Kingunge akerwa, akemea yanayoendelea ndani ya CCM

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
61,439
Reaction score
100,725
Pole sana Nape Nnauye naona nyota yako inazidi kufifia, mara nyingi kumekua na taarifa za wewe kushushwa jukwaani na Kinana kutokana na kauli zako, juzi kati hapa ukaja na goli la kidole mara na mkono na sasa umekuja na jipya!

Mzee Kingunge amejitokeza hadharani na kuonya kuwa kauli zako zinakizika chama chako na mimi nasema mfe tu maana tumechoka! Kingunge amethibitisha kuwa huko ndani ya CCM kuna fukuto kubwa na wala sio Demokrasia tena bali ni Domg ghasia ndio iliyojaa huko CCM.

Pumzikeni kwa amani

===========
Mwananchi:

Kingunge amtolea uvivu Nape Nnauye

 
Sasa ni dhahiri kuwa vita ya CCM kati ya Kingunge Ngombale Mwiru (mzee) na rais Jakaya Kikwete imeshika kasi baada ya kada huyo wa siku nyingi wa CCM kuweka bayana kuwa rais Kikwete sasa ameifanya CCM kama chama chake binafsi.

Kingunge pia amesema kuwa endapo Kikwete ataendelea kushikilia msimamo wake, CCM itaanguka katika uchaguzi mkuu ujao.

Hayo ameyasema wakati akihojiwa na ITV habari.

Mimi nipo Dodoma kusubiri maamuzi ya kamati ya maadili na usalama ya CCM na nitawaletea kila ninachopata.
 

Kingunge zama zake zilishapita. Wamwache mwenyekiti wao aongoze chama mpaka kife kama ilivyotabiriwa.
 
Nimemsikia Kingunge ITV anasema chaguo la watu ni EL na imejulikana hivyo kutokana na umati uliokuwa unamuunga mkono ktk kukusanya wadhamini.
Na kasema asipopita EL,basi chama ndio kimejizika
 
Kingunge anazeeka vibaya. Huyu mzee kigeugeu hana hata chembe ya haya.
 
kiujumla wote kingunge na nape hawakitendei haki chama chao. ni kingunge aliyetoa kauli ya kutatanisha kwamba lowasa akikatwa patachimbika.
 
Nimemsikia Kingunge ITV anasema chaguo la watu ni EL na imejulikana hivyo kutokana na umati uliokuwa unamuunga mkono ktk kukusanya wadhamini.
Na kasema asipopita EL,basi chama ndio kimejizika

mkuu kingunge mbele ya lowasa haambiliki.
 

Lakini bw. Sam wote tumeisikiliza hiyo taarifa ya habari na hakuna popote alipomtaja yeyote kwa jina. Angeweza akawa alikuwa anamlenga Kikwete au Nape.
 
Ukweli CCM migogoro na hawa wazee wenu inawangusha penda msipende hizo ni dalili ya CCM kufell mwaka huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…