Nilipoanza kusoma posts za Malaria Sugu na wengine wanao post kama yeye, nilishangaa kuwa je hawa watu hawaoni kweli hali ya nchi yetu na kule tunakoelekea? Je hawa watu wanaishi dunia ya wapi? Baadae nikatambua kuwa hawa wana lao jambo...wametumwa kuchanganya na kuvuruga mawazo ya jamii. Hata hivyo nimebaini kuwa hoja zao hazina ushawishi wala uzito wowote. Zimekuwa kama sahani ya santuri inayojirudia rudia. Hapo ndipo nikabaini udhaifu wao. Huwezi kukataa hoja kwamba nyumba yetu imejaa vinyesi, basi tuisafishe. Atakayekuja na kupinga hoja hiyo, ana walakini au ana lake jambo. Wale wanaokubaliana kuwa tusafushe nyumba yetu tuachane na vinyesi na harufu mbaya, tuwatose hawa ambao wanapinga kufanya hivyo. Hoja zao kila siku zinafichua udhaifu wa kile wanachokitetea na kuongezea nguvu wanaopenda mabadiliko. Acheni waandike tu.