende ikulu kwa kuwa amepazoea sana
   
 16. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #16
  Aug 3, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Yeye ni maarufu tu kwa kuwa hafungamani na dini yoyote. Mwalimu alimjua kuwa ni mbovu,ndio maana pamoja na umaarufu wake hajawahi ukwaa uwaziri mkuu. Ni mtu asiyekuwa na msimamo na hupenda kujikomba kwa kila utawala. In fact mzee kama huyu angekuwa nguzo kubwa kwa kipindi kama hiki nchi inaliwaa na kuangamia kwa ufisadi. Kwa sasa bora afe tu, hana mpango wowote
   
 17. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Mimi nilitegemea kwa ukomavu na ukongwe alionao basi angejali zaidi maslahi ya taifa kwanza kuliko chama kama walivyo wakongwe wengine
   
 18. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mwanae Alishaua Mtu Kwa Mgongo wake Hakufungwa Kesi Ikaisha na Wanatesa tu Kwenye Nchi Yenu huku wakimiliki sehemu zote za jiji la dar zenye vinafasi vya kupark gari hadi zisizo ruhusiwa.. Adhabu zao Siku zao Zikifika wawekwe panapo stahiri
   
 19. montroll

  montroll JF-Expert Member

  #19
  Aug 4, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 288
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  This is a good topic of some sort.
  If politics is an art, then among the very few early elites of this country, the pre and post colonian elite politicians who understood that siasa ni usanii it is this now-frail-old -man,kingunge. He studiet the art of it,and became exceedingly good artist, ready and able to assume any role with any team coz he bellieved in any ting but wht u blv, smart,cunning, ambitous. Learned and believed and became an addict of art. To believe and adopt play any musicwith any band of any language with his own orinal original language.

  Ndio maana hata sasa watu wengi hawajui kwa hakika kama ni msafi au mchafu. ni msanii wa siasa wa hali ya juu, mnafiki,muongo mkweli,mwaminifu,mponyaji,muumiza, ni msanii. Mjinga,mwerevu, mpole na mkali, mkupukaji,anahekima but he does/did/doing with the same languagge, same song,same stlye,ujamaa.

  Hata mwalimu hakuweza hili, kucheza bongo fleva lakini kuimba twist songs,akajitoa.

  Kingunge is a fiction and real,a devil in the dept of politics.
  I will not be wrong(i stand to be challenged) if i say that

  kingunge is a raper of politics


  <br />
  <br />
   
 20. T

  Taso JF-Expert Member

  #20
  Aug 4, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,649
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Check your history facts first.

  You make a positive claim "Huyu mtu alijulikana kama kichwa kilichokuwa nyuma ya Nyerere kuhusu uanzishaji na uendelezaji wa siasa na sera za Ujamaa hapa nchini," halafu kumbe uhakika huna unaaza ku guess guess "enzi za Nyerere kama vijiji vya ujamaa inawezekana yalitokana na ushawishi wa Kingunge."

  Hujui kitu hicho, au kitu at all, ondoa forthwith hiyo claim ya juu kwamba Kingunge alikuwa kichwa nyuma ya Nyerere. In the annals of political history of Tanzania no one has ever been chronicled to be the brain behind Nyerere.

   
Loading...