Kinga ya Rais iendelee kuwepo?

Kinga ya Raisi iendelee kuwepo?

  • Ndio

    Votes: 1 9.1%
  • Hapana

    Votes: 10 90.9%
  • Sijui

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    11
  • Poll closed .

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,673
149,858
Nina hakika moja ya tatizo kubwa la nchi yetu ni uwepo wa kile kinachoitwa kinga ya Raisi katika katiba yetu na inasikitisha zaidi watanzania ni kama tumeridhika na uwepo wa kinga hii kwani si wasomi,wanaharakati na hata wanasiasa wanaoonekana kutilia mkazo kinga hii iondolewe.

Ni bahati mbaya pia hata katika katiba inayopendekezwa kinga hii bado ipo.

Je,ni kweli hatujaona madhara ya hii kinga mpaka sasa?

Je,iendelee kuwepo?

Tafadhali piga kura yako hapo juu.

Harakati zinaweza kuanzia mitandaoni kwahiyo usipoteza fursa hii.
 
Iondolewe kwani inatumika vibaya.mfano:
1. Kukiuka miiko ya uongozi(kufanya biashara ikulu- Mkapa)
2.Kusamehe wezi bila kutiwa hatiani n.a. mahakama( Kikwete n.a. wezi wa EPA)
3.Kujimilikisha mali ya umma(mgodi) Mkapa).
 
Cha kusikitisha hatutumii nguvu kuipinga bali tunatumia nguvu nyingi kupinga matokeo ya hii kinga.

Watanzania ni kama tumelogwa!
 
Kinga ya rais itatoka tu pale watakapopatikana watu wa kunadili katiba, JPM mwenyewe ataibadili, upinzani mmeshindwa kujenga hoja za katiba mko bize na vijimatukio vinavyopulizwa na upepo ndani ya wiki.
 
Tume ya Jaji Warioba ilipopita kukusanya maoni suala hili lilikuwa mojawapo kati ya maoni mengi yaliyotolewa na wananchi kuwa yaingizwe kwenye Katiba Mpya.
Mengine ni kama haya:
1. Kinga ya Rais iondolewe baada ya muda wake wa uongozi
2. Matokeo ya uchaguzi wa Rais yaweze kupingwa mahakamani
3. Rais apunguziwe madaraka
4. Wakuu wa Mikoa wapewe nafasi hizo kwa profeshen maalum. Kigezo cha kuwa kada wa chama kiondolewe
4. Pawepo na Tume huru ya Uchaguzi
5. mamlaka ya Serikali ya Tanganyika irejeshwe.
6. Wabunge wasiowajibika ipasavyo katika majimbo yao waweze kuondolewa na wananchi waliowachagua
7. Kiongozi awe na elimu ya kutosha
N.k

Kwa hiyo suala zima hapa ni kuendeleza mchakato wa kupata Katiba Mpya kuanzia pale kwenye Rasimu ya Pili wala sio kuangalia Katiba feki inayopendekezwa ambayo ilipuuza maoni yote yaliyotolewa na wananchi
 
Iondolewe kwani inatumika vibaya.mfano:
1. Kukiuka miiko ya uongozi(kufanya biashara ikulu- Mkapa)
2.Kusamehe wezi bila kutiwa hatiani n.a. mahakama( Kikwete n.a. wezi wa EPA)
3.Kujimilikisha mali ya umma(mgodi) Mkapa).

Ongezea na Kulinda Majangili, wezi,na matumizi mabaya ya madaraka.
 
Kinga ya rais itatoka tu pale watakapopatikana watu wa kunadili katiba, JPM mwenyewe ataibadili, upinzani mmeshindwa kujenga hoja za katiba mko bize na vijimatukio vinavyopulizwa na upepo ndani ya wiki.
Hii ya sasa anaiheshimu?
 
Iachwe tu.... inasaidia saana katika swala la itifaki... pia hudumisha nidhamu ya kiutawala na kiutendaji....

Utambuzi wa mamlaka.... na uimara wa serikali....

Sio kila kitu ni cha kudiskas katika taifa... vingine ni vya kuamuliwa tu na kikundi cha watu au mtu mmoja....
 
Back
Top Bottom