Kindumbwendumbwe cha Muungano

Kindumbwendumbwe cha Muungano

albuluushiy

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2013
Posts
1,404
Reaction score
687
SHEREHE za kuadhimisha nusu karne ya Muungano
wa Tanzania zilizofikia kilele leo Jumamosi , Aprili
26, zinaghubikwa na utata kuhusu Muungano
wenyewe. Utata huo umezushwa na maswali kadhaa
ya kimsingi.
Kubwa kati ya hayo ni iwapo Muungano huo
ulioziunganisha Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri
ya Watu wa Zanzibar una uhalali wa kisheria.
Jamhuri hizo zilikuwa huru na kila moja ilikuwa na
kiti chake Umoja wa Mataifa.
Kadhalika, jamhuri hizo zilikuwa na mabaraza yao ya
kutunga sheria — Bunge kwa upande wa Tanganyika
na Baraza la Mapinduzi kwa Zanzibar. Kwa kawaida
— na ilivyo kwa mujibu wa sheria za kimataifa —
vyombo vya kutunga sheria vina umuhimu mkubwa
katika mchakato wa kuziunganisha nchi.
Aghalabu kazi ya mabunge ya kuidhinisha miungano
ya nchi hutanguliwa na hatua ya kuwashirikisha
wananchi kwa kuwauliza iwapo wanataka nchi zao
ziungane. Hilo halikutendeka Tanganyika wala
Zanzibar.
Wengi wanaamini kwamba Muungano wa Tanzania
hauna uhalali wa kisheria kwa sababu Hati ya
Muungano haikuidhinishwa na Baraza la Mapinduzi
la Zanzibar licha ya Bunge la Tanganyika kufanya
hivyo.
Swali jingine linalosababisha utata wa Muungano ni:
serikali ya Tanganyika iko wapi? Hivi ni kweli
imetoweka? Wengi wanaamini kwamba si kweli;
serikali ya Tanganyika ipo lakini imejificha. Hakika ya
mambo ni kwamba serikali ya Tanzania ndiyo
serikali ya Tanganyika.
Inafaa pia kuuliza: ni nini kilichomsababisha muasisi
mkuu wa Muungano, Mwalimu Julius Nyerere,
amhimize mwenziwe Sheikh Abeid Amani Karume,
Rais wa kwanza wa Zanzibar, aikubali rai ya
kuziunganisha nchi zao?
Nakwa nini Nyerere alifanya papara ya kutayarisha
Hati ya Muungano, tena kwa siri kubwa?
Majibu ya maswali hayo na mengine yenye kuhusika
na Muungano wa Tanzania yamo kwenye nakala za
nyaraka zilizo katika Maktaba ya Lyndon Baines
Johnson huko Texas, Marekani. Nakala hizo ni za
mawasiliano baina ya wizara ya mambo ya nje ya
Marekani, mawaziri wa wizara hiyo, mabalozi,
wanabalozi na majasusi wa Kimarekani waliokuwako
Afrika Mashariki, London na Washington.
Mmoja wa majasusi hao ni Frank Carlucci ambaye
1964 alikuwa balozi mdogo wa Marekani, Zanzibar.
Carlucci baadaye alikuwa mkurugenzi wa Shirika la
Ujasusi la Marekani (CIA) na waziri wa ulinzi chini
ya Rais Ronald Reagan.
Wamarekani wengine walioandika barua au
waliopeleka ujumbe wa maandishi ya simu (cables)
walikuwa Dean Rusk aliyekuwa waziri wa mambo ya
nje, George Ball (waziri mdogo wa mambo ya nje),
Averell Harriman (waziri mwingine mdogo wa
mambo ya nje), William Leonhart(Balozi wa
Marekani nchini Tanganyika), William Attwood,
(Balozi wa Marekani huko Kenya) na McGeorge
Bundy, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Rais
Lyndon Johnson.
Yalipozuka Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, 1964
serikali ya Johnson ilikuwa hamkani. Haikusahau
jinsi akina Fidel Castro, nduguye Raul, Camilo
Cienfuegos na Che Guevara walivyompindua dikteta
wa Cuba Fulgencio Batista na kuingia Havana Januari
Mosi 1959.
Kilichozidi kuifadhaisha Marekani yalikuwa
mahusiano yaliyochanua baina ya Cuba na
Muungano wa Jamhuri za Kisoshalisti za Kisovieti
uliokuwa hasimu mkubwa wa Marekani katika zama
hizo za vita baridi. Marekani ilishtuka kuiona nchi
jirani ikikumbatiana na Wakomunisti. Cuba ya
kimapinduzi ikawa mwiba katika koo la Marekani.
Marekani ilizidi kushtuka miaka mitano baadaye
watawala wapya wa Zanzibar walipokuwa na
mahusiano mema na madola ya Kikomunisti, hasa
Urusi, China na Ujerumani ya Mashariki (GDR).
Zanzibar ya kimapinduzi nayo ikawa mwiba
mwingine ulioichoma Marekani.
Kwa hakika Wamarekani waliingiwa na kiwewe kwau
habari za uongo za kuwepo Wacuba Zanzibar. Kwa
mfano, gazeti la New York Times la Januari 15,
liliripoti kwenye ukurasa wake wa mbele kwamba
Wamarekani waliokimbia Zanzibar walisema
waliwaona wanajeshi waliokuwa wakizungumza
Kihispania na waliovaa sare ya Cuba. Kumbe
walikuwa vijana wa Umma Party waliofunzwa kijeshi
Cuba.
Siku nne baadaye gazeti hilo likaonya kwamba
“Zanzibar inakaribia kuwa Cuba ya Afrika” na
likaeleza namna Cuba ilivyojiandaa kuchochea
mapinduzi kwingineko Afrika.
Shirika la CIA nalo lilizidisha hofu kwa ripoti zake
zilizotiwa chumvi za Wacuba kushiriki katika
Mapinduzi ya Zanzibar.
Marekani ilizidi kuingiwa na wahka baada ya jeshi la
Tanganyika kuasi Januari 20. Siku chache baadaye
majeshi ya Kenya na Uganda nayo yaliiga. Serikali za
nchi zote hizo tatu ziliomba msaada wa kijeshi
kutoka Uingereza.
Wakuu wa Marekani pamoja na Rais Johnson
mwenyewe waliishikilia Uingereza ipeleke majeshi
Zanzibar kuwang’oa waliodhaniwa kuwa ni
Wakomunisti waliomzunguka Karume.
Wamarekani waliwataja Abdulrahman Babu, Waziri
wa Mambo ya Nje, Waziri Mkuu Abdallah Kassim
Hanga, Waziri Hassan Nassor Moyo na Salim
Rashid, Katibu wa Baraza la Mapinduzi. Uingereza
ilikataa kuchukua hatua ya kijeshi Zanzibar.
Wamarekani wakaudhika.
“Waingereza hawalishughulikii tatizo hili,” Bundy,
Mshauri wa Usalama wa Taifa, alimlalamikia Rais
Johnson mwanzoni mwa Februari.
Wamarekani hawakujuwa kwamba Uingereza ilikuwa
na mkakati mwingine. Ikitaka kushirikiana na
Nyerere na Karume ili kuwashinda nguvu hao
waliokuwa wakidhaniwa kuwa Wakomunisti.
Wamarekani wakaanza kuwatia hofu viongozi wa
Afrika ya Mashariki kwamba wakilala kanda yao
nzima itatekwa na Wakomunisti.
Machi 6 Rusk, waziri wa mambo ya nje, aliwaandikia
mabalozi wa Marekani Nairobi na Dar es Salaam
akiwaamrisha wawasiliane haraka na Nyerere, Rais
Jomo Kenyatta wa Kenya na Rais Milton Obote wa
Uganda na wawaeleze jinsi Karume anavyofanya
hatari kwa kumtegemea Babu.
Rusk aliwashauri mabalozi wawaombe marais hao
wamsemeshe Karume afahamu hatari ya Babu kwa
madaraka yake Karume na kwa usalama wa
Zanzibar na wa Afrika ya Mashariki.
Rusk aliwauliza hao mabalozi “iwapo itasaidia
kumtajia tena Nyerere rai ya kuunda shirikisho la
Tanganyika na Zanzibar kwa dhamiri ya kuimarisha
madaraka ya Karume na kuupunguza ushawishi wa
Babu.”
Marekani ilijiandaa pia kuivamia kijeshi Zanzibar lau
rai ya kuunda shirikisho hilo ingeshindikana. Iliuita
mpango huo Zanzibar Action Plan (ZAP).
Carlucci akiwa Zanzibar alikuwa na mipango yake
miwili ya kimaluuni. Kwanza alikuwa mbioni
kuwafitinisha viongozi wa Afro-Shirazi Party na wa
Umma Party. Na Machi 30 aliiandikia wizara ya nje
Washington akishauri kwamba Marekani imhonge
Karume ndege ya aina ya “helikopta ikiwa na rubani
wa Kimarekani.”
Armando Estrada wa Idara ya Ujasusi ya Cuba –
Dirección General De Inteligencia (DGI)–
anawakumbuka Wazanzibari waliokuwa Cuba
wakifunzwa mbinu za kupindua lakini mawasiliano
nao yalikatika waliporudi kwao. Wakati huo Cuba
haikuwa na ubalozi Zanzibar.
Katika Afrika ya Mashariki nzima Cuba ilikuwa na
ubalozi Tanganyika tu, na ilikuwa na wanabalozi
wachache. Juu ya hayo, ilizidi kuvuma kwamba
kulikuwa Wacuba walioshiriki katika Mapinduzi ya
Zanzibar.
Magazeti ya nchi za Magharibi yakiandika kuwa
Wacuba walionekana, waliokuwa wamefuga madevu
kama Castro na wakizungumza Kihispania. Walizitaja
kauli mbiu zao, matamshi kama
“Venceremos!” (Tutashinda).
Uvumi huo uliwababaisha hata viongozi wa
Cuba.Wakijuwa kwamba hawakuwako Wacuba
Zanzibar lakini wakidhania kwamba labda kweli
Cuba iliwafunza wapinduzi wa huko.
Siku chache baada ya Mapinduzi ya Zanzibar Jorge
Serguera Balozi wa Cuba nchini Algeria alifunga
safari kwenda Zanzibar kuitathmini hali ya mambo.
Kutoka huko akafululiza kwenda Moscow kumuarifu
Castro aliyekuwa ziarani kutoka Januari 13 hadi
Januari 23.
Serguera anakumbuka kwamba Castro alimuuliza
ikiwa kweli wanamapinduzi wa Zanzibar
wakizungumza Kihispania.
Serguera alimjibu: “Ni kweli, Fidel.”
Castro akaendelea kumuuliza: “Ni kweli wanasema
Patria o Muerte (Nchi yangu au kifo) Venceremos!
(Tutashinda)?”
Serguera akamjibu: “Ni kweli, Fidel.”
Castro asitosheke, akaendelea kumuuliza:
“Ni kweli sisi ndio tuliowapa mafunzo (ya
kupindua)?” Naye Serguera akamjibu: “Ni kweli,
Fidel.”
Januari 15 Cuba iliitambua Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar lakini haikufungua ubalozi huko. Hatimaye
mwishoni mwa Januari Marekani ilikiri kwamba
Cuba haikushiriki katika Mapinduzi ya Zanzibar.
Lakini Wamarekani hawakukoma.Wakaanza
kuwaangaza Warusi, Wachina na Wajerumani wa
Mashariki na misaada waliokuwa wanaipa Zanzibar.
Wamarekani walikuwa kama waliingiwa na kichaa.
Carlucci akiwa Zanzibar alipeleka ujumbe wizara ya
mambo ya nje Washington ukisema: “Zanzibar
karibu itakuwa dola ya Kikomunisti…”
Thomas Hughes, mkurugenzi wa Ofisi ya Ujasusi na
Uchunguzi (Bureau of Intelligence and Research –
INR-) iliyo katika wizara wa mambo ya nje, alikuwa
akipenda kuikariri indhari ya Carlucci. Safari moja
aliandika: “…Katika muda wa miezi sita Zanzibar
inaweza kuwa taifa la kwanza la Kiafrika
kufungamana na Ukomunisti.”
Siku mbili baada ya hapo Waingereza waliiarifu
Marekani kwamba Nyerere ameweza kumshawishi
Karume waziunganishe nchi zao katika shirikisho.
Waingereza waliieleza Marekani kwamba kwa
kuikumbatia Zanzibar “Tanganyika itaweza kuuzima
moto wa kimapinduzi wa Zanzibar na kuyafunika
majivu yake.”
Siku ya pili George Ball, waziri mdogo wa mambo ya
nje wa Marekani, aliuandikia Ubalozi wajv Marekani
Dar es Salaam akisema: “Wizara (ya mambo ya nje
ya Marekani) iko tayari kuibariki na kuiunga mkono
juhudi ya Tanganyika…hii…inaonyesha kuwa njia
bora na yumkini ni uwezekano wa pekee wa
kuibadili hali ya sasa ya Zanzibar inayotatanisha.”
Aprili 22, 1964 Nyerere na Karume walitia saini Hati
ya Muungano. Kwa mujibu wa Carlucci, “Karume
akifikiria kwamba anaridhia shirikisho la nchi mbili
zilizo huru.” Siku nne baadaye ikazaliwa Jamhuri ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Tanzania ya
leo.
 
Imetia huruma sana, nadhani sasa ni dhahiri hakuna cha kuonyesha kwenye Muungano, Nilitegemea watuonyeshe yale mambo ambayo yameanzishwa na kusimamiwa na Muungano. Kilichoonyeshwa ni mambo ya kijeshi. Enzi za Mwalimu zana za kivita ni mambo ya siri yetu, lakini kwa utawala wa leo ni mambo ya kuwekwa hadharani.

Naamini kwamba kama CCM itaendelea kuwa madarakani hali itakuwa tete,
Nilitegemea wawambie walimwengu kuhusu mambo yaliyoanzishwa wakati wa Muungano, ambayo ni kielelezo cha wazi kwa umuhimu wa Muungano. Nadhani ilikuwa kutaka kujionyesha kwa majirani....
 
Imetia huruma sana, nadhani sasa ni dhahiri hakuna cha kuonyesha kwenye Muungano, Nilitegemea watuonyeshe yale mambo ambayo yameanzishwa na kusimamiwa na Muungano. Kilichoonyeshwa ni mambo ya kijeshi. Enzi za Mwalimu zana za kivita ni mambo ya siri yetu, lakini kwa utawala wa leo ni mambo ya kuwekwa hadharani.

Naamini kwamba kama CCM itaendelea kuwa madarakani hali itakuwa tete,
Nilitegemea wawambie walimwengu kuhusu mambo yaliyoanzishwa wakati wa Muungano, ambayo ni kielelezo cha wazi kwa umuhimu wa Muungano. Nadhani ilikuwa kutaka kujionyesha kwa majirani....

Sidhani hata kama ungeoneshwa hayo mambo ungekubali kwa akili zako zilivo negative!

Ila moja zao la miaka hamsini ya muungano ni UWEPO WA VYOMBO KAMA JAMII FORUM NA UHURU WA KUTUKANA!

nakutakieni week end njema kama si sherehe njema za tz at 50.
 
Ukweli hasa kuhusu muungano we2 wengi hawaujui
 
Back
Top Bottom