Kinara wa ufaulu Chuo Kikuu Dar es Salaam 2010

Hongera Salome ila usiishie hapo kama unanisikia, ninyi ndio wanasayansi wetu, sasa fanyeni mgundue vitu vipya badala tu ya kutumia au kujifunza vilivyogunduliwa na wazungu. BIGUP
 
mie naona kama kozi zote tu ni ngumu
Computer science ni kati ya kozi rahisi sana kwani vitu vipo direct haviitaji uchambuzi sana wala ulinganifu kama masomo mengine mfano uchumi, sheria etc. Tatizo ni lile lile watanzania kuogopa Science. Pili ukiweza kusolve past papers (MADESA) za miaka 5 na kwa mfumo wetu wa semester lazima mitihani hutoka humo humo jinsi ilivyo. Hata hivyo kwa perfomance yake anastahili pongezi.
 
Ni kweli masomo yote ni magumu hakuna kozi rahisi lakini kwa mwanamke kufaulu kiasi hicho anastahili pongezi maana mabinti wanakutana na vishawishi vingi sana.
 
kozi ya computer si sawa na education kabisaaa
Halafu kozi ya kompyuta sio sawa na Education wala fine arts ambayo niliisoma mimi.Yeye ni kinara wa kozi ya kompyuta na siyo vinginevyo. Lakini nampongeza kwa kufanya vizuri masomo yake. Tutegemee kuona anaongeza thamani na siyo kutuionyesha jinsi madesa yalivyo ya muhimu.
 
Kama ni rahisi mbona sioni watu 1000 wakitoka na 4.7/5.0???
Mpeni hongera huyu mdada bila mikingamo.

Uchumi ni course ngumu au watu hawana refence? Vitabu??
Sheria nayo ni course ngumu??

Kiswahili Je??
Siasa??
Tamthiria??( Hii muulizeni Edward Lowassa atawaambia ni ngumu sana)

Hakuna somo gumu duniani inategemea tu wewe ni kilaza kwa kiwango gani.

Computer science ni kati ya kozi rahisi sana kwani vitu vipo direct haviitaji uchambuzi sana wala ulinganifu kama masomo mengine mfano uchumi, sheria etc. Tatizo ni lile lile watanzania kuogopa Science. Pili ukiweza kusolve past papers (MADESA) za miaka 5 na kwa mfumo wetu wa semester lazima mitihani hutoka humo humo jinsi ilivyo. Hata hivyo kwa perfomance yake anastahili pongezi.
 
Sina hakika na chanzo cha habari yako, mimi ni moja ya wahitimu wa mwaka huu na aliyetangazwa mwanafunzi bora kwa maana ya GPA ni MARTIN CHEGELE. Huyu alikuwa Tanzania One form4 na mwaka 2007 alikuwa Tanzania one form 6. Labda kama huyo dada aliongoza kwa kozi yake na si chuo kizima mkuu.

Hata mm nakumbuka hivyo Chegele ndio alieongoza mwaka wetu.
 
hongera binti uitumie elimu yako kwa ustawi wa jamii ya watanzania.tunawategemea
 
Hongera sana salome, MMungu akuongezee zaid na mwenye manufaa kwa familia yako na waTZ
 
Back
Top Bottom