Kinda Like This Raza Guy... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kinda Like This Raza Guy...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gustanza_The, Dec 10, 2008.

 1. G

  Gustanza_The Senior Member

  #1
  Dec 10, 2008
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  *[Sorry if this has been posted already]*

  I'm not confused about how I feel about this Masha guy--I think he is terribly misguided lunatic. But that's not what bothers me. The thing that bothers me the most, is the fact that sor far haya majingamajinga ya CCM yamefunga midomo yao na wala hayajajitokeza kukemea upuzi uliocheuliwa na huyu son of a gun... Anyway, I'm glad Raza amepata courage ya ku-join battle!

  ___________________________________________________________________________________

  Raza ajitosa mvutano wa Mengi, Masha

  2008-12-10 16:07:15
  Na Mwandishi Wetu


  Mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar, Mohamed Raza, amejitosa katika mvutano uliopamba moto nchini sasa wa njama za kuhujumiwa kwa mfanyabiashara Reginald Mengi, kwa kusema kwamba anaungana naye katika harakati zake za kupambana na ufisadi.

  Raza akizungumza na Nipashe kwa simu kutoka Zanzibar jana asubuhi, alisema ameamua kuzungumzia suala hilo kama salamu zake kwa siku ya Uhuru wa Tanganyika, kwamba anaungana na Mengi katika kuendeleza mapambano dhidi ya mafisadi kwa sababu Rais Jakaya Kikwete mwenyewe ameonyesha nia ya dhati kabisa kutokomeza ufisadi nchini.

  Alimtakia kila la kheri Mengi na kumhakikishia kwamba Watanzania wapo nyuma yake.

  Alisema Mengi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, ikiwamo ya The Guardian Limited linalochapisha gazeti hili, atalindwa na Mungu kwa sababu anasimamia katika ukweli.

  ``Kila mmoja anakwenda kanisani au msikitini kumuomba Mungu, na ndiye atamlinda Mengi,`` alisema na kuongeza:

  ``Ufisadi umeharibu nchi. Maana ya Uhuru wa Tanganyika kama ilivyokuwa kwa Mapinduzi ya Zanzibar ni kuwapatia watu wao heshima; huduma bora za maji, umeme, barabara na afya.

  �Kuna wananchi vijijini hawana maji, hawana umeme, hawana barabara, lakini wapo matajiri waliojilimbikizia mabilioni ya shilingi kwa njia ya kifisadi. Hawa hawawezi kuachwa tu kwani uhuru hautakuwa na maana kwa wananchi.``

  Alisisitiza kwamba kama ambavyo watu wengi wametoa kilio chao juu ya kampuni ya Kagoda Agriculture Limited ambayo imetajwa kujinufaisha na fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ni vema wahusika wake wawekwe wazi. �Kagoda iwekwe wazi,`` alisema.

  Raza ambaye wakati wa utawala wa Rais wa Zanzibar, Dk. Salimin Amour, alikuwa mshauri wake wa masuala ya Michezo, alisema kwamba akiwa ni mwanachama mwaminifu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anaamini kwamba nchi haiongozwi na kundi la watu.

  ``Kundi haliongozi nchi, wala halitaongoza. Ni vizuri wazee wakae na kutafakari kwamba wakati tunasherehekea uhuru wa Tanganyika nchi inakwenda wapi?`` alisema na kusisitiza:

  ``Matajiri hawawezi kuwa wakuu kwa kila jambo. Leo ukitaka uongozi iwe ni udiwani au ubunge ni lazima utembee na mfuko wa Rambo uliojaa fedha ndipo upate uongozi. Sasa hii ndiyo misingi aliotuachia Mwalimu Nyerere?``

  Aliwaomba wananchi kwa ujumla wao wamuunge mkono Rais Kikwete kwa sababu anapigania maslahi ya nchi, na kusema suala la kuweka ubinafsi mbele kuliko nchi ndilo linaangamiza taifa.

  Alisema: ``Katika nchi hakuna urafiki.``
  Raza alisema kwamba kuna matatizo ya makundi Tanzania, na akaonya haya yasipodhibitiwa ndiyo yataharibu nchi, alitumia usemi �kikulacho ki nguoni mwako.`

  Tangu Mengi atamke hadharani kwamba wapo watu wanatishia maisha yake kutokana na vyombo vya habari anavyomiliki kuwa mstari wa mbele kupambana na ufisadi, pia kufichua njama za Waziri mmoja kijana kutaka abambikiziwe kodi kubwa ili ashindwe kulipa hivyo afilisiwe, Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, amejitokeza katika kile kinachoonekana kuhusika katika kadhia hiyo.

  Mengi alisema kwamba njama za kutaka abambikiziwe kodi kubwa zilikuwa zinasukuwa na waziri mmoja kijana, hata hivyo hakumtaja jina.

  Siku moja baadaye Masha alijitokeza hadharani na kumpa Mengi siku saba kuwasilisha ushahidi kwake juu ya njama za kutaka kubambikiziwa kodi, vinginevyo angekumbana na nguvu za sheria.

  Hata hivyo, baada ya kuibuka shinikizo kubwa kutoka kwa umma juu ya njama hizo, Masha alibadili kauli kwa kusema kwamba nia ya kumtaka Mengi atoe ushahidi ililengwa kumlinda dhidi ya njama hizo mbaya na si kumtisha.

  Hadi sasa watu mbalimbali na vikundi vya kijamii wametoa kauli zao wakimpinga Masha, wengine wakieleza wazi kwamba kitendo chake cha kujitokeza hadharani kumjibu Mengi ni kielelezo kwamba anahusika na tuhuma za kusuka mpango wa kumbambikizia kodi ili kumfilisi hivyo kumnyamazisha kabisa katika vita yake dhidi ya ufisadi.

  SOURCE: Nipashe
  ___________________________________________________________________________________
   
 2. S

  Sabri-bachani Member

  #2
  Dec 10, 2008
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 96
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Khaa porojo za Raza tena. Celebrity anayelilia publicity. Yeye si anao mfuko? lini amewahi kupata Uongozi? (wa kupigiwa kura na wajumbe).
   
 3. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35


  Huyu naye Raza yuko too cryptic! Haeleweki kabisa.
   
 4. G

  Gustanza_The Senior Member

  #4
  Dec 10, 2008
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  He's not a coward at least...
   
 5. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2008
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mmesahau alovyo iuzia SMZ mabenz mabovu kwajili ya Rais wa ZNZ.. Gari ya rais ikapata breakdown within a month of procurement.. The prices of the vehicles were astronomical as expected... Ikawa scandal. Huyu fisadi tuu hana lolote anataka kujisafisha by acting all righteous.. na wadanganyika kama kawa tunamkubali... hahaha.
   
 6. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu hii lugha haijakaa sawa, mimi ni mwanachama hai wa CCM lakini sifanani na hiyo lugha yako hapo juu,

  kumbuka Marmba na Yona wamelazwa rumande na serikali ya CCM na hakuna aliye juu ya sheria sasa hivi ndani ya CCM, mafisadi wote wako njiani kwenda kwenye sheria.

  Ahsante!
   
 7. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Huyu Raza naye fisadi tu, si naye anadaiwa alikuwa anasimamia mishahara ya watumishi wa SMZ?
   
 8. G

  Gustanza_The Senior Member

  #8
  Dec 11, 2008
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Geez, this whole rumande thing is the biggest fairy tale I have ever seen! You can mark my words: it's only a matter of time before you see Mramba, Yona, and some other mafisadi guys unaodai kuwa wako njiani kwenda kwenye sheria wakipeta mitaani freely. This rumande thing was simply a mediocre prank... I'm not convinced yet!
   
Loading...