Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahiman Kinana amesisitiza kuwa atahakikisha anaibana serikali kutekeleza Ahadi zote zilizoahidiwa katika uchaguzi Mkuu wa 2010 na CCM.
Akizungumza na wananchi wa wilaya ya Kilombero mjini Ifakara Jana, Kinana alisema bado kuna Ahadi nyingi ambazo zipo Kwenye hatua za utekelezaji na kwamba bila kuwepo kwa msukumo mkubwa na usimamizi aw karibu, utekelezaji wake utasuasua.
Alisema katika Siku tatu za kwanza za ziara yake ya siku nane Mkoani Morogoro amepata fursa ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ikiwemo ile ya Daraja la Kilombero, miradi ya usambazaji umeme na ule wa Ujenzi we Barabara ya Kilombero, ulama Mpaka Wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.
"Miradi Hii ni mingi, na inatumia fedha nyingi za walipa kodi, hivyo ni lazima kufanya kila namna ili kuifanya iwe na tija katika maisha ya watanzania, kwa kusaidia kukuza Mapato yatokanayo na shughuli zao za kiuchumi" alisema Kinana.
Katibu Mkuu huyo aw CCM alisisitiza kuwa CCM bado imara na kwamba kasi yake katika usimamizi wa serikali zake unadhihirisha utekelezaji wa wakati wa Ahadi zake za 2010.