Ustaarabu ni nini mkuu? Na kwa kigezo cha nani?Tusibeze hizi ndizo tamaduni zetu.....ila hazina hustarabh kabisa
Ustaarabu wa jamii ni mjadala mpana sana. Ustaarabu wa jamii moja unahusisha desturi zenye kuakisi maadili yenye uungwana pasipo kupendelea au kukiuka haki, sheria, kanuni na taratibu za jamii husika.Ustaarabu ni nini mkuu? Na kwa kigezo cha nani?
Asante mkuu. Maelezo ya ki Great thinker kabisa. Japo ni hivi bado kuna ule ukoloni wa kitamaduni ambapo, kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kihistoria na kiuchumi, utamaduni mmoja huchukuliwa kuwa ni bora kuliko mwingine. Ndiyo maana leo hii karibu kila kitu cha mzungu kinaigwa karibu na kila mtu duniani kwa sababu huchukuliwa eti ndiyo ustaarabu unaokubalika. Ziangalie dhana za urembo wa mwanamke, demokrasia na sasa tunatamadunishwa kukubali ushoga na usagaji kwa sababu ndiyo ustaarabu kisa tu mzungu mwenye ustaarabu wa juu karidhia.Ustaarabu wa jamii ni mjadala mpana sana. Ustaarabu wa jamii moja unahusisha desturi zenye kuakisi maadili yenye uungwana pasipo kupendelea au kukiuka haki, sheria, kanuni na taratibu za jamii husika.
Kimsingi hakuna kigezo cha kimataifa au kitaifa kinacho shadidisha kwamba jamii moja imestaarabika kuliko nyingine. Jambo kuu linaloshadidisha ustaarabu ni jinsi jamii inavyozingatia maadili yanachukuliwa kama uungwana na ustaarabu wa kufuata mambo mema yaliyokubalika katika jamii na wakati mwingine huchukuliwa kama elimu ya kufahamu mema na mabaya.
Na hapa tuwe waangalifu sana mema ya jamii moja yanaweza kuakisi mabaya ya jamii nyingine. Au mabaya ya jamii moja yaweza kuwa mazuri ya jamii nyingine.
Jamaa anaoa kila mwaka. Anawamudu kweli?Tusibeze hizi ndizo tamaduni zetu.....ila hazina hustarabh kabisa
Ukimwi unawavuruga vibaya huko ndio maana mfalme anatafuta bikra
Asante mkuu. Maelezo ya ki Great thinker kabisa. Japo ni hivi bado kuna ule ukoloni wa kitamaduni ambapo, kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kihistoria na kiuchumi, utamaduni mmoja huchukuliwa kuwa ni bora kuliko mwingine. Ndiyo maana leo hii karibu kila kitu cha mzungu kinaigwa karibu na kila mtu duniani kwa sababu huchukuliwa eti ndiyo ustaarabu unaokubalika. Ziangalie dhana za urembo wa mwanamke, demokrasia na sasa tunatamadunishwa kukubali ushoga na usagaji kwa sababu ndiyo ustaarabu kisa tu mzungu mwenye ustaarabu wa juu karidhia.
Mabinti hawa kwa Mswati kwa wazungu wanaakisi ustaarabu wa kinyama kwa sababu kwa mzungu matiti ya mwanamke ni matakatifu mno. Wangekuwa wanaachia matako na kuziba matiti bila shaka kungekuwa hakuna makelele ya kulalamika na kuita ustaarabu wa kijinga na udhalilishaji wa mwanamke. Kwa nini mabinti wakondefu waliovalia vibikini na kulazimishwa kupita mbele ya umati wa watu huku wameanika vitako vyao vilivyosinyaa katika mashindano ya urembo wachukuliwe sawa lakini hawa wanaocheza kwa furaha na mimea yao mikononi wakiwa na furaha ya dhati waonekane hawana ustaarabu? Kwa vile wameachia matiti nje?