Kinana: Serikali iwasikilize wananchi wa Mtwara

Kinana: Serikali iwasikilize wananchi wa Mtwara

huyu jamaa asiturubuni meli zake na maliasilisi zetu limeishia wapi? serengenti tunamsubiria wanatukataza kula vimulu wenyenye wanagawana maliasili zetu.
 
Hivi kwenye vikao vyenu CCM huwa mnazungumza nini?kama siyo umbeya kwaninini viongozi wenu wanalalamika kama wapinzani wakati nyie ndiyo wenye serikali?Pooor CCM
Huwa Wanafikiri na Kupanga namna ya Kuithibiti Chadema!
Hawana kazi nyingine zaidi ya hiyo ya Majungu dhidi ya Dk Slaa! Sasa safari hii wameshikwa pabaya wamekosa pa kutokea inabidi tu,wakubali kusalimu Amri!

Walizoea kusema ni CDM inawachochea wananchi, sasa ktk hili la Gesi wameshindwa kuwahusisha Chadema moja kwa moja!

Kinana na Nape kutowa matamko kwamba madai ya wanamtwara ni ya Msingi na Kwamba Serikili ikae nao kuwasikiliza,! Nikitu kilitegemewa.

Haiwezekani Waziri Mzima na Mkuu wa Mkowa kutowa Matusi, Kejeli na Vitisho kwa Wanakusini,na watu wakaonyesha Msimamo wao, kwa kutoogopa wala Kutotii na Wakaandamana, halafu Kina Nape wasitafute namna ya kuwapooza!

Subiri tu siku moja utasikia, Tamko walilo towa Waziri Muhongo na Mkuu wa Mkoa Simba Kalia, halikuwa tamko la Chama wala Serikali!!

Hakika Safari hii Watu watatapika 10% walizo chukuwa kwenye Kampuni iliyopewa zabuni ya Ujenzi wa Bomba la Kusafirishia Gesi!

Ni bora hayo Mabomba yatumike Kwa Maji. Umeme uzalishwe ndio usafirishwe.

Tunamsubiri, MWIGULU MZINZI na MZEE wa MWITUNI WASSIRA, tusikie Matamshi yao, wasiwe kila mara ni Chadema.,chadema,! Hata kwa mambo ya Msingi, wao Wataropoka tu!

MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!
MUNGU IBARIKI CHADEMA!!!
 
unafiki huu wa nyinyiemi ni mbaya sana na ndio uliotufikisha hapa tulipo, kinana na hiyo nyinyiemi yake walikuwa wapi ? nikisema waliiga matamshi ya viongozi wetu wa kitaifa CHADEMA nitakuwa nimewaonea? au tuwaeleweje akina kinana , ina maana ccm na serikali yake haina maamuzi ila inafuata upepo? hii ni hatari kwa taifa letu na rasilimali zake !!!!!!!!!!!!!
 
Umeona WABUNGE wao Wameanza kuchomewa MOTO NYUMBA zao... ndio KIAMA CHAO HICHOO
Good! nimefurahi sana, hao wabunge ni wabinafsi, wamesahau ni wananchi hao hao masikini ndio waliowachagua kuwawakilisha. Wabunge wanatetea maslahi ya serikali ya CCM na kuwasaliti wanamtwari. Light up, light up! burn everthing and Let them start over again
 
KITAIFA
Na Waandishi Wetu

Posted Jumatatu,Januari28 2013 saa 21:29 PM

KWA UFUPI

Wakati watendaji hao wa CCM wakitoa matamko hayo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana alifanya vikao mfululizo mkoani Mtwara akisaka suluhu ya mgogoro huo.






SAKATA la gesi sasa limeingia hatua mpya, baada ya watendaji wakuu wa CCM; Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kuitaka Serikali ikae na wana-Mtwara ili kuona namna ya kumaliza mgogoro huo kwa amani.


Kinana na Nape walitoa kauli hizo kwa nyakati tofauti jana. Wakati Kinana alisema hayo alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara mkoani Kigoma, Nape alifanya hivyo kupitia mtandaowa Twitter na baadaye kuthibitisha kauli hiyo alipoulizwa na mwandishi wetu.



Wakati watendaji hao wa CCM wakitoa matamko hayo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana alifanya vikao mfululizo mkoani Mtwara akisaka suluhu ya mgogoro huo.



Kinana na Nape
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Uvinza, Kigoma, Kinana aliitaka Serikali isikilize hoja za wakazi wa Mtwara na kuzitafutia usumbufu sahihi.



Mbali na kutoa ushauri huo, aliitaka pia Serikali kuwasaka watu wanaochochea mgogoro huo kwa kufanya vurugu na kuharibu mali za watu na kuwafikisha mbele ya sheria.
“Serikali ikae na wana-Mtwara na kuwasikiliza, wananchi hao wana hoja na Serikali inapaswa kutoa majibu sahihi kwa hoja hizo. Lakini pia iwasake na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha uvunjifu wa amani,” alisema Kinana.



Kwa upande wake, Nnauye aliitaka Serikali kuwasikiliza wananchi wa Mtwara kwa kuwa madai yao ni ya msingi... “Wakazi wa Mtwara na Lindi wanazo hoja za msingi juu ya suala la gesi, hoja ambazo ni muhimu kusikilizwa na kupatiwa majibu sahihi.”



Nape alisema hoja za wakazi hao ni za msingi lakini akaongeza kuwa kuna baadhi ya wahuni ambao wanatumia mwanya huo kupora na kuharibu mali za watu. “Kuna uhusiano gani kati ya hoja yao ya madai ya gesi na kuchoma nyumba za watu, kuharibu mali za umma na magari ya watu. Kuna kundi la wahuni ambalo Serikali inatakiwa kuhakikisha inapambana nalo na kuwachukulia hatua kali za kisheria,” alisema Nape.



Pinda asaka suluhu
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana alikuwa na kibarua kizito kusaka suluhu ya mgogoro wa gesi baada ya kuzungumza na makundi mbalimbali ya kijamii kupata mawazo yao.



Pinda aliyeongozana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja alianza kazi hiyo juzi kwa kufanya vikao vya ndani na viongozi wa Serikali mkoa wa Mtwara. Habari kutoka Mtwara zinaeleza kuwa kutwa nzima ya jana, Waziri Mkuu Pinda alikuwa akifanya mikutano mbalimbali na makundi kadhaa kwa lengo la kupata suluhu ya mgogoro huo wa gesi.



“Alianza kwa kufanya mazungumzo ya ndani na viongozi wa dini, wanaharakati, wanasiasa na baadaye viongozi wa Serikali za Mitaa,” kilieleza chanzo cha habari kutoka Mtwara.
Mbali na viongozi hao, Pinda pia alizungumza na wafanyabiashara, viongozi wa CCM na madiwani kabla ya mkutano wake na waandishi wa habari aliopanga kuufanya baadaye jioni.
Mmoja wa madiwani waliohudhuria mkutano huo wa Pinda alilieleza gazeti hili kuwa, Waziri Mkuu aliwaambia kuwa mkutano wake huo ni kwa ajili ya kukusanya maoni.



“Amesema amekuja kukusanya maoni na baadaye atakwenda kushauriana na Rais Jakaya Kikwete na atatoa tamko kuhusu hatima ya suala hilo baadaye,” alisema diwani huyo akimnukuu Waziri Mkuu Pinda.



Gesi kuteka Bunge
Mkutano wa Kumi wa Bunge unaanza leo mjini Dodoma, huku suala la gesi likitarajiwa kutawala mijadala mbalimbali ya wabunge.


Mbunge wa Mkanyageni (CUF), Habib Mnyaa ni miongoni mwa wabunge waliotangaza mapema kuwa watazungumzia suala hilo bungeni. Mnyaa alisema anakusudia kuwasilisha hoja binafsi za maombi ya wakazi wa Mtwara kupinga gesi kupelekwa Dar es Salaam.



Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Mawasiliano ya Bunge, Deogratius Igidio aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa shughuli zote zitakazofanyika ndani ya ukumbi huo zitajulikana leo baada ya Kikao cha Kamati ya Uongozi.Katika kipindi cha wiki nne sasa kumekuwa na maandamano, malumbano na vitendo vya ghasia kuhusiana na mradi wa kujenga bomba la kusafirishia gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam hatua ambayo inapingwa na wananchi wa eneo hilo ambao wanadai kuwa wamesahauliwa katika miradi ya maendeleo.



Wananchi hao wa Mtwara wanataka kusitishwa kwa mpango wa kusafirisha gesi hiyo kwa madai kuwa, eneo la Mtwara halijaendelezwa na mara zote Serikali haijaweka vipaumbele kwa ajili ya kusukuma mbele eneo hilo.



Wanataka uendelezwaji wa gesi hiyo ufanywe mkoani humo kwa madai kuwa utasaidia kuchochea shughuli za maendeleo na kuufanya uanze kuinuka kiuchumi.



Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa ambaye pia ni mwenyeji wa mkoa huo ametoa wito wa pande zote kukutana na kujadiliana ili kumaliza mvutano huo akisema ni jambo la kufedhehesha na kusikitisha kuona wananchi wakianzisha maandamano na kupinga mradi huo wa Serikali.



Chadema hakitaki
Chadema kimeitaka Serikali kusitisha mpango wa kusafirisha gesi iliyogunduliwa mkoani Mtwara kwenda Dar es Salaam mpaka itakapokutana na wananchi na kufikia maridhiano kwa pamoja.



Chama hicho pia kimeitaka Serikali iweke wazi mikataba yote 26 ya kampuni ilizoingia nayo kwa ajili ya kuchimba nishati hiyo ili wananchi waweze kuijua.



Mwenyekiti Freeman Mbowe alitoa wito huo jana alipokuwa akifungua mkutano wa siku moja wa Baraza Kuu la chama hicho, Dar es Salaam... “Kwa muda mrefu watu wamekuwa wakiuliza Chadema nini kauli yenu kuhusu mgogoro huo na kutaka kujua tuko na wananchi au Serikali? Chadema iko nyuma ya wananchi,” alisema Mbowe na kuongeza:



“Serikali iache kufanya kazi ikiwa Dar es Salaam iende kwa wananchi na kuzungumza nao na wakikubaliana kwa pamoja ndipo mradi huo utekelezwe.”
Habari hii imeandikwa na Raymond Kaminyoge, Kigoma; Ibrahim Yamola, Dar na Habel Chidawali na Ibrahim Bakari, Dodoma.




kinachotakiwa ni kuwaachia watu wote waliokamatwa kwenye vurugu za mtwara maana wao ndio wamesababisha serikali kusalim amri na kuongea na watu wa mtwara kuhusu gesi, kuwaita ni wahuni au wachochezi au kuwapa neno lolote baya nikuwaonea ,hivyo nawaomba wana mtwara tuwatetee kwa nguvu zote waachiwe bila masharti yeyote,ikibidi tufanye maandamano nchi nzima ili waachiliwe
 
2005 ccm ilitumia ubaguzi kwa kumdhalilisha waziri mkuu mstaafu,salim ahmed salim kwa kusema ni muarabu,ccm hiyo hiyo 2012 imemteua mwarabu mweusi(msomali)abdurahamani kinana.kinana ni mmoja wa wamiliki wa kampuni yenye tender ndani ya bomba la gesi mtwara dar,ccm chini ya kikwete imempa kazi kinana kuendeleza na kulinda wizi wa rasilimali ya nchi.serikali ya ccm chini ya kikwete inatumia polisi kukandamiza demokrasia kwa kuzuia mikutano mingi ya chadema kwa kisingizio cha kutokuwa na polisi wa kutosha.lakini wanaposisitiza kuwa wataendelea na mikutano yao idadi kubwa ya polisi inasambazwa kwa kuzuia mikutano yao.
Sasa litakalotokea tanzania ni umwagaji mwingi wa damu hadi kufikia 2015 sababu serikari chafu ya ccm haisikilizi wananchi bali inawalinda wachache wao wezi wa mali ya taifa letu,tumeona polisi wakiuwa raia kuanzia arusha,tabora,morogoro,mbeya ,songea na hakuna aliyechukuliwa hatua yeyote kwa mauwaji hayo.wananchi sasa wameanza kujibu mapigo kwa kuua askari,na kuna taafifa kuwa sasa ni jino kwa jino raia wakiuwawa na polisi mchana raia watauwa polisi usiku sasa amani iko wapi kama si ubaguzi uaolelewa na serikari ya ccm?
Mod ukiifuta hii habari nitakuwa nairidisha kila kukicha kwa watu mbalimbali mpaka ujumbe huu uenezwe kwa wapenda amani kote tanzania
 
Good! nimefurahi sana, hao wabunge ni wabinafsi, wamesahau ni wananchi hao hao masikini ndio waliowachagua kuwawakilisha. Wabunge wanatetea maslahi ya serikali ya CCM na kuwasaliti wanamtwari. Light up, light up! burn everthing and Let them start over again

Yeah, Kama Anna Abdallah alikuwa MBUNGE wa MASASI, MBUNGE wa VITI MAALUMU Mwenyekiti wa UWT na bado yuko BUNGENI MIAKA zaidi ya 30; Ukimuuliza ameifanyia nini MTWARA atasema alifanikiwa kupata MME - PIUS MSEKWA...
 
Back
Top Bottom